KLABU ya Leicester City imekata rufani kupinga kadi nyekundu alioonyeshwa mshambuliaji wao Jamie Vardy katika mchezo wa Jumamosi iliyopita uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Stoke City. Vardy alilimwa kadi hiyo katika dakika ya 28 baada ya kumkwatua kwa miguu miwili Mame Diouf. Kama rufani hiyo ikikataliwa nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza atatumikia adhabu ya kutocheza mechi tatu hivyo kukosa mechi dhidi ya Everton, West Ham United na Middlesbrough. Mabingwa hao wa Ligi Kuu wamesema kuwa wanatarajia kusikia matokeo ya rufani yao katika siku za karibuni.
Tuesday, December 20, 2016
Sunday, December 18, 2016
RONALDO APIGA HAT-TRICK MADRID IKITWAA TAJI LA KLABU BINGW AYA DUNIA.
KLABU ya Real Madrid mapema leo imefanikiwa kutwaa taji lake la pili katika kipindi cha miaka mitatu baada ya kuichapa Kashima Antlers ya Japan katika mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia. Katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Nissan jijini Yokohama Madrid walipata bao la mapema kupitia kwa Karim Benzema lakini wenyeji walicharuka na na kusawazisha bao hilo kabla ya mapumziko kupitia kwa nyota wao Gaku Shibasaki. Kipindi cha pili Kashima walipata bao lingine kupitia kwa Shibasaki kabla ya Cristiano Ronaldo hajasawazisha bao hilo kwa penati na kupelekea mchezo huo kwenda kwenye muda wa nyongeza. Ronaldo alifunga mabao mengine mawili kwenye muda wa nyongeza na kuweka historia mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick katika historia ya michuano hiyo. Ushindi huo pia unafanya timu za Ulaya kutwaa taji hilo mara tisa kati ya 10.
Thursday, December 15, 2016
STURARO ASAINI MKATABA MPYA JUVENTUS.
KIUNGO Stefano Sturaro amekuwa mchezaji wa pili wa Juventus wiki hii kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na mabingwa hao wa Serie A. Mapema jana beki Daniele Rugani alisaini mkataba wa miaka mitano na sasa kufuatiwa na Sturaro saa 24 baadae. Kiungo huyo alijiunga na Juventus akitokea Geona mwaka 2014, kabla ya kutumia kipindi chote cha msimu wa 2014-2015 akiwa kwa mkopo kwenye klabu hiyo iliyomkuza. Februari mwaka jana aliitwa Juventus na kufanikiwa kucheza mechi 19 za Serie A msimu uliopita na kufunga bao moja. Msimu huu Sturaro amecheza mechi 13 za mashindano yote lakini bado hajabahatika kufunga bao.
LIGI YASIMAMA DRC KUHOFIA VURUGU.
SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC, imelitaka Shirikisho la Soka la nchini hiyo kusimamisha mechi za ligi kuanzia leo mpaka hapo itakapotolewa taarifa zaidi. Hatua hiyo imekuja kufuatia hofu ya vurugu pindi rais Joseph Kabila atakapomaliza muda wake wa kuwepo madarakani wiki ijayo. Katibu Mkuu wa wizara ya michezo ya nchi hiyo, Barthelemy Okito amesema wanahofu jinsi hali ilivyo hivi sasa inaweza kuhamia viwanjani na kuhatarisha maisha ya watu. Kikatiba muda wa rais Kabila kukaa madarakani unamalizika Desemba 19 mwaka huu lakini mwenyewe ameshasema kuwa ataendelea kuwepo madarakani mpaka Aprili mwaka 2018 wakati serikali itakapokuwa imejipanga kwa ajili ya uchaguzi mwingine baada ya ule wa mwaka huu kuvurugika.
RONALDO APIGA BAO LA 500 MADRID IKITINGA FAINALI KLABU BINGWA YA DUNIA.
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo mapema leo amefunga bao lake la 500 kwa klabu katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Club America kwenye michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia. Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, alifunga bao lake la 500 kwa klabu na nchi yake katika mchezo dhidi ya Malmo Septemba mwaka jana na sasa amefikisha bao la 500 kwa klabu pekee. Nyota huyo alifunga bao hilo katika dakika 90 ya mchezo akiwahadaa walinzi wa America lakini ilibidi asubiri mwamuzi Enrique Caceres wa Venezuela kwenda kuangalia upya kama alikuwa kaotea kupitia mfumo mpya wa picha za video wa VAR unaotumika kwenye michuano hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye alijiunga na Madrid kwa ada iliyovunja rekodi mwaka 2009, amefunga bao lake la 500 katika mechi 689 pekee alizocheza. Ronaldo alifunga bao lake la 377 katika mechi 367 na pia alifunga mabao 118 katika mechi 292 alizoichezea Manchester United na matano katika mechi 31 alizocheza Sporting Lisbon.
KLOPP AMUWINDA WINGA WA GHANA.
MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp anadaiwa kuwa tayari kumuwania winga wa Anderlecht Frank Acheampong katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari mwakani. Klopp amekuwa akituma watu wake wamfuatilie nyota huyo wa kimataifa wa Ghana mara kadhaa na sasa anafikiria kumchukua kabisa Januari. Ingawa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 huwa anacheza kama winga wa upande wa kushoto lakini pia anaweza kucheza kama beki wa kushoto, idara ambayo Klopp anataka kuiboresha zaidi. Acheompong ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Ubelgiji miaka mitatu iliyopita, anatarajiwa kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika mwezi ujao hatua ambao inaweza kuyumbisha usajili wake huo.
EVERTON YAMUWANIA SCHNEIDERLIN.
KLABU ya Everton inadaiwa kuanza mazungumzo na Manchester United kwa ajili ya kumleta kiungo Morgan Schneiderlin Goodison Park kipindi cha Januari mwakani. Schneiderlin hajaanza katika mechi yeyote ya Ligi Kuu chini ya Jose Mourinho msimu huu na taarifa zinadai kuwa meneja huyo wa United anaweza kumruhusu Mfaransa huyo aondoke kiangazi kama atapata timu. Meneja wa Everton Ronald Koeman aliwahi kufanya kazi na Schneiderlin wakati wote wakiwa Southampton na sasa anataka kutenga kitita cha paundi milioni 24 ili aweze kuungana tena na mchezaji wake huyo wa zamani. Schneiderlin anapitia kipindi kigumu United kwasasa lakini kufanya kazi tena na Koeman inaweza kuwa hatua nzuri kwake ya kuendelea kuimarika zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)






