MABINGWA wa Afrika, Cameroon jana wameondoshwa katika michuano ya Kombe la Shirikisho inayoendelea nchini Urusi kwa kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa mabingwa wa dunia Ujerumani kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B. Katika mchezo huo Cameroon walijikuta wakimaliza pungufu kufiatia nyota wao Ernest Mabouka kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Emre Can. Hata hivyo pamoja na kuomba usaidizi wa mfumo wa matumizi ya picha za video, mwamuzi wa mchezo huo Wilmar Roldan kutoka Colombia alitoa kadi kwa mchezaji asiye sahihi mpaka aliposisitizwa kurudia mara ya pili ndio akatoa kadi kwa mchezaji stahili. Katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo Ujerumani wanatarajiwa kupambana na Mexico huku mabingwa wa Ulaya Ureno wao wakicheza na mabingwa wa Amerika Kusini Chile mechi zitakazofanyika huko Sochi.
No comments:
Post a Comment