KIUNGO mahiri wa klabu ya Barcelona, Xavi anaamini kuwa mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi Atletico Madrid bado uko wazi baada ya timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza. Katika mchezo huo Diego Costa na Neymar kila mmoja aliifungia timu yake bao na kupelekea timu hizo kutoka nguvu sawa kuelekea katika mchezo wa marudiano utakaofanyika katika Uwanja wa Vicente Calderon mwiki ijayo. Xavi amekiri Atletico ambao wananolewa na Diego Simeone wana nafasi nzuri zaidi katika mchezo wao wa marudiano ambao utachezwa kwao lakini amedai mchezo huo bado uko wazi na yoyote anaweza kupenya katika hatua inayofuata. Kiungo huyo amesema Atletico wana kikosi kikali na ilikuwa ngumu kwao kutafuta nafasi lakini wanahitaji kuwa wavumilivu na kutumia makosa machache yatakayofanywa na wapinzani wao ili waweze kupata mabao.
Wednesday, April 2, 2014
SERENA WILLIAMS APEWA KICHAPO NA DOGO.
MWANADADA nyota wa tenisi anayeongoza katika orodha za ubora duniani, Serena Williams amepewa kichapo cha kushtusha kutoka kwa Jana Cepelova katika mzunguko wa pili wa michuano ya Family Ciecle Cup huko South Carolina. Williams mwenye umri wa miaka 32 ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo alijikuta akishindwa kutamba mbele Cepelova raia wa Slovakia anayeshika nafasi ya 78 katika orodha hizo kwa kufungwa kwa 6-4 6-4. Mmarekani huyo ambaye alishinda michuano ya wazi ya Sony iliyofanyika jijini Miami wiki iliyopita alishindwa kurejea mchezoni baada ya kupoteza alama tano za kwanza kwa binti huyo mwenye miaka 20. Hata hivyi dada yake Serena, Venus alifanikiwa kutunga hatua ya mzunguko wa tatu kwa kumfunga kwa tabu Barbora Zahlavova wa Jamhuri ya Czech kwa 6-3 0-6 7-5.
UPASUAJI WAMKOSESHA WOODS MICHUANO YA MASTERS.
BINGWA mara nne wa michuano ya Masters, Tiger Woods anatarajiwa kuikosa michuano hiyo baada ya kufanyiwa upasuaji kufuatia maumivu ya mgongo yaliyokuwa yakimsumbua. Woods ambaye anaongoza katika orodha za ubora wa mchezo huo alikosa michuano ya Arnold Palmer ambayo huwa anaitumia kwa ajili ya kujiweka fiti na michuano hiyo mikubwa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 amesema ni jambo lililomhuzunisha lakini hana jinsi inabidi afuate ushauri wa madaktari ili aweze kupona vyema kwa kipindi kirefu kijacho. Woods ambaye hajawahi kukosa michuano ya Masters kwa kipindi cha miaka 19 iliyopita amewahi kushinda mataji manne ambapo mshindi huvalishwa koti la kijani mwaka 1997, 2001, 2002 na 2005.
KILA MTU ANATAKA WENGER ABAKI - VERMAELEN.
BEKI mahiri wa klabu ya Arsenal, Thomas Vermaelen amesema kila mchezaji wa timu hiyo anataka Arsene Wenger kusaini mkataba mpya na kubakia katika Uwanja wa Emirates. Kocha huyo raia wa Ufaransa tayari ameeleza nia yake ya kubakia lakini bado hajawa tayari kusaini mkataba mpya na kudai kuwa atafikiria kuhusu mstakabali wake mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anategemea Wenger ataongeza muda wake wa kubakia katika klabu hiyo yenye London ya Kaskazini ambapo tayari anakaribia kutimiza miaka 18. Vermaelen amesema kila mtu anataka katika klabu hiyo anataka Wenger kubakia kwa muda mrefu zaidi atakavyoweza kwasababu ameifanya mengi mazuri kwa wachezaji na klabu kwa ujumla.
SARE YAMFANYA MOYES KUANZA KUCHONGA.
MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes anaamini kuwa kikosi chake kina nafasi kubwa ya kuwaengua mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Bayern Munich baada ya sare ya bao 1-1 waliyopata katika mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali iliyofanyika katika Uwanja wa Old Trafford jana usiku. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Moyes amesema anajua wanatakiwa kufunga katika mchezo wao wa marudiano utakaofanyika Ujerumani hivyo atajitahidi kuwanoa washambuliaji wake. Lakini pamoja na hayo Moyes anaamini wamejitengenezea nafasi nzuri ya kuhakikisha wanasonga mbele. Katika mchezo wa marudiano Bayern watamkosa kiungo wao mahiri Bastian Schweinsteiger aliyelimwa kadi nyekundu jana kwa kumchezea faulo Wayne Rooney. Meneja wa Bayern Pep Guardiola atalazimika kubadilisha safu yake ya kati kabla ya mchezo wa marudiano Aprili 9 kwani atakuwa bila viungo wake muhimu akiwemo Thiago Alcantara aliyekuwa na mejeruhi huku Javi Martinez naye akiwa na adhabu ya kutumikia mechi moja.
Tuesday, April 1, 2014
NGORONGORO HEROES KWENDA NAIROBI APRILI 3.
Ngorongoro Heroes itaagwa kesho (Aprili 2 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF.
MARCELO KUWAKOSA DORTMUND.
KIKOSI cha klabu ya Real Madrid kinachonolewa na Carlo Ancelotti kimepata pigo kuelekea katika mchezo wao wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund baada ya beki wake tegemeo Marcelo kuondolewa kutokana na majeruhi ya msuli. Beki huyo wa kimataifa wa Brazil alikaa benchi katika ushindi wa mabao 5-0 iliyopata Madrid dhidi ya Rayo Vallecano mwishoni mwa wiki na tatizo litamuweka pia katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza Jumatano. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo imedai baada ya uchunguzi wa kina wamegungua kuwa beki huyo alichanika msuli wa nyuma ya paja wa mguu wake wa kushoto. Hajajulikana ni muda gani haswa nota huyo mwenye miaka 25 atakaa nje ya uwanja lakini mchezo wa kesho itakuwa ni mapema sana kwake.
Subscribe to:
Posts (Atom)






