Monday, May 27, 2013
LEWANDOWSKI BAYERN INAMHUSU - WAKALA.
WAKALA wa mshambuliaji nyota wa klabu ya Borussia Dortmund, Robert Lewandowski amesema kuna uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo kujiunga na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Bayern Munich. Hata hivyo, wakala huyoaitwaye Cezary Kucharski aliiambia luninga moja nchini Ujerumani kwamba Bayern bado hawajafikia makubaliano ya mambo binafsi ya nyota huyo wa kimataifa wa Poland. Wakala huyo aliendelea kusema kuwa wao wako tayari lakini badi hawajasaini chochote kwasababu klabu nayo inatakiwa iafiki makubaliano hayo. Bayern ambao ni mabingwa wapya wa Ujerumani tayari wamemnyakuwa kiungo wa Dortmund Mario Gotze mwenye umri wa miaka 20 kwa ada ya euro milioni 37.
ZIDANE APEWA KIBARUA CHA KUHAKIKISHA BALE ANATUA MADRID.
MMOJA wa wachezaji bora kabisa kuwahi kuitumikia klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amepewa kazi ya kuhakikisha anamshawishi mshambuliaji nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Gareth Bale ili aweze kusajili na klabu hiyo. Gazeti la Marca nchini Hispania limeripoti kuwa nyota huyo wa zamani ndio mshauri mkuu kuhusiana na suala la Bale ana anajaribu kumshawishi raia wa Madrid Florentino Perez kuwa lazima waipate saini ya nyota huyo. Kwa kuonyesha kwamba hawataki mchezo kwenye suala hilo Madrid wamepania hata kutoa kitita cha paundi milioni 65 kwa ajili ya kumchukua Bale kutoka Spurs.
Zidane kwa kipindi kirefu amekuwa akimhusudu nyota huyo wa kimataifa wa Wales akidai kuwa amekuwa akiitazama Tottenham kwa ajili ya Bale ukiachilia mbali Ronaldo na Messi ambao ndio wachezaji anaowahusudu duniani kwa hivi sasa. Zidane ameendelea kufafanua kwa kummwagia sifa Bale kwamba ni mchezaji aliyekamilika na amekuwa akifunga mabao mazuri na muhimu ana kasi, mbunifu na anavutia kumtizama.
RIBERY AKIRI FURAHA ILIMFANYA KWENDA NALO KITANDANI KOMBE LA LIGI YA MABINGWA ULAYA.
WINGA machachari wa klabu ya Bayern Munich, Franck Ribery amebainisha kuwa alichukua Kombe la Ligi ya Mabingwa na kwenda nalo kitandani kufuatia ushindi wa timu yao wa mabao 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund. Bayern wamefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo mara tatu katika kipindi cha miaka minne lakini walifanikiwa kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza toka mwaka 2001 kwa ushindi waliopata katika Uwanja wa Wembley Jumamosi. Na Ribery alibainisha hilo katika sherehe za kulitembeza kombe hilo mtaani huko Ujerumani kwamba alichukua kombe hilo na kwenda nalo nyumbani. Nyota huyo raia wa Ufaransa amesema alikuwa macho mpaka alfajiri na baadae kwenda kulala akiwa na mke wake pamoja na kombe hilo. Bayern sasa wana nafasi ya kushinda matatu matatu kwa mkupuo kama wakifanikiwa kushinda taji la DFB Pokal Juni mosi mwaka huu.
BENITEZ ATAKA KUFUNDISHA TIMU INAYOSHIRIKI CHAMPIONS LEAGUE.
MENEJA wa muda wa klabu ya Chelsea, Rafael Benitez amekiri kuwa anataka kufundisha timu inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza kazi yake katika klabu hiyo. Katika kipindi kifupi kijacho Benitez ataondoka Stamford Bridge akiwa ameisimamia klabu hiyo kwa mara ya mwisho Jumamosi iliyopita wakati walipochapwa na Manchester City katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jijini New York Marekani. Kocha huyo raia wa Hispania aliiongoza Chelsea kushinda taji la Europa League na pia kuwasaidia kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwimu ujao baada ya kuajiriwa kwa muda mfupi kuziba nafasi ya Roberto Di Matteo Novemba mwaka jana. Banitez anaondoka Chelsea kumpisha Jose Mourinho na kocha huyo sasa anaweza kuangalia mstakabali wake huko mbele baada ya kuhusishwa na tetesi za kwenda Napoli na Paris Saint-Germain ambapo klabu zote hizo zinakidhi matakwa yake ya kushiriki Ligi ya Mabingwa.
MARCEDES KUFANYIWA UCHUNGUZI NA FIA WAKITUHUMIWA KUFANYA MAJARIBIO YA KIUFUNDI KINYUME CHA UTARATIBU.
TIMU ya Marcedes inakabiliwa na uchunguzi kutoka kwa chama kinachosimamia mbio za magari yaendayo kasi ya langalanga-FIA baada ya kutuhumiwa kujaribu matairi yao kinyume cha utaratibu. Timu za Red Bull na Ferrari zilipelekea malalamiko hayo katika michuano ya Monaco Grand Prix baada ya kugundua matairi yanayotengenezwa na kampuni ya Pirelli yanayotumiwa na Mercedes yalifanyiwa majaribio kwa siku tatu. Kwenye sheria za mashindano hayo msimu ukishaanza majaribio huwa hayaruhusiwi labda kwa madereva chipukizi au kwa kiwango kilichowekwa ambacho ni kilometa 1,000 lakini Pirelli wamedai kuwa wana mkataba na FIA unaowaruhusu kufanya majaribio kwa kiwango. Hata hivyo Red Bull na Ferrari wamedai kuwa sheria inasema kama utafanya majaribio kwa kiwango hicho kilichowekwa inabidi utumie aina ya gari ambalo limeshatumika kwa zaidi ya miaka miwili lakini Marcedes wao walitumia gari lao jipya lilitoka 2013 pamoja na madereva wao nyota Lewis Hamilton na Nico Rosberg. Timu pinzani na Marcedes zimefikia hatua kwasababu majaribio kama hayo ya ziada yanaweza kuwapa faida ya kiufundi hivyo kuwawezesha kufanya vizuri zaidi.
Sunday, May 26, 2013
MSIMU UJAO NITAKUJA IMARA ZAIDI - KLOPP.
MENEJA wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp ameapa kuimarisha kikosi chake na kufikia fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kipigo walichopata dhidi ya Bayern Munich. Dortmund walipoteza mchezo huo ulizikutanisha timu zote kutoka Ujerumani kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Wembley baada ya bao la dakika za mwisho lililofungw ana Arjen Robben. Lakini kocha huyo ametamba kuwa pamoja na kushindwa katika fainali hiyo ya Wembley lakini anaamini atafikia fainali nyingine katika kipindi kifupi kijacho. Klopp amesema kwasasa ana kazi kubwa ya kuimarisha kikosi chake baada ya wachezaji kadhaa tegemeo kutaka kuondoka mwishoni mwa msimu huu lakini anaamini mpaka kufikia msimu mpya tayari atakuwa na kikosi imara. Kiungo tegemeo wa klabu hiyo Mario Gotze tayari imeshathibitishwa kwenda Bayern Msimu ujao huku mshambuliaji wake nyota Robert Lewandowski naye akijipanga kuelekea huko.
Subscribe to:
Posts (Atom)












