MSIMU mpya wa soka bara la Ulaya unakaribia kuanza kuanza rasmi tena huku tayari nchi kama Ujerumani mechi za duru ya kwanza ya Kombe la Shirikisho zimeanza. Michuano hiyo inazishirikisha timu kutoka Ligi Kuu maarufu kama Bundesliga hadi timu za daraja ya sita na mara nyingi mechi hizo hazikosi kuacha mshangao. Mwishoni mwa iki hii kutakuwa na mechi 32 zitakazochezwa ambapo mwaka jana Bundesliga ziliangushwa na timu za daraja za chini katika duru ya kwanza. Mashabiki katika mechi hizo watapata fursa ya kuona wachezaji wapya waliosajiliwa katika timu zao huku timu vigogo kama Bayern Munich, Borussia Dortmund na Bayern Liverkusen zikitegemewa kufanya vyema na kusonga mbele katika michuano hiyo. Fainali ya michuano hiyo kama kawaida huwa inaandaliwa katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin na itachezwa Mei mwakani.
Saturday, August 3, 2013
Friday, August 2, 2013
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
USAJILI WA WACHEZAJI SASA MWISHO AGOSTI 5
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali. Uamuzi wa kusogeza mbele umetokana kuchelewa kupata disc ya usajili msimu huu ambayo ndiyo inayotumika kwa usajili wa elektroniki unaofanywa kwa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Disc hiyo ambayo hutolewa na kampuni ya NAS Technology ya Tunisia tayari imeshawasili. Kutokana na mabadiliko hayo, sasa kipindi cha pingamizi kitakuwa kati ya Agosti 6 na 12 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo. Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 15 mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu. Timu zitakazoruhusiwa kusajili ni zile ambazo zitakuwa hazijajaza nafasi zote za usajili. Dirisha dogo za usajili litafunguliwa kuanzia Novemba 15 mwaka huu hadi Desemba 15 mwaka huu. Pia klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zinapowasilisha usajili wao zinatakiwa kuambatanisha nyaraka zinazoonesha viwanja vyao vya mazoezi, nakala za bima kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Masuala hayo yameelezwa kwenye Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom
KAMISHNA RWIZA KUSIMAMIA MECHI YA CHANShirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Rwiza wa Tanzania kuwa kamishna wa mechi ya raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN). Rwiza atakuwa kamishna katika mechi ya kwanza ya raundi hiyo itakayohusisha mshindi wa mechi kati ya Msumbiji na Namibia dhidi ya Angola itakayochezwa kati ya Agosti 9 na 11 mwaka huu. Mechi hiyo itachezeshwa na refa Noram Matemera kutoka Zimbabwe. Matemera atasaidiwa na Wazimbabwe wenzake Tapfumaney Mutengwa atakayekuwa mwamuzi msaidizi namba moja, Ncube Salani ambaye ni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ruzive Ruzive.

NAHODHA WA LAZIO AFUNGIWA MIEZI SITA KWA KASHFA YA UPANGAJI MATOKEO.
SHIRIKISHO la Soka la Italia, FIGC limetangaza kumfungia nahodha wa klabu ya Lazio Stefano Mauri kwa miezi sita baada ya kushindwa kutoa taarifa ya shughuli za upangaji matokeo katika mechi. Mbali na Mauri wachezaji wengine walioadhibiwa ni pamoja na Mario Cassano, Stefano Ferrario, Carlo Gervasoni na Alessandro Zamperini kutokana na sakata hilo. Wachezaji watano walikuwa katika uchunguzi kufuatia tuhuma za upangaji matokeo wa mechi za Lazio dhidi ya timu za Genoa na Lecce katika msimu wa Serie A 2010-2011 na sasa wamekutwa na hatia na kamati ya nidhamu ya FIGC. Katika taarifa ya FIGC iliyotumwa katika mtandao wake imedai kuwa katika tukio lililohusha mchezo kati ya Lazio na Genoa, Gervasoni amefungiwa miezi miwili, Cassano amefungiwa miezi minne, Ferrario na Mauri wamefungiwa miezi sita na Zamperini amefungiwa miaka miwili. Kwa kuongezea timu ya Lecce ilitozwa faini ya euro 20,000 na Lazio euro 40,000 baada ya timu hizo nazo kukutwa na hatia ya upangaji matokeo.
RAIS WA ZAMANI WA SHIRIKISHO LA SOKA LA BENIN ATUPWA LUPANGO.
RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka nchini Benin, Anjorin Moucharafou amekamatwa tena na kutupwa lupango ikiwa ni siku mbili baada ya kukataa kugombea nafasi hiyo kwa muhula wa tatu. Moucharafou ambaye alifikishwa mbele ya Mahakama Julai 2011 kwa matumizi mabaya ya fedha za shirikisho hilo na kuwekwa rumande katika gereza moja la kiraia, aliitwa tena mahakamani wiki hii pamoja na mhasibu wake Cecile Houssou kwa tuhuma hizohizo za ubadhilifu. Kiongozi huyo ambaye pia ni mfanyabiashara anatuhumiwa kusifuja isivyotakiwa kiasi cha dola 650,000 za udhamini kutoka kampuni ya simu ya MTN kati ya mwaka 2008 na 2010. Mbali na kushikilia wadhifa huo nchini kwao lakini pia Moucharafou amewahi kuwa mjumbe katika kamati za utendaji za Shirikisho la Soka Duniani-FIFA na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF.
ITAKUWA NGUMU BALE KUICHOMOLEA MADRID - REDKNAPP.
MENEJA wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Harry Redknapp amedai kuwa itakuwa ni ngumu kwa Gareth Bale kukataa kwenda katika klabu ya Real Madrid ya Hispania. Meneja wa Madrid, Carlo Ancelotti alibainisha mapema kuwa vigogo hao wa soka nchini humo wako katika mazungumzo ya kujaribu kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 24. Redknapp amesema anadhani itakuwa ngumu kwake kutokubali kuondoka sasa kwani ameshasikia kutoka katika vyanzo tofauti kwamba anataka kuondoka katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi. Kumekuwa na taarifa kuwa Madrid wanajiandaa kutoa ofa itakayovunja rekodi ya dunia ya paundi milioni 80 waliyomsajili Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United mwaka 2009 ingawa mpaka sasa hakuna ofa rasmi iliyotolewa. Redknapp amesema Madrid ni klabu ya kipekee ambapo mchezaji yoyote ana ndoto ya kuichezea siku moja hivyo kukataa ofa yao huwa ni ngumu kwa mchezaji yoyote.
SAA KUBWA ILIYOWEKWA KATIKA UFUKWE WA COPACABANA KUHESABU MUDA ULIOSALIA KABLA YA KUANZA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA YASHINDWA KUFANYA KAZI.
SAA kubwa ambayo inahesabu muda uliosalia kabla ya kuanza michuano ya Kombe la Dunia mwakani iliyopo jijini Rio de Janeiro imepigwa picha ikiwa imesimama. Ikiwa mpaka sasa imebakia takribani miezi 11 kabla ya kuanza kwa michuano hiyo saa kubwa iliyowekwa na waandaaji katika ufukwe wa Copacabana bado inaonyesha kuwa zimebaki siku 365 kabla ya kuanza kwa tukio hilo kubwa katika soka. Saa hiyo ilionekana kusimama toka alipowasili Papa Francis wiki chache zilizopita na kuvutia mamilioni ya watu aliowahutubia katika ufukwe huo. Katika taarifa yake kamati ya maandalizi ya michuano hiyo ilidai kuwa walikuwa wakijua tatizo la saa hiyo na kuwa kampuni inayohusika na matengenezo inatarajiwa kutatua tatizo hilo mapema. Brazil imekuwa ikikumbwa na changamoto nyingi katika maandalizi ya michuano hiyo hivyo kuibua wasiwasi wa kama miundo mbinu pamoja na viwanja vinavyojengwa kukamilika kwa wakati uliopangwa.
MASHABIKI MARUFUKU KUSHUHUDIA MECHI ZA LIGI NCHINI ARGENTINA.
KATIKA harakati za kupunguza vurugu katika soka nchini Argentina, msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo utaanza mwishoni mwa wiki hii kwa wanachama pekee kuruhusiwa kuingia viwanjani na kutizama mechi zao za nyumbani. Sheria hiyo itaendelea kwa wiki mbili za kwanza na baada ya hapo hatua itakayofuata ni kuwazuia mashabiki wa pinzani kuhudhuria mechi. Katika kipindi cha karibuni soka nchini humo limekuwa likimbwa na vurugu za mara kwa mara ambapo mwezi uliopita mashabiki wawili wa klabu ya Boca Juniors waliuawa katika majibishano ya risasi kati ya makundi ya wahuni ambao hishabikia klabu hiyo. Tahadhari hiyo imechukuliwa baada ya Chama cha Soka nchini humo kulaumiwa kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti ili kudhibiti vurugu hizo ambazo zinaonekana kuota mizizi.
Subscribe to:
Posts (Atom)