Thursday, December 20, 2012

UEFA CHAMPIONS LEAGUE DRAW.

Galatasaray v Schalke 04
Celtic v Juventus
Arsenal v Bayern Munich
Shakhtar Donetsk v Borussia Dortmund
AC Milan v Barcelona
Real Madrid v Manchester United
Valencia v Paris St Germain
Porto v Malaga

Wednesday, December 19, 2012

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.

SUALA LA AKINA MORRIS, CANNAVARO KWENDA KAMATI YA NIDHAMU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) ikieleza kuwafungia wachezaji kadhaa Wazanzibari wanaochezea klabu mbalimbali za timu za Tanzania Bara na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Suala hilo limepelekwa kwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF kwa hatua zaidi, hivyo kwa sasa Shirikisho litasubiri uamuzi wa kamati hiyo. Baadhi ya wachezaji hao ni nahodha msaidizi wa Taifa Stars, Aggrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nassoro Masoud Cholo, Mcha Khamis, Seif Abdallah na Selemani Kassim Selembe.

MTIBWA YAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA UHAI
Mtibwa Sugar imekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) kuzamisha African Lyon mabao 3-1. Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam, hadi mapumziko Mtibwa Sugar ilikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 22 na Hillary Kasela. Hassan Kabunda aliisawazishia African Lyon katika dakika ya 53. Mabao mengine ya washindi yalifungwa na Godfrey Mohamed dakika ya 64 na Juma Lazio akapachika la mwisho dakika ya 87. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar sasa itacheza mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Azam ambayo nayo leo asubuhi (Desemba 19 mwaka huu) iliilaza JKT Ruvu bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Chamazi. Bao la Azam lilifungwa dakika ya 46 na Mudathiri Yahya. Mechi hiyo ya kwanza ya nusu fainali itachezwa Ijumaa (Desemba 21 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Nusu fainali ya pili nayo itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 10 kamili jioni. Robo fainali ya tatu kati ya Oljoro JKT na Simba, na robo fainali ya nne zinachezwa leo saa 10 kamili jioni (Desemba 19 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Chamazi, Dar es Salaam. Mechi ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Jumapili (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

TANZANIA YAPAA VIWANGO FIFA.

TANZANIA imekwea kwa nafasi nne mpaka nafasi ya 130 katika viwango vya ubora duniani vinavyotolewa leo na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ambavyo ndio vitakuwa vya mwisho kwa mwaka 2012 huku ikishika nafasi ya 38 kwa upande wa Afrika. Katika orodha hizo Ivory Coast imeendelea kuongoza kwa upande wa Afrika kwa kukupanda nafasi moja mpaka nafasi ya 14 ikifuatiwa na Algeria waliopo katika nafasi ya 19 huku Mali wakiwa katika nafasi ya 25 baada ya kupanda kwa nafasi tatu. Nafasi ya nne kwa Afrika inashikwa na Ghana ambao wameporomoka kwa nafasi moja mpaka nafasi ya 30 wakifuatiwa na mabingwa wa Afrika Zambia ambao ndio wanafunga orodha ya tano bora, ambapo wamepanda nafasi nne mpaka nafasi ya 34. Kwa upande wa tano bora duniani Hispania bado wako katika nafasi ya kwanza wakifuatiwa na Ujerumani katika nafasi ya pili na Argentina nafasi ya tatu wakati nafasi ya nne inashikiliwa na Italia ambao wamepanda nafasi moja tofauti na mwezi uliopita. Nafasi ya tano katika orodha hizo inashikiliwa na Colombia ambao wamekwea kwa nafasi tano toka nafasi ya 10 waliyokuwepo mwezi uliopita huku mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia Brazil nao wakizidi kuporomoka mpaka nafasi ya 18 kutoka nafasi ya 13 walioyokuwepo mwezi uliopita.

MESSI ANASTAHILI BALLON D'OR - IBRAHIMOVIC.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSV, Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa Lionel Messi anastahili tuzo ya Ballon d’Or pamoja na kwamba mshambuliaji huyo wa Barcelona ameshashinda tuzo hiyo mara tatu mfululizo. Akihojiwa na gazeti moja nchini Ufaransa Ibrahimovic alimsifu Messi na kumfananisha kama mchezaji wa kwenye michezo ya luninga inayojulikana kama PlayStation na kudai kuwa anayeponda uwezo wa mchezaji huyo hajui mchezo wa soka. Ibrahimovic pia alisifu uwezo kiungo nyota wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuwa ni wa kipekee kwani pindi anapoingia uwanjani wachezaji wenzake wote hubadilika na kucheza vyema na kupelekea timu yao kupata matokeo mazuri. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alifika mbali na kudai kuwa hadhani kama kutatokea mchezaji wa aina ya Zidane huko mbele katika ulimwengu wa soka. 

Arsenal VS Reading 5 - 2 All Goals & Highlights Full HD 17/12/2012

Monday, December 17, 2012

BRAZIL YAZINDUA UWANJA WA KWANZA UTAKAOTUMIKA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA.

UWANJA wa Castelao Arena uliopo kaskazini-mashariki mwa Brazil katika mji wa Fortaleza umekuwa uwanja wa kwanza kukamilika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika nchini humo mwaka 2014. Sambamba na Uwanja wa Mineirao uliopo jijini Belo Horizonte ambao utafunguliwa Desemba 21 ndivyo vinakuwa viwanja pekee kukamilika kwa wakati kabla ya michuano ya Kombe la shirikisho itakayochezwa Juni mwakani. Rais wan chi hiyo Dilma Rousseff alihudhuria sherehe za ufunguzi wa uwanja wa Castelao ambao umekamilika kwa kutumia gharama za dola milioni 249 ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 67,000. Rousseff amesema kuwa kukamilika kwa uwanja huo kwa ajili ya michuano ya 2014 na ushindi wa timu ya Corinthians katika michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia jana unaonyesha jinsi gani Brazil ilivyokuwa na uwezo ndani na nje ya uwanja. Amesema nchi hiyo inauwezo wa kufanya vyote viwili kushinda mataji uwanjani na kujenga uwanja bora kama huo uliofunguliwa jana.

Barcelona Vs Atletico Madrid 4 - 1 All Goals & Highlights HD 16/12/2012