Wednesday, June 14, 2017

ROMA YAMCHUKUA DI FRANCESCO.

KLABU ya AS Roma imetangaza kumteua Eusebio di Francesco kuwa meneja wao mpya kwa mkataba wa miaka miwili. Meneja huyo mwenye umri wa miaka 47 raia wa Italia, anachukua nafasi ya Luciano Spalletti ambaye alijiuzulu mwishoni mwa msimu huu na kwenda kuwa meneja wa Inter Milan. Di Francesco ambaye aliisaidia Roma kutwaa taji la Serie A msimu wa 2000-2001 wakati huo akicheza nafasi ya kiungo, amesema amefurahi kurejea katika klabu hiyo baada ya kupita miaka mingi. Di Francesco aliisaidia Sassoulo kupanda katika Serie A mwaka 2013 na msimu uliopita aliiwezesha kushika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi. Roma ambao wamemsajili beki wa Mexico Hector Moreno kutoka PSV Eindhoven hivi karibuni, walimaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita na wanatarajiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment