Wednesday, October 5, 2011

TFF KUVISHITAKI VILABU VYA NJE FIFA.

DAR ES SALAAM, Tanzania
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) LEODGAR CHILA TENGA amesema wanatarajia kuwasilisha malalamiko yao katika shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA juu wa vilabu kutoka nje ya Nchi  kushindwa kuwaruhusu wachezaji kuja kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars pindi wanapohitajika.

Hatua hiyo imekuja kufuatia timu ya Vancouver Whitecapes ya Canada  anayoichezea Nizer Khalfan pamoja na timu ya DT LONG kutoka nchini Vietnam anayoichezea DANNY MRWANDA kushindwa kuwaruhusu wachezaji wake  kuja kujiunga na Stars.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo TENGA amesema imekuwa ni kawaida kwa timu hizo  kuwazuia wachezaji wao kuja kujiunga na Stars mara wanapokuwa wanahitajika hivyo wameamua kuwasilisha malalamiko yao FIFA.

Katika hatua nyingine Stars itawakosa wachezaji VICTOR COSTA pamoja na JUMA NYOSO kutokana na kukabiliwa na maumivu.

Kocha mkuu wa Stars JAN PAULSEN amesema NYOSO anasumbuliwa na ugonjwa wa malaria huku COSTA akikabiliwa na maumivu ya nyonga hivyo kuwalazimu kubakiia nchini kwa matibabu zaidi.

Tayari Stars imemkosa nahodha na mlinzi namba moja wa timu hiyo SHADRACK NSAJIGWA kutokana na kuwa majeruhi.

Timu hiyo inatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea nchino Morocco kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo.

MAN CITY KUMFUNGIA TEVEZ WIKI SITA.

LONDON, England
KLABU ya Manchester City itamfungia kwa muda wa wiki sita pamoja na faini ya Paundi milioni 1.5 mchezaji Carlos Tevez hata kama katika utetezi wake itaonekana hakukataa moja kwa moja kucheza katika baina ya timu hiyo na Bayern Munich.

City wanaamini kuwa kukataa kwa Tevez kuendelea kupasha misuli ili kujiandaa kuingia ndani ni ushahidi tosha kwa adhabu hiyo.

Klabu hiyo imeamua kuchukua ushauri wa kisheria na kujaribu kupeleka kesi hiyo kwa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) kuonyesha kwamba Tevez anastahili adhabu zaidi ya aliyopewa ya kusimamishwa wiki mbili na kutozwa faini ya paundi 500,000.

Kama itakuwa hivyo, City wako tayari kutumia kauli aliyoitoa baada ya mchezo huo wakati akihojiwa na luninga ya Sky Sports ambapo alisema. "Nilikuwa sijisikii kucheza ndio maana sikucheza."

Mahojiano hayo yanachanganyana na kauli aliyoitoa siku moja baada ya mchezo huo ambapo alisema hakukataa kucheza.

Kocha wa klabu hiyo Roberto Mancini anataka mchezaji huyo awekwe katika orodha ya wachezaji wataouzwa atamruhusu kufanya mazoezi na kikosi cha akiba mchana.

ADEBAYOR AUMIZWA NA MASHABIKI WA ARSENAL WALIVYOKUWA WAKIMTUKANA.

LONDON, England
MCHEZAJI wa Tottenham Hotspurs Emmanuel Adebayo amekiri ameumizwa na kitendo cha mashabiki wa Arsenal jinsi walivyokuwa wakimtukana wakati wa mchezo ulizikutanisha timu hizo zinazotoka Kaskazini mwa London wiki iliyopita.

Mashabiki wa Arsenal walisikika wakiimba nyimbo zenye mfano wa milio ya risasi kukumbushia tukio la kuvamiwa walilopata timu ya Taifa ya Togo wakati wakielekea katika michuano ya Kombe la Afrika (CAN) mwaka uliopita, tukio ambalo Adebayo alipoteza marafiki zake watatu.

Lakini Adebayor (27) anayecheza kwa mkopo katika klabu hiyo, ambaye aliondoka Arsenal kuelekea Manchester City mwaka 2009 alisema wimbo waliokuwa wakiimba mashabiki hao haukumshangaza ila ulimhuzunisha.

"Ni wazi kwamba walikuwa wanataka kuniumiza, kunicharua na kunitia hasira. lakini nashukuru nilitunza heshima yangu mbele ya nyuso za mashabiki hao.

MAN UNITED KLABU YA SOKA TAJIRI DUNIANI.

KLABU ya Manchester United ya England imeendelea kuwa namba moja katika listi ya klabu ya soka tajiri duniani lakini ikishuka na kuwa namba 2 katika listi ya jumla ya vilabu tajiri vya michezo duniani kwa mujibu wa jarida maarufu na linaloheshimika duniani “THE FORBES MAGAZINE”.

United ambao walikuwa wanatop listi ya vilabu tajiri duniani kwa takribani miaka 4 iliyopita lakini sasa wamepitwa na klabu ya mchezo wa Baseball ya nchini Marekani, New York Yankees kutokana na kuimarika kwa dola ya Marekani dhidi ya paundi ya Uingereza.

Pamoja na kutokuwa na wakati mzuri katika ligi Arsenal ndio klabu nyingine pekee ya EPL iliyopo kwenye top 10 ya vilabu tajiri vya michezo duniani.

The Forbes top ten:

1 - New York Yankees (Baseball) - $340m
2 - Manchester United - $269m
3 - Real Madrid - $264m
4 - Dallas Cowboys (NFL) - $193m
5 - Bayern Munich - $179m
6 - Boston Red Sox (Baseball) - $173m
7 - Barcelona - $172m
8 - Arsenal - $158m
9 - AC Milan - $147m
10 - New England Patriots (NFL) - $146m

Monday, October 3, 2011

NSAJIGWA KUIKOSA MOROCCO.

NAHODHA wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa ameumia nyonga (groin) kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana (Oktoba 3 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa daktari wa Taifa Stars, Dk. Mwanandi Mwankemwa, maumivu hayo yatamweka Nsajigwa ambaye pia ni Nahodha wa Yanga nje ya uwanja kwa kati ya wiki mbili hadi nne.

Kutokana na ushauri wa daktari, Kocha Jan Poulsen amemuondoa kwenye kikosi hicho ambacho kitasafiri Oktoba 6 mwaka huu kwenda Casablanca, Morocco kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Oktoba 9.

Badala yake Kocha Poulsen amemuita kwenye timu yake Nassoro Masoud Said ‘Cholo’ wa Simba kuziba nafasi ya beki huyo wa pembeni.

Wakati huohuo wachezaji wanaocheza nje ya nchi walioitwa na Kocha Poulsen wameanza kuwasili. Idrissa Rajab anayechezea Sofapaka ya Kenya na Mbwana Samata wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili jana jioni na tayari wameripoti kambini Taifa Stars.

Henry Joseph wa Kongsvinger IL ya Norway), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) wanatarajiwa kuwasili leo (Oktoba 3 mwaka huu) usiku kwa ndege ya KLM.

Washambuliaji Abdi Kassim na Dan Mrwanda wanaochezea timu ya DT Long An ya Vietnam ndiyo watakaokuwa wa mwisho kujiunga na kambi ya Stars ambapo watawasili nchini kesho (Oktoba 4 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Qatar Airways.

Sunday, October 2, 2011

ESPERANCE YAJIWEKEA MAZINGIRA MAZURI YA KUTINGA FAINALI ORANGE CAF CHAMPIONS LEAGUE.

Wachezaji wa Esperance wakishangilia bao pekee katika mchezo huo dhidi ya Al Hilal ya  Sudan mchezo ulichezwa Jumapili.

TIMU ya Esperance ya Tunisia wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika kwa pili mfululizo baada ya kuifunga kwao Al Hilal ya Sudan kwa bao 1-0 Jumapili.

Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo unatarajiwa kuchezwa katikati ya mwezi Octoba jijini Tunis na matokeo yoyote ya sare yataivusha katika hatua ya fainali Esperance, ambao bado wanauguza kidonda cha kufungwa jumla ya mabao 6-1 katika hatua ya fainali dhidi ya TP Mazembe ya DRC msimu uliopita.

Kiungo wa pembeni wa esperance Youssef Msakni ndio aliyefunga bao hilo pekee katika Uwanja wa Al Hilal, Omdurman dakika ya nne baada ya mpira kuanza.

Hilo ni bao la nne kwa Msakni (20) katika mashindano hayo msimu huu, lakini ni la kwanza toka alipoifungia timu yake hiyo bao mwezi Aprili wakati alipochangia bao moja katika ushindi  wa mabao 5-0 uliyopata timu yake dhidi ya timu ya Senegal ya Diaraf Dakar.

Kwa kawaida Al Hilal ni wazuri zaidi wakiwa nyumbani kuliko ugenini hivyo watakuwa na wakati mgumu kuvuka hatua hiyo ya nusu fainali kwa mara ya tatu ndani ya miaka mitano.

Wydad Casablanca ya Morocco ikiwa nyumbani ilishinda bao 1-0 dhidi ya Enyimba ya Nigeria katika mchezo mwingine wa nusu fainali ya michuano hiyo uliochezwa Jumamosi, bao ambalo lilifungwa na Pascal Angan kwa mpira wa adhabu dakika moja kabla ya kulia kwa kipenga cha mwisho.

Fainali za michuano hiyo zinatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa Novemba mwaka huu ambapo kati ya Wydad au Enyimba ndio watakuwa wenyeji katika mchezo wa kwanza kushindania zawadi ya dola milioni 1.5 (bilioni 17) pamoja na tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ya dunia itakayofanyika Japan, mwishoni mwa mwaka huu.

ARSENAL YAENDELEA KUSUASUA, CHELSEA YANG'AA.

Add caption

LONDON, England
KATIKA Ligi Kuu ya Uingereza Arsenal imekubali kipigo cha nne katika ligi hiyo nyumbani kwa mahasimu wao Tottenham wakati mabao matatu ya Frank Lampard yaliisaidia timu yake ya Chelsea kuifunga Bolton katika mchezo uliochezwa Jumapili jioni.

Wachezaji Rafael van der Vaart na Kyle Walker ndio walioihakikishia Tottenham ushindi dhidi ya mahasimu wao Arsenal ambao iko mbili tu juu ya mstari wa kushuka daraja baada ya kucheza mechi saba.

Katika mchezo huo pia Arsene Wenger alipata pigo baada ya beki wake wa kushoto Bacary sagna kuumia mfupa wa ugoko, ambapo anatarajiwa kuwa nje ya dimba miezi mitatu.

Chelsea ni ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo baada lampard kuonyesha ubora wake katika Chelsea katika ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu inayoburuza mkia ya Bolton.

Matokeo mengine katika ligi hiyo kwenye michezo iliyochezwa jana ni kama ifuatavyo.

Bolton                1-5 Chelsea
Fulham   6-0 QPR
Swansea City 2-0 Stoke City
Tottenham 2-1 Arsenal