Sunday, May 26, 2013
AGUERO AJITIA KITANZI CITY MPAKA 2017.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester City, Sergio Aguero ameongeza mkataba wa mwaka mmoja ambao utamuweka katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza mpaka mwaka 2017. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 12 katika mechi 30 za ligi alizocheza msimu uliopita na kufunga bao la ushindi dhidi ya Queens Park Rangers lililowapa taji la ligi katika msimu wa 2011-2012. Mara baada ya kusaini mkataba huyo Aguero aliuambia mtandao wa klabu hiyo kwamba anajisikia furaha na kuhitajika hivyo atafanya kila awezalo ili aendelee kufanya kazi vyema na kuipa mataji klabu hiyo. Vyombo vya habari nchini Uingereza vilikuwa vikiripoti kuwa mchezaji huyo anaweza kutimkia Real Madrid lakini tetesi hizo zitakwisha baada ya kuwa mchezaji mwingine wa timu hiyo kuongeza mkataba baada ya Gael Clichy, Yaya Toure na David Silva kufanya hivyo.
SUALA LA KUONDOKA KWANGU HALIHUSIANI NA MASUALA YA FEDHA - ANCELOTTI.
MENEJA wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Carlo Ancelotti amesisitiza kuwa ombi lake la kuondoka klabuni hapo ni suala la binafsi na halihusiani na mambo ya kifedha. Akiongea kabla ya mechi ya mwisho ya Ligi Kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 dhidi ya Lorient, Ancelotti aliongeza kuwa hajazungumza na klabu yoyote toka aweke wazi kutaka kwake kuondoka mwishoni mwa wiki iliyopita. Kocha huyo aliendelea kusema kuwa uamuzi wa kutaka kuondoka ni wa binafsi zaidi na hauhusiani na mtu au kiongozi yoyote ndani ya klabu hiyo na pia siyo suala la fedha. Anceloti Jumapili iliyopita alibainisha kuwa kuna uwezekano akaelekea kuifundisha klabu ya Real Madrid baada ya Jose Mourinho kutangazwa kuondoka mwishoni mwa msimu lakini klabu hiyo imeonekana haitaki kumuachia kocha huyo. Hata hivyo Ancelotti amesisitiza kuwa hakuna chochote kilichoongelewa kwa wiki hii na mambo yote yapo kama yalivyozungumzwa wiki iliyopita.
TAIFA STARS KWENDA ADDIS ABABA LEO.
TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuondoka leo (Mei 26 mwaka huu) usiku kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo itaweka kambi na kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya kwenda Morocco. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka saa 5 usiku kwa ndege ya EgyptAir ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 chini ya nahodha wake kipa Juma Kaseja. Timu hiyo ikiwa Ethiopia, Juni 2 mwaka huu itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan ambapo siku inayofuata itaondoka kwenda Marrakech, Morocco kwa kupitia Cairo, Misri. Mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.
Mbali ya nahodha Kaseja, wachezaji wengine wanaoondoka katika kikosi hicho ambacho kina wiki sasa tangu kingie kambini jijini Dar es Salaam ni Mwadini Ally na Ally Mustafa ambao wote ni makipa. Wengine ni Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Aggrey Morris, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd na Haruni Chanongo. Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wako na timu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watajiunga moja kwa moja na Stars jijini Marrakech, Juni 4 mwaka huu wakitokea Maputo, Msumbiji mara baada ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya huko. Katika msafara huo wa Ethiopia benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Mbali ya nahodha Kaseja, wachezaji wengine wanaoondoka katika kikosi hicho ambacho kina wiki sasa tangu kingie kambini jijini Dar es Salaam ni Mwadini Ally na Ally Mustafa ambao wote ni makipa. Wengine ni Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Aggrey Morris, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd na Haruni Chanongo. Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wako na timu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watajiunga moja kwa moja na Stars jijini Marrakech, Juni 4 mwaka huu wakitokea Maputo, Msumbiji mara baada ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya huko. Katika msafara huo wa Ethiopia benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
SISI NI KIZAZI CHA DHAHABU CHA BAYERN - LAHM.
BEKI wa kati wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich, Philipp Lahm anaamini kuwa ushindi wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya unakifanya kikosi cha timu hiyo kuwa kizazi cha dhahabu. Bayern ambao wanajulikana pia kama The Bavarians walishindwa mara mbili katika hatua ya fainali ya michuano hiyo katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita lakini bao la ushindi la dakika ya 89 lililofungwa na Arjen Robben liliwahakikishia ushindi mabao 2-1 dhidi ya wajerumani wenzake Borussia Dortmund. Lahm anaamini ushindi huo waliopata katika Uwanja wa Wembley utakuwa chachu ya kufanya vizuri zaidi katika mchezo wao mwingine wa fainali ya Kombe la Ujerumani itakayofanyika Juni mosi katika Uwanja wa Allianz Arena huku tayari wakiwa wameshanyakuwa taji la Bundesliga.
Nyota huyo aliendelea kusema kuwa kama mchezaji unahitaji kuweno katika kizazi cha dhahabu unatakiwa kushinda mataji makubwa na anashukuru walifanya hilo jana.
NEYMAR KUSAINI MKATABA WA MIAKA MITANO BARCELONA.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar amesema kuwa anatarajia kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Barcelona ya Hispania Jumatatu. Neymar alichagua Barcelona na kuwatema mahasimu wao Real Madrid baada ya klabu yake ya Santos kumaliza utata wa kumng’ang’ania mchezaji huyo kwa kipindi cha miaka mitatu na kumwachia kuondoka kabla ya michuano ya Kombe la Dunia 2014. Nyota huyo alithibitisha hayo katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram na Twitter kwamba atasaini mkataba wa miaka mitano kesho huku klabu ya Santos kwenye ukurasa wake wa facebook na katika mtandao wa Barcelona wote wakithibitisha uamuzi huo wa Neymar. Neymar aliongeza kuwa familia na marafiki zake tayari wote wanajua kuhusiana na uamuzi wake huku akiwashukuru mashabiki wa Santos kwa kuwa pamoja naye katika kipindi cha miaka tisa ambayo amekuwepo hapo.
Saturday, May 25, 2013
ADEBAYOR AITWA TOGO.
KOCHA wa timu ya taifa ya Togo, Didier Six amemuita mshambualiaji nyota na nahodha wan chi hiyo Emmanuel Adebayor katika kikosi chake ambacho kinakabiliwa na mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon Juni 9 na Libya Juni 16 mwaka huu. Mshambuliaji huyo anayecheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs hakutokea mara ya mwisho alipoitwa na kocha huyo kwa ajili ya mchezo dhidi ya Cameroon uliochezwa Machi mwaka huu. Adebayor amekuwa katika mzozo na kocha huyo raia wa Ufaransa ambaye amedai kuwa ndio alikuwa chanzo cha nchi hiyo kung’olewa katika michuano ya Mataifa ya Afrika yaliyofanyika Afrika Kusini 2013. Six pia amemuita golikipa Kossi Agassi ambaye amekuwa katika mzozo na Shirikisho la Soka nchini humo kuhusiana na masuala ya posho. Togo kwasasa inashika nafasi ya pili katika kundi I wakipisha alama moja na Cameroon ambao wanaongoza kundi hilo wakifuatiwa na Libya alama tano na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alama nne.
Subscribe to:
Posts (Atom)








