Monday, June 19, 2017

KIPA WA AC MILAN ATISHIWA KUUAWA.

WAKALA maarufu Mino Raiola amedai kuwa kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma ametumia vitisho vya kuuwawa wakati wa majadiliano ya nyongeza ya mkataba. Mapema wiki iliyopita mvutano ulikuwa mkubwa baada ya Milan kutangaza kuwa kipa huyo mwenye umri wa miaka 18 ameamua kutoongeza mkataba mwingine mpya zaidi ya ule wa awali unaomalizika mwaka 2018. Taarifa zinadai kuwa kipa huyo anayedaiwa kuwa na kipaji cha kipekee alikataa ofa ya mshahara wa euro milioni tano kwa mwaka jambo ambalo lilizua hisia mbaya miongoni mwa mashabiki wa timu hiyo. Akizungumza na wanahabari, Raiola amesema Donnarumma ametishiwa na familia yake imetishiwa hivyo hadhani kama mchezaji huyo ataendelea kubaki Milan. Raiola aliendelea kudai kuwa uongozi wa Milan ulikosea jinsi ya kujadili nyongeza ya mkataba na kipa huyo ndio maana hali imekuwa hivyo.

No comments:

Post a Comment