Thursday, June 22, 2017

JUVENTUS MBIONI KUNASA MSHAMBULIAJI WA SAMPDORIA.

KLABU ya Juventus inatarajia kukamilisha usajili wa Patrik Schick wa euro milioni 25 kutoka Sampdoria baada ya nyota huyo kuwasili jijini Turin kwa ajili ya vipimo vya afya leo. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amefunga mabao 11 katika mechi 32 za Serie A alizoichezea Sampdoria toka alijiunga nao kwa kitita cha euro milioni nne akitokea Sparta Prague. Ingawa nyota huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech alikuwa na mkataba na Sampdoria unaomalizika mwaka 2020, lakini kwa kipindi kirefu amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwaniwa na klabu kadhaa zikiwemo Juventus, Inter na Tottenhma Hotspurs. Mapema hivi karibuni alikiri kuwa upo uwezekano wa kuhamia Juventus na sasa suala hilo linaonekana kukaribia kukamilika.

No comments:

Post a Comment