Thursday, June 15, 2017

PSG WAKIRI KUMUWINDA MBAPPE.

MENEJA wa Paris Saint-Germain-PSG, Unai Emery amemtaka mshambuliaji wa AS Monaco Kylian Mbappe kusajiliwa na klabu yake. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 18, amekuwa akiwani klabu mbalimbali barani Ulaya huku dau lake likidaiwa kufikia euro milioni 120. Klabu za Real Madrid na Arsenal zimekuwa zikipigana vikumbo kuwania kumsajili chipukizi huyo lakini Emery amekiri kuwa anataka mchezaji ahamie PSG. Akizungumza na wahabari, Emery amesema ukimzungumzia Mbappe nchini Hispania lazima utazitaja klabu za Real Madrid na Barcelona lakini kwakuwa yeye anafundisha PSG angependa nyota huyo aiwakilishe timu yake. Emery aliendelea kudai kuwa pamoja na kluiheshimu Monaco lakini anadhani Mbappe anastahili kwenda PSG kwani familia yake iko kule na pia alianza katika akademi ya huko.

No comments:

Post a Comment