MENEJA mpya wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amesisitiza kuwa anajali zaidi kuboresha viwango vya wachezaji wake kuliko kushinda mataji. Guardiola mwenye umri wa miaka 42 aliiongoza Barcelona kushinda mataji 14 katika kipindi cha miaka minne ambayo ameinoa klabu hiyo na kuwa kocha aliyepata mafanikio zaidi katika historia. Hatahivyo kocha huyo ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania amesisitiza kuwa kuboresha viwango vya wachezaji mmoja mmoja ni motisha kubwa kwake kuliko kushangilia mataji. Guardiola alionja taji lake la kwanza jana usiku katika michuano ya Kombe la Audi ambapo kikosi chake kilifanikiwa kutoka nyuma na kuifunga Manchester City mwaka mabao 2-1 katika mchezo fainali. Guardiola alichukua nafasi ya Jupp Heynckes kama kocha wa Bayern katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi baada ya kupumzika kwa mwaka mmoja toka alipoondoka Barcelona mwaka 2012.
Friday, August 2, 2013
SUAREZ ABAKIE LIVERPOOL KWA MSIMU MWINGINE - WRIGHT.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal, Ian Wright amedai kuwa Luis Suarez anatakiwa kubakia Liverpool na kukataa nafasi ya kuijunga na Arsenal katika usajili wa kipindi hiki cha kiangazi. Liverpool tayari imekataa ofa mbili za Arsenal kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 ambaye anataka kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Akihojiwa Wright amesema atamkaribisha Suarez kwa mikono miwili kama akijunga na Arsenal lakini kama angekuwa yeye angeipa Liverpool msimu mwingine kabla ya kuamua kuondoka. Wright pia alishukuru kuona Arsenal wameamka na kutaka kusajili majina makubwa maana bila ya kufanya hivyo wangekuwa wanaachwa na timu zingine ambazo husajili wachezaji nyota. Suarez ambaye ni raia wa Uruguay tayari ameonyesha nia ya kuondoka Anfield pamoja na kusaini mkataba mpya Agosti mwaka jana.
Thursday, August 1, 2013
HINGIS AAONJA USHINDI WA KWANZA BAADA YA KUREJEA TENA KATIKA ULINGO WA TENISI.
MCHEZAJI tenisi namba moja wa zamani kwa upande wa wanawake, Martina Hingis amepata ushindi wake wa kwanza toka aliporejea tena uwanjani baada ya kushinda mechi ya mzunguko wa kwanza ya wawili wawili katika michuano ya wazi California. Hingis mwenye umri wa miaka 32 raia wa Switzerland alistaafu mchezo huo mwaka 2007 lakini alikubali mwaliko wa kucheza pamoja na Daniela Hantuchova wa Slovakia. Wawili hao walitumia muda wa dakika 51 pekee kuwagaragaza Julia Goerges na Darija Jurak kwa seti 2-0 zenye alama za 6-1 6-1 na kusonga mbele katika hatua ya pili ya michuano hiyo. Hingis ambaye ji raia wa Switzerland amesema anajisikia vyema kushinda mchezo huo na kumpongeza mwenzake kwamba alifanya mchezo huo uwe rahisi kwao kutokana na uwezo mkubwa alionao. Maumivu ya kifundo cha mguu yalimlazimisha Hingis kustaafu mchezo huo kwa mara ya kwanza mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 22 lakini alirejea miaka mitatu baadae na kushinda taji lake la 43 la WTA kabla ya kushindwa vipimo vya dawa za kuongeza vilivyopelekea kufungiwa kwa miaka miwili.
ENNIS-HILL AMEFANYA UAMUZI WA BUSARA KUJITOA MICHUANO YA DUNIA - LEWIS.
BINGWA wa zamani wa michuano ya olimpiki, Denise Lewis amedai kuwa mwanadada nyota katika mbio za kuruka chini Jessica Ennis-Hill anaweza kupoteza zaidi kama angeshiriki michuano ya riadha ya dunia ambayo inatarajiwa akufanyika baadae mwezi huu. Ennis-Hill ambaye ni bingwa wa olimpiki katika mbio za kuruka chini mapema jana aliamua kujitoa katika michuano hiyo itakayofanyika jijini Moscow kutokana na majeraha yanayomsumbua. Lewis ambaye naye aliwahi kuwa bingwa wa mbio hizo miaka 13 iliyopita katika michuano iliyofanyika jijini Sydney amesema mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Marekani alifanya uamuzi wa busara kujitoa. Ennis-Hill ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya kisigino alijitoa katika mashindano matano tofauti kuanzia Mei na Julai kabla ya kushiriki mashindano ya Diamond League ya Uingereza ikiwa ni mara ya pili kushindana toka anyakue medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki mwaka jana.
MCHEZAJI WA TAHITI ASHINDWA VIPIMO VYA DAWA ZZILIZOPIGWA MARUFUKU.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limemsimamisha mchezaji wa timu ya taifa ya Tahiti kwa siku 30 baada ya kushindwa vipimo vya madawa ya kuongeza nguvu katika michuano ya Kombe la Shirikisho. Katika taarifa yake FIFA haikumtaja mchezaji huyo wala kuelezea kwa undani suala hilo lakini ilidai kuwa mchezaji huyo alichukuliwa vipimo baada ya Tahiti kufungw ana Uruguay mabao 8-0 jijini Racife Juni 23. FIFA imeeleza kuwa itafungua kesi ya kinidhamu na kumuoita mchezaji huyo kujibu tuhuma hizo zinazomkabili. Hilo ni tukio la tatu kwa wachezaji kushindwa vipimo hivyo katika mechi za FIFA huku tayari shirikisho hilo machi mwaka huu likiwa limeshamfungia miaka miwili kiungo wa kimataifa wa Peru Joel Sanchez kwa kukutwa ametumia dawa hizo kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Bolivia Octoba mwaka jana. Wiki iliyopita Shirikisho la Soka la Jamaica lilidai kuwa mchezaji wake mmoja alishindwa vipimo vya dawa za kuongeza nguvu baada ya mechi dhidi ya Honduras iliyochezwa Juni mwaka huu.
HATUNA MPANGO WA KUMUUZA MODRIC - ANCELOTTI.
MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amesisitiza kuwa hana mpango wa kumuuza kiungo wake mahiri Luka Modric katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi. Kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia ni mmoja wa viungo David Moyes anaowahitaji kama Manchester United ikishindwa kumsajili Cesc Fabregas wa Barcelona katika kipindi hiki cha kiangazi. Modric ambaye alijiunga na Madrid akitokea Tottenham Agosti mwaka jana amecheza mechi 33 za La Liga msimu uliopita chini ya Jose Mourinho na Ancelotti amesema kiungo huyo mwenye miaka 27 yuko katika mipango yake kwa ajili ya msimu mpya. Ancelotti amesema wachezaji wote wanafuraha kuwepo hapo na kufanya kazi pamoja naye na kudai kuwa hawajazungumza na mchezaji yoyote kuhusu kuondoka hivyo Modric hawezi kwenda popote.
HATIMAYE TOTTENHAM WALEGEA NA KUMUACHIA BALE.
KLABU ya Real Madrid ya Hispania wanaamini kuwa hatimaye wameweza kuishawishi klabu ya Tottenham Hotspurs kumuuza mshambuliaji wake Gareth Bale kwa ada ya paundi milioni 87 ambayo itavunja rekodi ya dunia. Baada ya kupita wiki kadhaa wakisisistiza kuwa Bale hauzwi, Spurs wameonekana kulegea na kukubali kumuachia nyota huyo wa kimataifa kutoka Wales. Kuna tetesi kuwa Spurs wamekubali kumuachia nyota huyo kwa masharti kwamba mpaka watakapomaliza kuwasajili wachezaji wanaowahitaji ndio habari hizo zitangazwe hadharani. Spurs kwasasa inategemea kukamilisha usajili wa Roberto Soldado uliowagharimu paundi milioni 26 kutoka Valencia na meneja wa klabu hiyo Andre Villas-Boas pia anamnyatia kinda lenye miaka 20 Alvaro Morata kutoka Madrid.
Subscribe to:
Posts (Atom)






