Tuesday, June 20, 2017

FIFA WATETEA MFUMO VAR.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetetea matumizi ya mfumo wa picha za video kumsaidia mwamuzi-VAR katika michuano ya Kombe la Shirikisho wakidai kuwa teknologia hiyo ni kwajili ya soka lijalo. Mfumo huo umeshatumika mara tano mpaka sasa katika michuano hiyo inayoendelea nchini Urusi, na kusababisha mkanganyiko miongoni mwa mashabiki. Rais wa FIFA, Gianni Infantino amesema tumeona jinsi gani mfumo huo unavyosaidia waamuzi kufanya maamuzi sahihi. Infantino aliongeza kuwa anafurahia jinsi VAR inavyofanya kazi mpaka sasa katika michuano hiyo. Mfumo wa VAR ulianza kutambulishwa rasmi kwa mara ya kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA iliyofanyika Japan Desemba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment