Thursday, October 23, 2014

KUELEKEA KATIKA MCHEZO WA EL CLASICO KATI YA REAL MADRID NA BARCELONA WAJUE MASTAA NA TIMU WANAZOSHANGILIA.

Jenifer Lopez au J Lo na mwanae wakiwa wametinga jezi za Real Madrid.

Mchezaji tenisi nyota wa Hispania naye ni shabiki namba moja wa Madrid.

Mfalme wa Jordan Abdullah naye ni mnazi wa Madrid, pichani akisalimiana na rais wa klabu hiyo Florentino Perez.

Dogo Justin Bieber naye anaifagilia Barcelona, pichani anaonekana akiwa ametinga jezi ya timu hiyo wakati alipokuwa ziarani Hispania.

Shakira yeye ni zaidi ya mnazi kwani mume wake Gerard Pique ndio kitasa cha kutegemewa Barcelona, picha wakiwa na mtoto wao katika moja ya mechi za timu hiyo.

Mkali wa mpira wa kikapu kutoka NBA katika timu ya Los Angeles Lakers, Kobe Bryant na kafa kaoza kwa Barcelona.

Sio Hollywood pekee bali mpaka Bollywood, pichani ni nyota wa filamu wa India Ranbir Kapoor naye anaishabikia Barcelona.

Mkongwe wa kikapu katika NBA, Magic Johnson pia ni mzee wa Catalan.

MASTAA MAN UNITED WADHARAU MAGARI YA WADHAMINI CHEVROLET NA KUSUKUMA MIKOKO YAO WENYEWE.

Mshambuliaji nyota wa United akitinga uwanja wa mazoezi na gari lake la kifahari aina ya Porche 911.

Nahodha wa United Wayne Rooney akitinga na mkoko wake matata aina ya Range Rover "Overfinch".

Kocha msaidizi Ryan Giggs akiwa ndani ya gari lake aina ya Range Rover.

Marouane Fellaini naye ni mmoja wa mastaa waliogoma kutumia Chevrolet pichani anaonekana akitinga mazoezini na Marcedes.

Anderlecht vs Arsenal 1-2 All Goals & Highlights

Galatasaray vs Borussia Dortmund 0:4 2014 , Dortmund VS Galatasaray 4-0 ...

Atletico Madrid VS Malmo FF 5-0 All Goals & Highlights UCL 2014

KAMA ULI-MISS JINSI LIVERPOOL WALIVYOFEDHEHESHWA NA REAL MADRID KATIKA DIMBA LAO LA ANFIELD.

Wednesday, October 22, 2014

BALOTELLI AZUA JAMBO TENA LIVERPOOL IKICHAPWA 3-0 NA REAL MADRID.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Mario Balotelli anakabiliwa na karipio kutoka kwa meneja wake Brandan Rodgers baada ya kubadilishana fulana na beki wa Real Madrid Pepe katika muda wa mapumziko wakati timu hiyo ilipotandikwa kwa mabao 3-0 katika Uwanja wa Anfield. Balotelli alifanya tukio hilo wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao matatu katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo baadae mshambuliaji huyo alitolewa. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Rodgers amesema jambo hakulifurahia kwani kama mchezaji anataka kubadiishana fulana na mwenzake anapswa kusubiri mpaka mchezo utakapomalizika. Rodgers ambaye pia amewahi kumvaa beki wake Mamadou Sakho ambaye alifanya tukio hilo kama hilo na Samuel Eto’o wakati akiwa Chelsea msimu uliopita amesema suala hilo ni ndani na atakabiliana nalo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kubadilishana fulana wakati wa mapumziko na jambo ambalo halifanyikagi katika timu hiyo hivyo inapaswa wachezaji wake wakaelewa hilo.