NAHODHA wa kimataifa wa Nigeria, Mikel John Obi amekanusha taarifa zilizozagaa kuwa anakaribia kuondoka Chelsea. Kiungo huyo amesema atabakia na kupigania nafasi yake na mkataba mpya katika klabu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge. Taarifa zilikuwa zimedai kuwa Mikel alikuwa akiwindwa na klabu kadhaa za China lakini mwenyewe amejitokea na kuweka wazi kuwa bado ataendelea kucheza soka Uingereza. Mikel amesema anataka kupigana ili kuisaidia timu yake kupata kila alama ili waweze kushinda mataji msimu ujao. Kwasasa Mikel yuko na kikosi cha Nigeria wakijiandaa kwa ajili ya michuano ya soka ya Olimpiki itakayofanyika huko nchini Brazil.
Wednesday, August 3, 2016
Monday, August 1, 2016
MOYES ATAKA KUWACHUAKUA FELLAINI NA JANUZAJ.
MENEJA mpya wa Sunderland, David Moyes amethibitisha ni yake ya kutaka kuwasajili nyota wa Manchester United Marouane Felleini na Adnan Januzaj. Moyes, ambaye amechukua nafasi ya Sam Allardyce, ndio aliyemleta Fellaini nchini Uingereza wakati akiwa meneja wa Everton mwaka 2008 na baadae kumsajili wakati alipokwenda United mwaka 2013. Meneja huyo pia ndiye aliyempa nafasi Januzaj ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha United wakati akiinoa klabu hiyo na chipukizi huyo alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa kwanza ambao ulikuwa dhidi ya Sunderland Octoba mwaka 2013. Fellaini na Januzaj wanadaiwa kukosa nafasi chini ya meneja mpya Jose Mourinho na Moyes amethibitisha katika mkutano wake wa kwanza na wanahabari kuwa anataka kuwasajili wawili hao.
WOLFSBURG YNASA WINGA WA DORTMUND.
KLABU ya Wolfsburg imefanikiwa kumsajili Jakub Blaszczykowiski kutoka Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka mitatu. Nyota huyo wa kimataifa wa Poland ambaye alijiunga na Dortmund mwaka 2007, amekamilisha mkataba wake huo wa moja kwa moja Wolfsburg ambao unakadiriwa kufikia euro milioni tano. Jakub mwenye umri wa miaka 30 anajiunga na klabu hiyo kuziba nafasi ya Andre Schurrle aliyekwenda Dortmund mapema kiangazi hiki. Mkurugenzi wa michezo wa Wolfsburg Klaus Allofs alithibitisha taarifa hizo na kuongeza kuwa winga huyo atasaidia sana klabu hiyo msimu ujao kutokana na ubora wake.
MAHREZ AMCHANGANYA RANIERI.
MENEJA wa Leicester City Claudio Ranieri amekiri Riyad Mahrez anaweza kuwa amechanganywa na tetesi zinazomhusisha na yeye kwenda Arsenal kufuatia Arsene Wenger kudokeza kumuhitaji winga huyo. Taarifa zimekuwa zikizagaa kuwa Arsenal wanakaribia kukamilisha dili la kumsajili Mahrez mwenye umri wa miaka 25, lakini Ranieri amekanusha taarifa hizo akidai winga huyo wa kimataifa wa Algeria atabakia katika klabu hiyo. Hata hivyo, akihojiwa baada ya Leicester kuchapwa mabao 4-0 na Paris Saint-Germain katika mchezo wa kirafiki, Ranieri amesema anadhani mchezaji huyo amebadili mawazo. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa Mahrez pengine atakuwa amechanganywa na tetesi zinazoendelea lakini angependa abaki.
WENGER AMLILIA CAZORLA.
MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo wake tegemezi Santi Cazorla anaweza asiwe fiti kwa ajili ya mwanzo wa msimu. Cazorla alirejea uwanjani kwa mara ya kwanz akatika mchezo wa kirafiki ambao Arsenal ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Guadalajara ya Mexico jana akicheza kipindi cha kwanza pekee. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania alikosa kucheza kwa miezi mitano msimu uliopita kutokana na majeruhi ya goti na Wenger amepanga kumrejesha taratibu mpaka atakapokuwa fiti kwa asilimia 100. Akihojiwa Wenger amesema kwasasa Cazorla bado hajawa fiti kwa asilimia zote ndio maana ameamua kuanza kumtumia taratibu kadri atakavyoona inafaa. Wenger aliendelea kudai kuwa Cazorla anaweza kuwa fiti kabisa mwishoni mwa mwezi huu hivyo kuwepo uwezekano mkubwa wa kukosa mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu ambao watacheza Liverpool Agosti 14.
GATTUSO AIKIMBIA KLABU YA SERIE B.
KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Italia, Gennaro Gattuso amejiuzlu kuifundisha klabu ya daraja la pili ya Pisa ya Italia muda mfupi kabla ya kuanza msimu mpya kwasababu ya kushindwa kuelewana na viongozi. Gattuso aliiongoza klabu hiyo inayotoka katika mji wa Tuscan, Italia kupanda daraja mpaka Serie B msimu uliopita na alishatishia kujiuzulu kama uongozi usingetimiza matwaka yake. Mara baada ya kuinoa timu hiyo kwa wiki kadhaa kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya, Gatusso ameamua kujiuzlu sababu kubwa ikiwa mazingira mabovu ambayo yanamfanya kushindwa kufanya kazi yake vyema. Gattuso enzi zake alitumia kipindi kirefu akiitumikia klabu ya AC Milan kabla ya kuamua kutundika daruga zake na kuhamia masuala ya ukocha miaka minne iliyopita.
MAN CITY YAKARIBIA KUMNASA CHIPUKIZI WA SCHALKE.
KLABU ya Manchester City inadaiwa kukaribia kukamilisha usajili wa Leroy Sane kutoka klabu ya Schalke ya Ujerumani kwa ada inayotajwa kufikia paundi milioni 37. Klabu hiyo ya Bundesliga imetangza leo kuwa kiungo huyo hajajiunga nao katika kambi ya mazoezi nchini Austria na badala yake alisafiri kuelekea Manchester. Meneja mpya wa City, Pep Guardiola alithibitisha Julai 21 mwaka huu kuwa anataka kumsajili Sane. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 aliisaidia nchi yake ya Ujerumani kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ulaya mwaka huu, akiwa ameitwa kwa mara ya kwanza Novemba mwaka jana.
Subscribe to:
Posts (Atom)






