RAIS wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell amesisitiza kuwa Lionel Messi hajaomba mkataba mpya wenye maslahi zaidi baada ya Real Madrid kumfanya Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno amesaini mkataba mpya wa miaka mitano utakaomuwezesha kukunja kitita cha euro milioni 21 kwa msimu Jumapili iliyopita na kuzusha chokochoko kuwa Messi naye atahitaji kupandishiwa mshahara ili kumfikia Ronaldo. Hata hivyo Rosell alifafanua kuwa mkataba mpya wa Ronaldo hauna athari zozote kwenye mkataba wa sasa wa Messi. Rosell amesema nyota huyo wa kimataifa wa Argentina hajazungumza lolote kuhusiana na hilo na anaonyesha kufurahia kuwepo katika klabu hiyo bora kabisa duniani.
Wednesday, September 18, 2013
KROL KUINOA TUNISIA.
SHIRIKISHO la Soka nchini Tunisia limetangaza kumpa kibarua nahodha wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi Ruud Krol kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo katika mechi zake za mtoano ili kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Tunisia imepangwa kuchezwa na Cameroon katika mechi za mikondo miwili zitakazochezwa Octoba na Novemba wakichukua nafasi ya Cape Verde walioondolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Krol anachukua nafasi ya nabil Maaloul ambaye alijiuzulu baada ya Tunisia kupoteza mechi yake ya mwisho nyumbani kwa kufungwa mabao 2-0 na Cape Verde Septemba mwaka huu. Matokeo hayo yalimaanisha nchi hiyo kukosa nafasi ya kwenda hatua ya mtoano lakini walipata nafasi hiyo siku chache baadae wakati Cape Verde walipokutwa na hatia ya kumchezesha mchezaji asiyeruhusiwa na FIFA kuwapa ushindi wa mabao 3-0 uliowazesha kusonga mbele. Krol ambaye amepewa mkataba wa miezi miwili pia ataendelea kukinoa kikosi cha CS Sfaxien klabu ambayo ameiwezesha kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Tunisia Mei mwaka huu.
DEL PIERO ATEULIWA NAHODHA WA SYDNEY FC.
MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Italia, Alessandro Del Piero ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa kikosi cha Sydney FC ya Australia kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya nchi hiyo maarufu kama A League. Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Juventus ambaye aliweka rekodi ya usajili katika historia ya ligi ya Australia amechangia kwa kiasi kikubwa kuvutia mashabiki uwanjani pamoja na vyombo vya habari nchini humo. Kutokana na hilo Sydney imeamua kumpa unahodha katika msimu wa 2013-2014 ambao unatarajiwa kuanza kutimua vumbi Octoba akichukua nafasi ya Terry McFlynn. Del Piero ambaye pia amewahi kuwa nahodha Juventus kwa miaka 11, amesema ni heshima kubwa kwake kuwa nahodha katika moja ya klabu kubwa nchini humo na bara ya Asia. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 alijiunga na Sydney mwaka jana akitokea Juventus na kuvunga mabao 14 mpaka sasa.
BAO LA ISCO LILIBADILISHA MATOKEO - ANCELOTTI.
MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti anafikiri kuwa bao alilofunga kiungo mahiri wa klabu hiyo Isco ndilo lililobadilisha matokeo katika ushindi waliopata dhidi ya Galatasaray ya Uturuki. Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Madrid walionekana kubanwa katika dakika za mwanzo lakini walifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 baada ya Isco kufungua karamu hiyo ya mabao katika dakika ya 33. Akihojiwa mara baada ya mechi hiyo Ancelotti alikiri kikosi chake kubanwa katika dakika za mwanzoni lakini bao la Isco liliwatuliza na kuwafanya waweze kumiliki mchezo. Kocha huyo pia aliwapongeza washambuliaji wake Cristiano Ronaldo aliyefunga mabao matatu na Karim Benzema aliyefunga mawili katika mchezo huo kwa kiwango kikubwa walichokionyesha.
Tuesday, September 17, 2013
PLATINI KUTOA UAMUZI WA KUGOMBEA URAIS FIFA MWAKANI.
RAIS wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini amebainisha kuwa atatoa uamuzi wake wa kama atagombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ifakapo mwakani. Platini aliwaambia wajumbe wa kamati ya utendaji ya UEFA kabla ya mkutano wao huko Dubrovnik, Croatia kwamba hajaamua kitu cha kufanya huko mbele na anahitaji miezi kadhaa ili kufikiria kwa makini. Platini ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Ufaransa aliendelea kudai kuwa atatoa uamuzi wake kabla au baada ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Rais wa FIFA Sepp Blatter muda wake unamalizika mwaka 2015 na Platini amekuwa akipewa nafasi ya kuchukua mikoba ya Blatter mwenye umri wa miaka 77 kwa kipindi kirefu.
AM TRAIN WITH THE BEST - BALE.
MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale amepania kupandisha kiwango chake na anaamini kuwa uwepo wa Cristiano Ronaldo, kocha mkuu Carlo Ancelotti na kocha msaidizi Zinedine Zidane utamsadia kwa kiasi kikubwa kufikia lengo lake. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales alifunga bao lake la kwanza akiwa na Madrid katika mchezo wa La Liga dhidi ya Villarreal mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo ana uhakika kucheza kwake katika klabu hiyo kutambadilisha na kumpeleka hatua nyingine katika soka lake. Bale amesema Ronaldo ni mchezaji aliyekamilika na atajifunza na kucheza pamoja naye huku akipewa ujuzi kutoka kwa walimu walio bora kama Ancelotti na Zidane. Kwa mara nyingine Bale mwenye miaka 24 amerudia tena kusema kwamba ilikuwa ni ndoto zake kujiunga na Madrid hivyo alipopigiwa siku kueleza kumuhitaji ilikuwa ni siku yenye kubwa kwake na alikuwa akiomba mambo yaende sawa ili afanikiwe kutimiza ndoto zake.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
UWAKILISHI KWENYE MKUTANO MKUU TFF
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema uwakilishi wa ujumbe kwenye Mkutano Mkuu unaanzia kwenye chama cha mpira wa miguu cha mkoa, kufuatiwa na chama shiriki na baadaye klabu ya Ligi Kuu. Mwongozo huo juu ya uwakilishi wa wajumbe kwenye Mkutano Mkuu umetolewa kutokana na maombi ya Sekretarieti ya TFF kwa kamati hiyo iliyokutana jana (Septemba 16 mwaka huu) baada ya kubaini baadhi ya wajumbe wanashikilia nafasi mbili kwenye vyama tofauti. Kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba, kuna makundi ya aina tatu ya wanachama wanaounda TFF. Makundi hayo ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu. Sekretarieti ya TFF imebaini kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kuchaguliwa wa mikoa ambao pia ni viongozi wa vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu, hivyo wana nafasi zaidi ya moja ya kuingia kwenye Mkutano Mkuu. Hivyo, kutokana na mwongozo huo ushiriki wa wajumbe kwenye Mkutano Mkuu wa TFF utaanzia chama cha mkoa, kufuatiwa na chama shiriki na baadaye klabu za Ligi Kuu. Pia nafasi ambazo zinaweza kuwakilishwa kwenye Mkutano Mkuu kama mhusika hayupo ni za Mwenyekiti atakayewakilishwa na Makamu Mwenyekiti, na Katibu atakayewakilishwa na Katibu Msaidizi. Nafasi za ujumbe wa Mkutano Mkuu na ile ya mwakilishi wa klabu hazina uwakilishi kama mhusika hayupo.
LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA NNEMichuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya nne kesho (Septemba 18 mwaka huu) kwa mechi saba katika viwanja saba tofauti. Vinara wa ligi hiyo, JKT Ruvu wanaonalewa na Kocha Mbwana Makata watakuwa ugenini Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani dhidi ya Ruvu Shooting ya Charles Boniface Mkwasa. Mechi hiyo inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa washabiki mkoani Pwani kutokana na aina ya soka inayochezwa na timu hizo. Baada ya sare dhidi ya Mbeya City wikiendi iliyopita, Yanga inaendelea kubaki Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo itacheza na Tanzania Prisons katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Simon Mbelwa kutoka Pwani. Nayo Simba itaumana na Mgambo Shooting Stars ya Tanga katika mechi itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mechi hiyo itakuwa chini ya Kamishna David Lugenge kutoka Iringa. Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Oljoro JKT kutoka Arusha na wenyeji Kagera Sugar wakati Azam na Ashanti United zitakwaruzana kwenye uga wa Azam Complex ulioko Chamazi jijini Dar es Salaam. Mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara ndiye atakayechezesha mechi kati ya Coastal Union na Rhino Rangers itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Mtibwa Sugar inarejea uwanja wake wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro ambapo inaikaribisha Mbeya City ya Kocha Juma Mwambusi. Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) nayo inaendelea kesho (Septemba 18 mwaka huu) kwa mechi moja ambapo Lipuli ya Iringa ambayo wikiendi iliyopita ilicheza Mkamba mkoani Morogoro inapita mjini Morogoro kuikabili Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Subscribe to:
Posts (Atom)