Monday, June 19, 2017

KOCHA WA CHILE ALAUMU MFUMO WA VAR.

KOCHA wa timu ya taifa ya Chile, Juan Antonio Pizzi anadhani mfumo wa matumizi wa picha video kumsaidia mwamuzi-VAR uliwaathiri wachezaji wake na kufanya kupata tabu kuwafunga Cameroon katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho uliochezwa jana usiku. Mabingwa wa Amerika Kusini walishuhudia bao zuri la Eduardo Vargas katika kipindi cha kwanza likikataliwa baada ya mfumo huo wa VAR kutumika na kuonekana kuwa alikuwa ameotea. Hata hivyo, baadae Vargas alinufaika baada ya VAR kukataa maamuzi ya mshika kibendera na kuamua kuwa Alexis Sanchez alikuwa hajaotea wakati akitengeneza mazingira ya bao la pili. Bao hilo la Vargas liliifanya Chile kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ambapo la kwanza lilifungwa na Alex Vidal aliyemalizia pasi safi ya Sanchez. Pizzi amesema anadhani mfumo huo unahitaji muda kwani hata wachezaji wake walionekana kuathirika kwa kiasi fulani.

No comments:

Post a Comment