Wednesday, April 3, 2013
TEVEZ KUTUMIKIA JAMII KWA SIKU 250.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza, Carlos Tevez ameamriwa kufanya kazi za kijamii kwa saa 250 baada ya kukutwa na hatia ya kuendesha gari wakati amesimamishwa na bila bima. Tevez mwenye umri wa miaka 29 pia amefungiwa kuendesha gari kwa kipindi cha miezi sita na kutozwa faini ya paundi 1,000. Nyota huyo alikamatwa baada ya kukiuka adhabu yake ya kufungiwa kuendesha gari aliyopewa mara ya kwanza kwa kosa la kushindwa kujibu barua ya polisi kuhusu gari lake kukutwa katika mwendo kasi. Mahakimu hao walisikia kuwa tevez hakuwa na leseni ya udereva ya Uingereza kwasababu alikuwa akishindwa kufaulu majaribio aliyopewa ili kupata leseni ya kuendesha nchini humo. Tevez alikamatwa Machi 7 mwaka huu akiendesha gari bila bima na huku amefungiwa na kuelekwa katika kituo cha karibu ambapo baadae alitolewa kwa dhamana.
MESSI HATI HATI KUWEPO KUWAPOKEA PSG WIKI IJAYO.
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi ameumia msuli wa paja wakati wa mchezo wa kwanza wa robo fainali kati ya timu yake na Paris Saint Germain ambao walikwenda sare kwakufungana mabao 2-2. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 25 ambaye aliifungiwa timu yake bao la kwanza katika dakika ya 38 aliumia dakika chache baadae na kulazimika kutolewa nje katika muda wa mapumziko. Messi ambaye alibadilishana na kiungo wa timu hiyo Cesc Fabregas anatarajiwa kufanyika vipimo zaidi ili kugundua ukubwa wa tatizo lake. Mbali na Messi Barcelona pia ilipata pigo lingine baada ya beki wake Javier Mascherano naye kutolewa nje kwa machela baada ya kuumia mguu wake wa kulia dakika ya 88 ya mchezo huo na anatarajiwa kukaa nje kwa kipindi cha wiki nne mpaka sita.
Tuesday, April 2, 2013
LIVERPOOL KUZURU THAILAND.
KLABU ya Liverpool kucheza mechi za kirafiki nchini Thailand ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na msimu wa 2013-2014. Liverpool ambao ni mabingwa mara tatu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya watachuana na timu ambayo itatangazwa baadaye katika Uwanja wa Taifa wa Rajamangala jijini Bangkok Julai 28 mwaka huu. Mkurugenzi Mtendaji wa Liverpool, Ian Ayre amesema mara ya kwanza timu hiyo kwenda huko ilikuwa ni mwaka 2001 na mpaka sasa wameshakwenda mara nne hiyo inaonyesha jinsi gani wanavyowajali mashabiki wao waliopo nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu hiyo inaaminika kuwa na mashabiki wapatao milioni 14 nchini Thailand na mara ya mwisho kwenda huko ilikuwa mwaka 2009. Mbali na kwenda nchini Thailand klabu hiyo pia imepanga kucheza mechi zingine za kujipima nguvu katika nchi za Australia na Indonesia.
COMORO KUCHEZESHA MECHI YA AZAM.
MWAKYEMBE MGENI RASMI MEDIA DAY BONANZA.
WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza la vyombo vya habari linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA). Bonanza hilo litafanyika Jumamosi wiki hii viwanja vya Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa moja usiku likidhaminiwa na na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Pamoja na mambo mengine, Waziri Mwakyembe atakabidhi zawadi za vikombe na medali kwa washindi mbalimbali watakaoibuka siku hiyo, pia atapata fursa ya kuzungumza na washiriki wa bonanza hilo. Lengo la bonanza ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja na huwa linafanyika mara moja kwa mwaka, likiandaliwa na TASWA. Bonanza hilo ambalo litahusisha wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari litaambatana na michezo mbalimbali itakayohusisha vyombo vyote vitakavyoshiriki na pia kutakuwa na burudani ya muziki. Tunataka bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia mgeni rasmi, burudani, michezo na mambo mengine yawe ya kuvutia, ambapo Alhamisi Aprili 4,2013 saa tano asubuhi kutakuwa na mkutano na wanahabari mgahawa wa City Sports Lounge, Posta Dar es Salaam ambao ni maalum kutangaza makundi yatakayotumbuiza kwenye Media Day na tunatarajia makundi hayo nayo yatakuwepo kwenye mkutano huo. Tunaomba vyombo vya habari ambavyo havijathibitisha ushiriki wao kwa njia ya maandishi vifanye hivyo kama vilivyoagizwa kwenye barua zao za mialiko, vinginevyo ushiriki wao hautathaminika. Bonanza litaanza saa tatu asubuhi, ambapo baadhi ya michezo itakayoshindaniwa ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu, mbio za magunia, mbio meta 100, kuruka kichura, kuvuta kamba, kucheza muziki na kuimba.
BECKHAM ATAMANI KUITUMIKIA UINGEREZA.
NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, David Beckham amesema bado ana matumaini ya kuichezea nchi yake katika siku za usoni. Akihojiwa na kituo cha CNN kiungo huyo ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Paris saint-Grmain-PSG ya Ufaransa amesema anajua amekaribia kufikisha umi wa miaka 38 hivyo nafasi yake ya kuitwa ni ndogo lakini amedai huwezi kujua nini kitatokea huko mbele. Beckham ni mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha Uingereza lakini hajaitwa na timu hiyo toka Octoba mwaka 2009. Nyota huyo amesema mojawapo ya vitu vinavyomfanya asistaafu kucheza soka la kimataifa ni kwasababu kama nafasi itatokea ya kuitwa tena yeye atakuwa tayari. Kiungo huyo amejumuishwa katika kikosi cha PSG ambacho kitakuwa na kibarua kizito kwa kuikaribisha Barcelona katika mchezo wa kwanza robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
NASRI AMTUHUMU KREONKE KUHUSU KUONDOKA KWAKE ARSENAL.
KIUNGO wa zamani wa klabu ya Arsenal, Samir Nasri amemtuhumu mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke kumuuza Manchester City kwasababu alikuwa akitaka fedha kauli ambayo itazorotesha zaidi uhusiano wake na waajiri wa zamani. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger siku zote amesisitiza kuwa hakuwepo katika msukumo wowote wakati anamuuza Nasri kwenda City kwa ada ya paundi milioni 24 Agosti mwaka jana, pamoja na kwamba kiungo huyo wa Ufaransa alikuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake. Nasri amesema Wenger alimwambia kuwa kama Cesc Fabregas ataondoka yeye atabakia lakini Kroenke alikuwa akihitaji fedha ndio maana akaamua kuondoka. Kiungo huyo alimalizia kuwa hajuti kujiunga na City na kuondoka kwake Arsenal ni kwasababu za kimichezo sio kifedha kama wengi wanavyodai.
Subscribe to:
Posts (Atom)






