Tuesday, October 11, 2011

POULSEN: TUMEFUNGWA NA TIMU BORA.

KOCHA wa timu ya Taifa "Taifa Stars" Jan Poulsen amesema tofauti ya ubora wa viwango ndio chanzo kikubwa cha timu hiyo kufanya vibaya katika mchezo wake dhidi ya Morocco.

Poulsen alizungumza hayo leo asubuhi wakati kikosi cha Stars kilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, kwa ndege ya Shirika la Ndege Qatar.

Amesema timu hiyo ilionyesha kiwango kizuri katika mchezo huo ndio maana mpaka wanakwenda mapumziko walikuwa wako nguvu sawa kwa kufungana bao 1-1, kabla ya kipindi cha pili ambapo tulizidiwa mbinu kidogo na kujikuta tukifungwa bao la pili kabla ya kumalizia la tatu dakika za lala salama.

"Wakati mwingine mashabiki wa soka hapa nchini wanasahau kuwa timu yetu "Stars" iko katika nafasi ya ngapi kwa ubora wana viwango vya Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) ukilinganisha na Morocco tuliocheza nao." alisema Poulsen wakati akihojiwa na waandishi wa habari uwanjani hapo.

Amesema kwasasa wanajipanga kwa ajili ya mchezo dhidi ya Chad ili waweze kufanikiwa kuingia katika hatua ya makundi kwa michezo yakutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Dunia litalofanyika nchini Brazil 2014.

Stars inabidi ipigane kufa na kupona kushinda mchezo dhidi ya Chad ili kupata nafasi hiyo, kwani wakishindwa mchezo huo timu hiyo itakosa nafasi kama hiyo kwa muda wa miaka miwili, na kama wakifanikiwa basi itajiunga timu zingine katika kundi C ambazo ni Gambia, Morocco na Ivory Coast ambazo zenyewe zilipita moja kwa moja kwa viwango vizuri katika orodha ya FIFA.

Monday, October 10, 2011

ROONEY KUKALIA BENCHI EURO 2012.

Wayne Rooney akimkwatua Miodrag Dzudovic wa Montenegro.
Miodrag Dzudovic
KOCHA wa Uingereza Fabio Capello amemuonya Wayne Rooney kuwa anaweza kukalia benchi katika kipindi cha michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2012).

Capello sasa anapanga mikakati madhubuti kwa ajili ya michuano hiyo huku akijua Rooney ambaye pia ni mshambualiaji wa Manchester United atakosa kama sio mchezo mmoja basi itakuwa miwili kufuatia kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo dhidi ya Montenegro.

Na alimwambia mshambualiaji huyo kama aina mpya ya mchezo atakaoutumia utafanya kazi atalazimika kumuondoa katika kikosi cha kwanza hata kama hatafungiwa.

Capello tayari amemuondoa Rooney katika kikosi chake kitakachocheza mchezo wa kirafiki na Hispania katika Uwanja wa Wembley mwezi ujao kwasababu anataka kuanza mikakati yake mara moja.

Amesema bado atamchukua Rooney katika michuano hiyo. Lakini "Nahitaji kutafuta mbadala wa Rooney katika mchezo mmoja au miwili ambayo hatacheza. Na kama nikipata basi atalazimika kupigania kurudi katika kikosi cha kwanza." alisema Capello.

"Katika maisha yangu kama kocha nimeshawaweka benchi wachezaji wengi wazuri. Nitakwenda na Rooney katika michuano hiyo ya Ulaya, ndio. nadhani atafungiwa mchezo mmoja tu."

Maamuzi ya adhabu ya mchezaji huyo yanatarajiwa kutolewa na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) wiki hii.

FAINALI ZA EURO 2012 KUCHEZWA UWANJA HUU.


Mashabiki wakiingia uwanjani muda mfupi kabla ya kuanza kwa sherehe hizo.
MASHABIKI wa Soka wapatao 70,000 wa nchini Ukraine Jumamosi hii wamepata nafasi ya kushuhudia uzinduzi wa Uwanja wa Olimpiki uliopo Kiev.
Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 70,000 waliokaa na Rais wa nchi hiyo Viktor Yankuovich ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Ulaya itakayochezwa 2012.
"Kwa Uwanja huu Ukraine itaandaa mashindano ya Ulaya yenye mafanikio," alisema Yankuovich akihutubia mashabiki hao walioonekana hawana furaha kufuatia tuhuma zinazomkabili Rais huyo.

Shakira akiwajibika katika uzinduzi wa Uwanja huo.
Hatahivyo hali hiyo ilibadilika ghafla pale mwanamuziki nguli wa muziki wa Pop Shakira kuliteka jukwaa na kuimba kwa dakika 40, ikiwemo wimbo maalumu wa Kombe la Dunia 2010 uitwao Waka Waka, ikifuatiwa na ufyatuaji wa mafataki na hotuba kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Ukraine, Hryhoriy Surkis.
"Uwanja huu umefanyiwa ukarabati katika kiwango cha hali ya juu. Utakuwa mmoja kati ya viwanja kumi bora Ulaya, ni ukweli kwamba kila kitu hapa kimetengenezwa kwa teknologia ya hali ya juu kitu ambapo sio tu kitatumiwa kwa ajili ya mpira bali hata riadha." alisema Surkis akiusifia uwanja huo.
Uwanja huo ambao umegharimu Euro milioni 585 na umekuwa katika matengenezo toka Desemba 2008, utatumiwa kwa mechi tano ukiwemo mchezo wa fainali utakaochezwa July 1 2012, katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ambapo Ukraine kwa kushirikiana na Poland ndio watakuwa wenyeji wa michuano hiyo.
Uwanja pia utachezwa mchezo wake wa kwanza November 11 mwaka huu wakati timu ya taifa ya nchi hiyo itapoikaribisha Ujerumani katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Sunday, October 9, 2011

TANZANIA NAYO YATOLEWA AFCON.

MARRAKECH, Morocco
TIMU ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" imetolewa katika kinyang'anyiro cha kutafuta tiketi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Morocco mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Grand jijini Marrakech, Morocco. Jumapili jioni.

Morocco ndio waliokuwa wa kwanza kuona lango la Stars baada ya mshambuliaji wake machachari anayechezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Maroune Chamakh kuipa timu yake bao la kuongoza dakika ya 20 kutoka mpira kuanza.

Bao hilo la Morocco liliongeza kasi kwa wachezaji wa Stars ambao mara kwa mara walikuwa langoni mwa wenyeji wao hao, juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 40 baada ya Abdi Kassim "Babi" kuisawazishia Stars bao hivyo kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambualiana kwa zamu lakini ilikuwa ni Morocco ndio waliandika bao la pili kwa mpira wa adhabu dakika ya 68 kupitia kwa mchezaji wake Adel Taarabt kabla timu hiyo kuongeza bao la tatu dakika 89 hivyo kuzima ndoto za Stars kushiriki michuano hiyo itakayofanyika kwa ushirikiano baina ya Equatorial Guinea na Gabon 2012.

Kwa matokeo hayo Morocco inaungana na timu za Gabon, Equatorial Guinea ambao ndio waandaaji, Niger, Angola, Botswana, Ivory Coast, Ghana, Guinea, Mali, Senegal, Tunisia, Zambia, Burkina Faso, Sudan and Libya kuunda timu 16 zitakazoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika 2012.

Saturday, October 8, 2011

Argentina Vs Chile (4-1) Eliminatorias Mundial Brasil 2014

NIGERIA YAUNGANA NA CAMEROON NA MISRI KUTOLEWA KATIKA MICHUANO YA AFCON 2012.

AFCON 2012
ANGOLA, Ghana, Guinea, Libya na Zambia zimekata tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika 2012 Jumamosi hii wakati Nigeria wakitolewa katika kinyang'anyiro hiyo baada ya kukubali bao la kusawazisha lilifungwa dakika za mwisho dhidi ya timu ya Guinea.

Mabao ya mapema yaliyofungwa na Asamoah  Gyan na John Mensah yaliisaidia Ghana kuibuka na ushindi dhidi ya Sudan na kupelekea kuongoza kundi lake kwa kuwa na pointi 16 katika michezo sita walizocheza.

Ibrahima Traore alisawazisha bao dakika ya mwisho ya mchezo na kuifanya timu yake kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi Nigeria katika mchezo uliokuwa wa kusisimua uliochezwa mjini Abuja. Guinea ndio walioanza kupata bao kupitia Ismael Bangura kabla ya Obinna Nsofor na Ikechukwu Uche kuifungia Nigeria.

Ni mara ya kwanza kwa Nigeria kutokushiriki michuano hiyo katika kipindi cha miaka 26 toka mwaka 1986.

Nigeria sasa wanaungana mabingwa wa zamani ambao nao wametolewa katika michuano hiyo ambao ni Cameroon na Misri.

Timu zilizojikatia tiketi ya kucheza michuano hiyo mpaka sasa ni Gabon, Equatorial Guinea ambao ndio waandaaji, Niger, Angola, Botswana, Côte d’Ivoire, Ghana, Guinea, Mali, Senegal, Tunisia, Zambia, Burkina Faso,  and Libya.

Michezo mingine ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika itachezwa leo ambao timu ya Taifa ya Tanzania itatupa karata yake ya mwisho itapomenyana na Morocco katika mji wa Marrakech jioni ya saa 1:30 kwa saa za kule ambapo huku itakuwa saa 4:30 usiku. Mungu Ibariki Taifa Stars Mungi Ibariki Tanzania.

AFCON 2012: MATOKEO YA JANA PAMOJA NA TIMU ZILIKATA TIKETI YA KUCHEZA MICHUANO HIYO.

Group A
In Monrovia
Liberia 2 (Williams Dioh 2, Patrick Wieh 90+2) - Mali 2 (Cheick Diabate 16, Cedric Kante 87)

In Praia
Cap Vert Islands 2 (Valdo 3, Ryan 13) - Zimbabwe 1 (Knowledge Musona 68-pen)

Group B
In Addis Ababa
Ethiopie 4 (Omodokwury Omod 31, Adane Girma Gebreyes 56, Fikru TeferraLemessa 59, Shimeles Bekele 73) - Madagascar 2 (Razafimanindry Tigana 3, Rakoto Nomenjanahary 57)

In Abuja
Nigeria 2 (Obinna Nsofor 64, Ikechukwu Uche 71) - Guinea 2 (Ismael Bangura 62, Ibrahima Traore 90)

Group C
In Chingola
Zambie 0 - Libya 0

In Maputo
Mozambique 3 ('Maninho' 6, Dario Monteiro 18, Elias 'Dominquez' Pelembe 39) - Comoros 0

Group E
 In Kinshasa
 RD Congo 2 (Alain Kaluyitukadioko 12, Deo Kanda 40) – Cameroon 3 (Samuel Eto'o 18, Matthew Andongcho Mbuta 75, Eric Maxim Choupo-Moting 79)

Group G
In Cairo
Egypt 3 (Omar Mohsen 48, 71, Mohamed Salah 56) - Niger 0
 
In Nelspruit
South Africa 0 - Sierra Leone 0

Group I
In Lobamba
Swaziland 0 - Congo Brazzaville 1 (Loris Nkolo 47)
 
In Omdurman
Sudan 0 - Ghana 2 (Asamoah Gyan 11, John Mensah 20)

Group J
In Bissau
Guinea Bissau 0 - Angola 2 ('Manucho' 8, 'Mateus' 70)

In Kampala
 Uganda 0 - Kenya 0

Group K
In  N'Djamena
Tchad 2 (Mahamat Labbo 65, Karl Max Barthelemy 90+4 - Malawi 2 (Robert Ngambi 35, Harry Vyranda 81)

In Rades
Tunisia 2 (Walid Hicheri 35, Saber Khelifa 79) - Togo 0

 Qualified teams: Gabon, Equatorial Guinea (co-hosts), Niger, Angola, Botswana, Côte d’Ivoire, Ghana, Guinea, Mali, Senegal, Tunisia, Zambia, Burkina Faso,  and Libya, which is confirmed as one of the two best second place team. The other second best placed team will be decided following matches to be played on 9/10/2011