Wednesday, February 18, 2015

ROONEY AOMBA RADHI KWA KUJIRUSHA.

GOLIKIPA wa klabu ya Preston Thorsten Stuckmann amesema Wayme Rooney alimuomba radhi kwa jinsi alivyodanganya na kupata penati katika mchezo wao dhidi ya Manchester United waliofungw amabao 3-1. Rooney alianguka katika eneo la hatari baada ya kile kilichoonekana kama kuguswa na Stuckmann. Stuckmann alikaririwa na gazeti la The Sun akidai kuwa Rooney alimfuata na kumuomba radhi kwani ilikuwa nafasi yake ya kupata penati na alilazimika kuitumia. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza alifunga penati hiyo na kuihakikishia nafasi United ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la FA dhidi ya Arsenal. Kitendo hicho cha Rooney kilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wachambuzi wa soka lakini aliungwa mkono na kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Roy Hodgson na mchezaji mwenzake wa zamani Phil Neville ambao walidai alijirusha ili kumkwepa golikipa. Stuckmann mwenye umri wa miaka 33 amesema suala hilo liko wazi kuwa ile haikuwa penati lakini walipewa kwasababu wenyewe ni United kwasababu kama ingekuwa mchezaji wao ndio kafanya vile hadhani kama angepewa.

RAIS WA PALERMO AITAKA JUVENTUS KUTOA EURO MILIONI 25 KAMA WATAMUHITAJI NYOTA WAKE VAZQUEZ.

RAIS wa klabu ya Palermo Maurizio Zamparini amesema Franco Vazquez anaweza kuigharimu Juventus euro milioni 25 lakini amekanusha kufanyika mazungumzo yeyote juu ya kumuuza kiungo huyo. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akizivutia vilabu kadhaa vya Serie A kutokana na kiwango bora alichokionysha katika msimu wa 2014-2015 huku Napoli nao wakitajwa kumuwinda. Pamoja na Palermo kukanusha kufanya mazungumzo yeyote kuhusu kiungo huyo lakini inaonekana atakayekuja fungu kubwa anaweza kuishawishi timu hiyo kumuuza. Zamparini amesema hakuna klabu yeyote tuliyofanya nao mazungumzo hivyo bado ataendelea kuwa mchezaji wao labda klabu ije na kitita cha paundi milioni 25 ndio tunaweza kufikiria kumuuza. Vazquez bado ana mkataba wa kuitumikia Palermo unaomalizika Juni mwaka 2019.

KESHI KIBARUA CHANUKIA BURKINA FASO.

KOCHA wa timu ya taifa ya Nigeria aliyemaliza muda wake Stephen Keshi anakaribia kuteuliwa kuinoa timu ya taifa ya Burkina Faso. Keshi ametajwa katika orodha ya makocha watatu wa mwisho ambao watafanyiwa usaili kwa ajili ya kibarua hicho. Shirikisho la Soka la Burkina Faso-FBF jana kilitaja majina hayo ambapo mbali na Keshi lakini pia inawajumuisha Milovan Rajevac kutoka Serbia na Gernot Rohr wa ujerumani. Baada ya kuwafanyia usaili FBF inatarajia kutangaza jina la kocha atakaechukua nafasi ya Paul Put katika kipindi cha wiki tatu zijazo.

KASHFA YA UBAGUZI CHELSEA, MASHABIKI WAKE WAFUMWA WAKIMZUIA MTU MWEUSI KUINGIA KATIKA TRENI.

MASHABIKI wa Chelsea wameonekana katika picha za video wakimzuia mtu mmoja mwenye asili ya Afrika kuingia katika treni jijini Paris. Katika picha hizo, zinemuonyesha mtu huyo akijaribu kuingia mara kadhaa lakini alikuwa akizukumwa na mashabiki hao. Kundi hilo la watu lilikuwa likisikika likiimba kuwa wao ni wabaguzi na dio jinsi wanavyopenda kuwa. Msemaji wa Chelsea amesema tabia hiyo haivumiliki na klabu hiyo itaunga mkono hatua zozote za kihalifu zitakazochukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika. Maelfu ya mashabiki wa Chelsea walikuwa nchini Ufaransa kwa kushuhudia mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya timu yao dhidi ya Paris Saint-Germain ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Tuesday, February 17, 2015

MAN UNITED KUKWAANA NA ARSENAL KATIKA ROBO FAINALI YA KOMBE LA FA.

HATIMAYE timu nane zitakazocheza robo fainali ya michuano ya Kombe la FA huko Uingereza zimejulikana baada ya kukamilika kwa mchezo wa mwisho jana. Mabingwa watetezi wa kombe la FA, Arsenal watachuana na Manchester United katika hatua hiyo ya nane bora. United ndio watakaokuwa wenyeji wa Arsenal katika Uwanja wa Old Trafford kwenye hatua hiyo ambayo inatarajiwa kuchezwa kati ya Machi 7 au 8 mwaka huu. United ilijihakikishia nafasi hiyo ya hatua ya nane bora baada ya kuishindilia Preston North End mabao 3-1 jana. Mechi zingine itazikutanisha Liverpool na mwenyeji Blackburn Rovers, Bradford City itapambana na Reading wakati wapinzani wa jadi kutoka West Midlands Aston Villa na West Bromwich Albion zitamenyana katika uwanja wa Villa Park.

TETESI ZA USAJILI ULAYA: UNITED YAMUWINDA NEYMAR MPYA KUTOKA FLUMINESE, ARSENAL YAMCHACHAMALIA DYBALA, CHELSEA NA UNITED KUTOANA MACHO KWA VERANE.

KATIKA habari za tetesi za usajili klabu ya Manchester United iko tayari kutoa kitita cha euro milioni 6.5 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Fluminese Kenedy ambaye anatabiriwa kuwa Neymar mpya. Nyota huyo wa Brazil amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na United ingawa wanakabiliwa na upinzani kutoka kwa klabu ya Inter Milan. Katika taarifa nyingine inayoihusu United ni kuwa rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez amedai yuko tayari kupokea fedha kwa ajili ya timu itakayotaka kumsajili Cristiano Ronaldo. Kumekuwa na tetesi mbalimbali kuhusu kurejea kwa nyota huyo Old Trafford hivyo taarifa hizo zinaweza kuwa muhimu kwa United kufikia lengo lao. Klabu ya Arsenal inaongoza mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Palermo Paulo Dybala ambapo viongozi wake wanajipanga kukutana na rais wa timu hiyo Maurizio Zamparini. Arsenal wanataka kutenga kitita cha euro milioni 40 kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Argentina kabla ya majira ya kiangazi. Klabu ya West Ham United nayo imeingia katika kinyang’anyiro cha kuwania kumsajili mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Paris Saint-Germain Nene. Nene mwenye umri wa miaka 33 kwasasa ni mchezaji huru baada ya kusitisha mkataba wake na klabu ya Al Gharafa na pia anawindwa na klabu ya West Bromwich Albion. Klabu ya Paris Saint-Germain bado ina matumaini ya kumsajili Eden Hazard pamoja na nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na Chelsea. Klabu za Chelsea na Manchester United ziko katika mapambano ya kumuwania Rafael Verane. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaonekana hana furaha katika klabu ya Real Madrid kutokana na kupata muda mchache wa kucheza na yuko tayari kuondoka, ingawa klabu hizo za Ligi Kuu zitalazimika kutoa paundi milioni 25 kama watamuhitaji.

Monday, February 16, 2015

TETESI ZA USAJILI: ATLETICO YAMTAKA CAZORLA, AJAX YAMNYEMELEA VAN DE VAART.

KATIKA habari za tetesi za usajili zilizopamba vichwa vya habari na mitandao mbalimbali barani Ulaya ni pamoja na taarifa kuwa kiungo wa Arsenal Santi Cazorla amekubali uhamisho wa kwenda Atletico Madrid. Hatua hiyo imekuja kufuatia taarifa kuwa tayari klabu hizo zilishafikia makubaliano huku kocha wa Atletico Diego Simeone sasa akikabiliwa na kibarua cha kuishawishi Arsenal kuhusu ada ya usajili. Kwingineko nyota wa Barcelona Ivan Rakitic anaripotiwa kuzitolea nje klabu za Arsenal na Manchester United ambazo zilikuwa zikiwinda saini yake katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari. Kiungo wa zamani wa Real Madrid, Lassana Diarra ana matumaini West Ham United bado wanakuwa wakimhitaji mwishoni mwa msimu huu. Diarra alinjimwa kibali cha kujiunga na West Ham Januari na sasa anatakiwa kusubiri mpaka mwishoni mwa msimu ili aweze kutafuta klabu mpya. Klabu ya Ajax Amsterdam imedai kuwa na matumaini ya kumnyakuwa kiungo wa Hamburg Van Der Vaart ambaye mkataba wake unamalizika katika majira ya kiangazi. Klabu ya Atletico Madrid inajipanga kutenga fungu kwa ajili ya kiungo wa Manchester United Juan Mata. Mata mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na United mwaka mmoja uliopita akiwagharimu paundi milioni 37.1 lakini Atletico wamepania kuwajaribu United kama bado wanamhitaji nkiungo huyo.