Thursday, June 22, 2017

JUVENTUS YAKIRI KUPOKEA OFA YA SANDRO.

KLABU ya Juventus imedai kupokea ofa kubwa kwa ajili ya Alex Sandro na hawatamzuia beki huyo wa kushoto kuondoka katika timu hiyo kama akitaka. Mabingwa wa Ligi Kuu Chelsea wamekuwa wakihusishwa na tetesi za kumuwania beki huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 26. Meneja wa Chelsea, Antonio Conte alikuwa akiinoa Juventus wakati walipomsajili Sandro kwa kitita cha paundi milioni 23 kutoka FC Porto mwaka 2015. Ofisa mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta amesema kama mchezaji ataamua kuondoka hawawezi kumzuia. Sandro alikuwepo katika kikosi cha Juventus kilichofungwa katika hatua ya fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment