TAKWIMU mpya zilizotolewa zimebainisha kuwa klabu za Ligi Kuu zimetumia zaidi ya paundi bilioni moja katika usajili wa msimu mmoja kwa mara ya kwanza. Kiasi cha paundi milioni 965 kilivunja rekodi ya msimu wa 2014-2015, lakini tayari rekodi hiyo imeshapitwa huku klabu bado zikiwa na muda wa kusajili wachezaji zaidi mpaka ifikapo leo saa sita usiku dirisha litakapofungwa. Klabu 20 za Ligi Kuu tayari zimeshatumia paundi milioni 130 katika kipindi hiki cha usajili wa Januari pekee, huku Newcastle United ndio klabu iliyotumia fedha nyingi zaidi mpaka sasa wakitumia paundi milioni 29. Klabu hiyo imewasajili Jonjo Shelvey, Andros Townsend na Henri Saivet huku wakiwa tayari wametuma maombi ya paundi milioni 21 kwa ajili ya kuwania mshambuliaji wa West Bromwich Albion Saido Berahino.

Monday, February 1, 2016
BENFICA HAINA HOFU JUU YA TETESI ZA KUONDOKA SANCHEZ.
KLABU ya Benfica imedai kutohofia tetesi za Manchester United kumuwania kiungo wake chipukizi Renato Sanchez. United inaripotiwa kuwa tayari kutoka euro milioni 30 kwa ajili ya kumsajili Sanchez ambaye aliibuka katika kikosi cha kwanza cha Benfica msimu huu. Akihojiwa meneja wa Benfica Rui Vitoria amesema hana shaka yeyote kuhusu chipukizi huyo kuwaniwa na vigogo wa soka wa Uingereza. Benfica wanadaiwa kuweka kiasi cha euro milioni 80 kwa klabu ambayo iatatka kuvunja mkataba wa chipukizi huyo wa kimataifa wa Ureno. Meneja wa United, Louis van Gaal bado hajafanya usajili wowote katika kipindi hiki cha usajili wa Januari.
RONALDO AMMWAGIA SIFA ZIDANE BAADA YA HAT TRICK.
MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema kujituma kwa bidii mazoezini chini ya meneja mpya Zinedine Zidane kumewasaidia na kusifia mbinu za Mfaransa huyo kuwa nzuri kuliko wenzake waliomtangulia. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alifunga hat-trick katika ushindi wa mabao 6-0 wa La Liga waliopata dhidi ya Espanyol katika Uwanja wa Santiago Bernabeu jana. Ronaldo sasa anakuwa amefikisha mabao 19 na kumfanya kuungana na nyota wa Barcelona Luis Suarez kuwa wachezaji wanaoongoza kwa mabao mpaka sasa. Mabao mengine ya Madrid yalifungwa na Karim Benzema na James Rodriguez huku la sita likiwa la kujifunga wenyewe kupitia kwa Oscra Duarte. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Ronaldo alimpongeza Zidane kwani amekuwa akifanya kazi nzuri kutokana na mbinu zake tofauti ambazo imekuwa rahisi kwa wachezaji kuzizoea haraka.
CHELSEA BADO MGUU NJE MGUU NDANI KWA TERRY.
KLABU ya Chelsea, imesisitiza kuwa haijafunga milango ya uwezekano wa kumuongeza mkataba mwingine nahodha wake John Terry baada ya msimu huu. Terry alibainisha baada ya mchezo ambao Chelsea walishinda mabao 5-1 dhidi ya MK Dons katika mzunguko wa tano wa Kombe la FA jana, kuwa ametaarifiwa kuwa mkataba wake wa sasa hautaongezwa. Lakini wakati Chelsea wakithibitisha kukata kumpa ofa ya mkataba mpya Terry katika kikao kilichoombwa na mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35, bado wanadai hawajafikia uamuzi wa mwisho kuhusiana na suala lake. Taarifa ya klabu hiyo imedai kuwa Teery aliomba kukutana na viongozi wiki mbili zilizopita na kuuliza kuhusu uwezekano wa kuongeza mkataba mwingine lakini jibu alilopewa halikuwa la moja kwa moja kwani mambo yanaweza kubadilika na kuongeza mkataba mwingine. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa Chelsea inatambua mchango wa Terry akiwa kama mchezaji na nahodha katika kipindi chaote ambacho amekuwa akiwatumikia ndio maana bado milango iko wazi kwake.
MARSEILLE YAKARIBIA KUMCHUKUA ODEMWINGIE.
KLABU ya Olympique Marseille inatarajia kukamilisha usajili wa mkopo wa Peter Odemwingie kutoka Stoke City. Inaripotiwa kuwa klabu hiyo ya Ufaransa inataka kumchukua Edemwingie kwa mkopo wa mpaka mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria anadaiwa kuwa tayari ameshatua Ufaransa leo kwajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilihsa mambo binafsi katika uhamisho huo. Marseille jana walituma maombi ya kumtaka mshambuliaji huyo ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
AC MILAN YAACHANA NA DE JONG, AAMUA KUTIMKIA MERKANI.
HAKUNA USAJILI MWINGINE KWA ARSENAL LABDA ATOKEE MESSI - WENGER.
MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ana uhakika wa asilimia 99 kuwa klabu hiyo haitafanya usajili katika dakika hizi za mwisho labda utokee uwezekano wa kumnasa Lionel Messi. Arsenal imemsajili Mohamed Elneny pekee katika kipindi hiki cha usajili wa Januari na kuifanya klabu hiyo kuwa kimya sana katika muda wote wa usajili. Wenger hategemei usajili wa dakika mwishoni kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo baadae saa sita usiku lakini amekiri kuwa itawezekana tu kama kuna mchezaji wa kipekee atakayetokea ghafla. Akihojiwa Wenger amesema kipindi chote cha usajili wa dirisha dogo kimekuwa kimya kuliko alivyotegemea na hilo limetokana na kukosekana kwa aina ya wachezaji aliowahitaji. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa maajabu yanaweza kutokea siku zote lakini ana uhakika wa asilimia 99 kuwa hakuna usajili mwingine utakaofanyika labda Messi atokee dakika za mwisho kwani hawezi kumkataa nyota huyo wa Barcelona.
Subscribe to:
Posts (Atom)