Thursday, June 15, 2017

HUDDERSFIELD YAANZA USAJILI KWA KISHINDO.

KLABU ya Huddersfield iliyopanda Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu imekubali kutoa ada ilitakayovynja rekodi ya klabu hiyo ya paundi milioni 10 kwa ajili ya kiungo wa kimataifa wa Australia Aaron Mooy kutoka Manchester City. Mooy mwenye umri wa miaka 26 aliitumikia Huddersfield kwa mkopo msimu uliopita na alicheza pia mchezo wa mwisho wa mtoano dhidi ya Reading ambao walishinda na kujihakikishia nafasi ya kukwea Ligi Kuu. Taarifa zinadai kuwa Huddersfield watatoa kitita cha paundi milioni nane awali na paundi milioni mbili zilizobaki watalipa baadae. Mooy alijiunga na City akitokea klabu ya Melbourne City miezi 12 iliyopita kwa mkataba wa mitatu.

No comments:

Post a Comment