Monday, September 3, 2012

FC Barcelona Vs Valencia 1-0 All Goals And Highlights [Sept.2 2012]

Real Madrid vs Granada 3-0 All Goals and Highlights 2/9/12

US OPEN: AZARENKA KUKWAANA NA BINGWA MTETEZI SAM STOUR KATIKA ROBO FAINALI.

MCHEZAJI tenisi anayeongoza katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake, Victoria Azarenka amefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika michuano ya wazi ya Marekani baada ya kumfunga Anna Tatishvili. Katika mchezo huo Azarenka alitumia muda wa dakika 82 kumsambaratisha Tatishvili kwa 6-2 6-2 ambapo sasa atakutana na bingwa mtetezi wa michuano hiyo Sam Stour kwenye hatua ya robo fainali. Maria Sharapova ambaye anashika namba tatu katika michuano hiyo naye alifanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kumuondosha Nadia Petrova 6-1 4-6 6-4. Sharapova atakutana na Mario Bartoli wa Ufaransa baada ya mchezaji huyo kumuondosha Petra Kvitova kwa 1-6 6-2 6-2. Kwa upande wa wanaume bingwa mtetezi wa michuano hiyo Novac Djokovic amefanikiwa kusonga mbele baada ya kumfunga kirahisi Julien Benneteau wa Ufaransa kwa 6-3 6-2 6-2 katika mzunguko wa tatu. Nyota mwingine wa mchezo huo Andy Roddick ambaye ametangaza kustaafu baada ya michuano hiyo amefanikiwa kumfunga Fabio Fognini ambapo sasa anatarajiwa kukutana na Juan Martin del Porto ambaye ni bingwa wa michuano hiyo mwaka 2009.

Saturday, September 1, 2012

Chelsea Vs Atletico Madrid 1-4 All Goals & Match Highlights 31-8-12 HD

CHELSEA WALINIOMBA NIMWACHE MATA - DEL BOSQUE.

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque ameweka wazi kuwa klabu ya Chelsea ilimuomba asimuite Juan Mata katika kikosi chake kwa ajili ya michezo miwili watakayocheza dhidi ya Saudi Arabia na Georgia. Mata alikuwemo katika kikosi cha Hispania kilichoshiriki michuano ya Kombe la Ulaya kabla ya kusafiri kwenda London kwa ajili ya michuano ya Olimpiki majira ya kiangazi na kocha huyo anadhani ni uamuzi sahihi wa kumpumzisha mchezaji katika kipindi hiki. Del Bosque pia amesema kuwa alipokea simu kutoka kwa kocha wa Bayern Munich ya Ujerumani Jupp Heynckes akimuomba kutomwita Javi Martinez kwani ana muda mfupi toka atue katika klabu hiyo hivyo anahitaji nafasi ili aweze kuzoea mazingira ya soka la huko. Mabingwa hao wa soka barani Ulaya na Dunia wanatarajiwa kupambana na Saudi Arabia katika mchezo wa kirafiki kabla ya kuanza mbio zao za kufuzu katika michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Georgia Septemba 10 mwaka huu.

JAPAN KUPEPETANA NA BRAZIL.

MABINGWA wa soka barani Asia Japan inatarajiwa kuchez mchezo wa kimataifa wa kirafiki na Brazil mchezo ambao utafanyika barani Ulaya, ikiwa ni mipango ya kocha wa Japan Alberto Zaccheroni ambaye anataka kujaribu kikosi chake na moja ya timu bora duniani. Chama cha Soka cha Japan-JFA kimesema kuwa kikosi cha nchi hiyo kitamenyana Brazil ambao ni mabingwa mara tano ya Kombe la Dunia jijini Wrocklaw, Poland Octoba 16 mwaka huu ikiwa ni siku nne baada ya kucheza na Ufaransa jijini Paris. Zaccheroni ambaye anapambana kuivusha Japan iweze kushiriki fainali zake nne za Kombe la Dunia mwaka 2014 amesema kuwa amefurahishwa na kupata michezo hiyo miwili migumu ya kirafiki. Michezo hiyo miwili itakuja kabla ya timu hiyo kumaliza mzunguko wake wa mwisho wa mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa bara ya Asia huku wao wakiwa wanaongoza kundi lao kwa alama saba baada ya kucheza michezo mitatu.

MADRID YAMCHUKUA ESSIEN KWA MKOPO.

KLABU ya Real Madrid ya Hispania imetangaza kufikia makubaliano ya kumnyakuwa kiungo wa Chelsea Michael Essien kwa mkopo katika kipindi chote cha msimu huu. Essien mwenye miaka ambaye alijiunga na Chelsea mwaka 2005 akitokea klabu ya Olympique Lyon ya Ufaransa anatua Madrid na kukutana na Jose mourinho ambaye amewahi pia kuinoa klabu hiyo ya Uingereza. Mchezaji huyop anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji akiwa na Chelsea amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu nchini humo, mataji manne ya Kombe la FA na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Essien hakuwemo katika kikosi cha Chelsea ambacho kilichabangwa mabao 4-1 na Atletico Madrid katika mchezo wa Super Cup uliochezwa jijini Monaco, Ufaransa jana usiku.