Thursday, June 22, 2017

OSCAR AFUNGIWA MECHI NANE KWA VURUGU CHINA.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea, Oscar amefungiwa kutocheza mechi nane na Chama cha Soka cha China-CAF kufuatia kuzusha vurugu katika mchezo ambao timu yake ya Shanghai SIPG ilitoka sare ya bao 1-1 Jumapili iliyopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, alipiga mpira kwa makusudi kuwalenga wachezaji wawili wa Guangzhou R&F na kusababisha tafrani kubwa kati ya wachezaji wa timu zote mbili. Oscar sasa anatarajiwa kutumikia adhabu hiyo mpaka Agosti 13 huku pia akitozwa faini ya dola 5,000 kutoka tukio hilo. Awali CFA walikuwa hawafamu ni jinsi gani haswa kumuadhibu kiungo huyo na walilazimika kuliandikia Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kuwaomba ushauri kutokana na tukio hilo. Oscar ameichezea SIPG mechi 21 na kufanikiwa kufunga mabao manne na kusaidia mengine 10.

No comments:

Post a Comment