Thursday, June 15, 2017

JUVENTUS YAPELEKA NGUVU KWA COSTA BAADA YA KUMNASA N'ZONZI.

MENEJA wa Juventus, Massimiliano Allegri amethibitisha kuwa klabu hiyo inataka kumsajili winga wa Bayern Munich Douglas Costa. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil hana furaha Bayern baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza katika siku za karibuni na kukiri kuwa anafikiria kuondoka. Akizungumza na wanahabari, Allegri amesema Douglas Costa yuko katika mipango yao ya usajili kwani ni mchezaji mzuri lakini hakuna lolote liliafikiwa mpaka sasa. Wakati huohuo kluna taarifa kuwa kiungo wa Sevilla Steven N’Zonzi amekubali kujiunga na klabu hiyo kipindi hiki cha majira ya kiangazi. N’Zonzi ambaye alikuwa akihusishwa na tetesi za kuwaniwa na Barcelona, amekuwa akicheza kwa kiwango kikubwa msimu uliopita chini Jorge Sampaoli kwa kufunga mabao matatu katika mshindano yote na kusaidia mengine matatu.

No comments:

Post a Comment