Thursday, October 25, 2012

SEREA AMGARAGAZA TENA AZARENKA.

MCHEZAJI nyota anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake mwanadada Victoria Azarenka amebakia katika mashaka kama atamaliza mwaka huu katika nafasi hiyo baada ya kufungwa na Serena Williams kwa mara ya tano katika vipindi tifauti walivyokutana mwaka huu. Azarenka ambaye anatoka Belarus alikubali kufungwa kwa 6-4 6-4 naWilliams kutoka Marekani katika michuano ya WTA inayofanyika jijini Istabul ambapo sasa itabidi ahakikishe anamfunga Li Na bingwa wa zamani wa michuano ya wazi ya Ufaransa kutoka China ili aweze kujihakikishia nafasi hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Williams amesema kuwa alifanya mazoezi ya nguvu ili aweze kucheza vyema na anatarajia ataendlea kufanya vyema na kama ikishindikana atajaribu kufanya hivyo tena mwakani. Azarenka ambaye alifungwa na Williams katika michuano ya wazi ya Marekani mwezi uliopita alianza vyema mchezo huo kwa kuongoza katika seti ya kwanza lakini Williams ambaye naye alikuwa akicheza chini ya kiwango alikuja juu na kuhakikisha hapotezi mchezo huo muhimu.

MADRID, MILAN, CITY, ARSENAL ZAANGUKIA PUA CHAMPIONS LEAGUE.

KLABU za Real Madrid, Manchester City, Arsenal na AC Milan zimeshindwa kutamba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kukubali vipigo katika michezo yao ya jana na kujiweka katika nafasi ngumu ya kusonga mbele katika michuano hiyo. Timu za Ujerumani zilionyesha kiwango bora jana baada ya mabingwa wa Bundesliga Borussia Dortmund kuwafunga mabingwa mara tisa wa michuano hiyo Madrid kwa mabao 2-1 nyumbani wakati mahasimu wao Schalke 04 wenyewe walifanikiwa kupata ushindi ugenini kwa kuingamiza Arsenal kwa mabao 2-0. Mabingwa mara saba wa michuano hiyo Milan wameendelea kucheza kwa kiwango cha chini baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 nyumbani kwa Malaga timu ambayo imekuwa ikisumbuliwa na ukata lakini wamekuwa wakifanya vyema katika kundi C wakiwa na alama nyingi zaidi. Mabingwa wa Ligi Kuu chini Uingereza, Manchester City ambao waliishia katika hatua ya makundi msimu uliopita nao wamejikuta wakijiweka tena katika nafasi ya hatari ya kutoka baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka Ajax Amsterdam na kujikuta wakishika mkia katika kundi D kwa kukusanya alama moja katika michezo mitatu.

IVORY COAST, TOGO, TUNISIA, ALGERIA KUNDI LA KIFO AFCON 2013.

WENYEJI wa michuano ya Mataifa ya Afrika 2013, Afrika Kusini itakata utepe wa michuano hiyo kwa kucheza na Cape Verde ambao waliwashangaza mabingwa wa zamani wa Afrika Cameroon na kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza. Morocco ambao watakuwa wenyeji wa michuano hiyo mwaka 2015 sambamba na Angola ndio wanakamilisha timu za kundi A. Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Zambia wamepangwa kundi moja na Nigeria pamoja na Ethiopia na Burkina Faso katika kundi C huku kundi B likiwa na timu za Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Niger na Mali. Katika Kundi D ambalo wadau wengi wa mchezo wa soka wanasema ndio kundi la kifo lina timu za Ivory Coast, Togo, Tunisia na Algeria ambapo michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 19 mpaka Februari 10 mwakani.

ETO'O AMPONDA SONG.

MSHAMBULIAJI nyota wa Cameroon, Samuel Eto’o amemkosoa mchezaji mwenzake Alex Song kwa kudai kuwa hajafikia kiwango cha mchezaji nyota wa dunia. Eto’o mwenye umri wa miaka 31 ambaye anakipiga katika klabu ya Anzhi Makhachkala ya nchini Urusi amekuwa na uhusiano usio wa kuridhisha na kiungo huyo wa Barcelona toka Song alipokataa kushikana mikono naye katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Senegal mwaka uliopita. Akihojiwa na luninga moja nchini Ufaransa kama nyota hao wana mgogoro unaoendelea, Eto’o amesema kuwa hakuna mgogoro unaondelea kati ya nyota wawili kwani yeye ni mmoja wa wachezaji bora duniani na Song hata Cameroon sio mmoja wa wachezaji bora. Wachezaji hao walionekana kama wamshamaliza matatizo yao katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde lakini Eto’o ana wasiwasi kwamba hakutaweza kuwa na maridhiano baina yake na Song. Tetesi zinasema kuwa uhasama wa wachezaji umeongezeka kutokana na Song kutaka kumnyang’anya kitambaa cha unahodha Eto’o ambaye alifungiwa kwa miezi nane baada ya kushawishi wachezaji wenzake kugoma wakidai posho zao. Eto,o amenyakuwa tuzo ya mchezaji bora duniani mana nne huku akiwa ndiye mfungaji anayeongoza kwa mabao mengi kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika katika kipindi chote baada ya kufunga mabao 18. 

Dortmund vs Real Madrid 2 1 All Goals & Highlights 24 10 2012

Ajax Amsterdam Vs Manchester City 3-1 All Goals And Highlights [Oct.24 2...