Wednesday, February 1, 2012

MENSAH FITI KUIVAA GUINEA.

NAHODHA wa Ghana John Mensah anaamini kuwa atakuwa amepona ndani ya muda na kuwemo katika kikosi cha Ghana kitakachocheza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Guinea. Katika mchezo huo Ghana itahitajika ishinde na kuongoza kundi lao ili ibakie jijini Franceville na nahodha huyo anadai sasa anajisiki vyema baada kuumia na kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Botswana. Mensah hakushiriki mazoezi na wenzake Jumapili asubuhi lakini anaweza kucheza baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja kutokana na kadi nyekundu aliyopewa ambapo kocha wa timu hiyo itabidi aumize kichwa baada ya kuwa na mabeki wa kati wanne. Nahodha huyo alitazama kikosi chake kilipoifunga Mali akiwa benchi na kusema kuwa amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu hiyo wakati yeye akiwa hayupo.

AMR ZAKI APATA OFA YA KUJIUNGA NA MISR ELMQASAH.

MSHAMBULIAJI wa Zamalek Amr Zaki amepata mwaliko wa kujiunga na klabu ya Misr Elmqasah katika msimu wa pili wa Ligi Kuu ya Misri mkataba ambao utakuwa ni wa miezi sita. Akihojiwa kocha mkuu wa Elmqasah Tarek Yehia amesema kuwa anaamini mchezaji huyo atajiunga katika kikosi chake kwakuwa ni mchezaji mzuri na anamuhitaji katika msimu wa pili wa ligi hiyo. Zaki hataitumikia klabu yake ya Zamalek kwa kipindi kirefu cha msimu wa kwanza kutokana na mgogoro wa mshahara lakini klabu hiyo imedai imeshalimaliza tatizo hilo. Mchezaji huyo alijiunga na Zamalek mwaka 2006 ambapo pia alishawahi kuchezea vilabu kadhaa nchini Uingereza zikiwemo Wigan Athletic mwaka 2009 na Hull City 2010.

AMOROS APEWA MKATABA WA MIAKA MIWILI.

Manuel Amoros
BEKI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Manuel Amoros amepewa mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Benin. Rais wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo Moucharafou Anjorin amesema kuwa Amoros ndiye mgombea na baada ya kusafiri kuelekea jijini Cotonou alikubali kusaini mkataba huo utakaomuwezesha kumuweka nchini humo mpaka 2014. Amoros ambaye ana miaka 50 aliwahi pia kwa kipindi kifupi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Comoros mwaka 2010 na wakati akiwa mchezaji aliwahi kushiriki mara mbili michuano ya Kombe la Dunia na pia alikuwemo katika kikosi cha Ufaransa kilichonyakuwa Kombe la Ulaya mwaka 1984. Mchezo wa kwanza akiwa kocha wa Benin uwakuwa ni dhidi ya Ethiopia Februari 29 mwaka mchezo ambao utakuwa ni wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.

FULHAM YAMNYAKUWA MSHAMBULIAJI WA URUSI.

Pavel Pogrebnyak
Klabu ya Fulham imenyakuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Urusi Pavel Pogrebnyak kutoka klabu ya Stuttgart na kumuuza mchezaji wake Bobby Zamora kwa mahasimu wao jijini London klabu ya Queens Park Rangers katika kipindi cha mwisho cha usajili wa dirisha dogo la usajili jana. Pogrebnyak mwenye umri wa miaka 28 amejiunga na Fulham kwa mkataba wa miezi sita ambapo alikuwa sehemu ya kikosi cha Urusi kilichoongoza kundi B katika kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya itakayofanyika baadae mwaka huu. Uhamisho huo umemuwezesha Zamora kujiunga na kocha wake wa zamani Mark Hughes katika klabu ya QPR. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu na QPR ambapo sas atacheza pamoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Djibril Cisse ambaye nae alikamilisha taratibu za uhamisho mapema jana.

Gabon vs Tunisia 1-0 All Goals & Highlights 31/01/2012 CAF Africa Cup 2012

Niger Vs Morocco 0-1 All Goals -HD