Monday, June 26, 2017

STARS WAANZA VYEMA COSAFA.

TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeanza vyema michuano ya Kombe la COSAFA baada ya kuididimiza kwa mabao 2-0 Malawi kwenye mchezo wa kundi A uliochezwa jana katika Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini. Mabao mawili yaliyofungwa na kiungo Shiza Ramadhani Kichuya katika dakika ya 13 na 18 yalitosha kuihakikishia Stars ushindi huo muhimu kwenye mchezo huo. Stars sasa inaongoza kundi A kwa kujikusanyia alama tatu sambamba na Angola ambao nao walishinda bao 1-0 dhidi ya Mauritius jana. Timu moja pekee ndio itafuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambapo watakwenda kukutana na Botswana, Zambia, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland zilizofuzu hatua hiyo moja kwa moja. Kesho Stars inatarajiwa kupambana na Angola wakati Malawi wao watachuana na Mauritius kwenye mchezo mwingine wa kundi B.

No comments:

Post a Comment