Thursday, June 22, 2017

TIMU YA SOKA YA CHINA KUCHEZA LIGI UJERUMANI.

Ligi Daraja la Nne nchini Ujerumani, inatarajiwa kufanya jambo la kipekee msimu ujao kwa kuongeza timu kutoka China kuwa miongoni mwa timu 20 zitakazoshiriki ligi hiyo. Chama cha Soka cha Ujerumani-DFB kilifikia makubaliano nawashirika wao Chama cha Soka cha China-CFA Novemba mwaka jana kuhusu mpango huo. Makamu wa rais wa DFB, Ronny Zimmermann alikaririwa na jarida la Kicker akidai kuwa klabu zote zinazoshiriki ligi hiyo zimekubaliana na mpango huo. Timu hiyo kutoka China itakuwa sio klabu badala yake itakuwa ni kundi la wachezaji walio chini ya umri wa miaka 20. Timu hiyo haitarajiwi kuwa na uwanja wake wa nyumbani na haijawekwa wazi wataweka kambi yao wapi ingawa kila klabu inatarajiwa kucheza mechi mbili za nyumbani dhidi yao. Timu hiyo itakuwa ikicheza nje ya mashindano kwa maana kuwa hawataweza kupandishwa daraja wala kushushwa.

No comments:

Post a Comment