Monday, June 19, 2017

IBRAHIMOVIC ANA OFA KIBAO - RAIOLA.

WAKALA Mino Raiola amesema mteja wake Zlatan Ibrahimovic angekuwa tayari amesharejea AC Milan kama Adriano Galliano angekuwa katika klabu hiyo, lakini amesisitiza nyota huyo ana ofa kibao mezani za kuchagua. Ibrahimovic amekuwa mchezaji huru baada ya kuachwa na Manchester United wakati akiendelea kujiuguza jeraha la goti alilopata Aprili mwaka huu. Ingawa nyota huyo mwneye umri wa miaka 35 atakuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa, tayari ameshahusishwa na tetesi za kuwaniwa na klabu mbalimbali ikiwemo suala la kurejea Italia. Kwa mujibu wa wakala wake Inter, Juventus na Milan zote zingeweza kuwa chaguo lake. Raiola amesema Ibrahimovic anaendelea vyema hivi sasa na ameshapokea ofa nyingi kutoka Marekani na sehemu nyinginezo.

No comments:

Post a Comment