WAENDESHA mashitaka nchini Hispania wamekubali kubadilisha kifungo cha miezi 21 jela alichohukumiwa Lionel Messi kwa kosa la kukwepa kodi kwa kuamua kumtoza faini. Nyota huyo wa kimataifa wa Barcelona alipewa kifungo hicho Julai mwaka jana aada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu ya kukwepa kodi sambamba na baba yake Jorge. Mahakama iliamua kuwa Messi kati ya mwaka 2007 na 2009 alikwepa kodi ya kiasi cha euro milioni 4.1 kutokana na mapato yake ya haki ya matumizi ya picha zake. Rufani kupinga adhabu hiyo ilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu nchini Hispania Mei mwaka huu. Hata hivyo, taarifa zinadai kuwa waendesha mashitaka wamekubali kubadili kifungo hicho kwa faini ya euro 255,000.
No comments:
Post a Comment