Kundi A: Villarreal, Maccabi Tel Aviv, Astana, Slavia Prague.
Kundi B: Dynamo Kiev, Young Boys, Partizan Belgrade, Skenderbeu.
Kundi C: Sporting Braga, Ludogorets, Hoffenheim, Istanbul Basaksehir.
Kundi D: AC Milan, Austria Vienna , Rijeka, AEK Athens.
Kundi E: Lyon, Everton, Atalanta, Apollon Limassol.
kundi F: FC Copenhagen, Lokomotiv Moscow, Sheriff Tiraspol, FC Zlin.
Kundi G: Vitoria Plzen, Steaua Bucarest, Hapoel Beer-Sheva, FC Lugano.
Kundi H:Arsenal, BATE Borisov, Cologne, Red Star Belgrade.
Kundi I: Salzburg, Marseille, Vitoria Guimaraes, Konyaspor.
Kundi J: Athletic Bilbao, Hertha Berlin, Zorya Luhansk, Ostersund.
Kundi K: Lazio, Nice, Zulte Waregem, Vitesse Arnhem.
Kundi L: Zenit St Petersburg, Real Sociedad, Rosenborg, Vardar.
Kundi A: Benfica, Manchester United, Basel, CSKA Moscow
Kundi B: Bayern Munich, Paris St-Germain, Anderlecht, Celtic
Kundi C: Chelsea, Atletico Madrid, Roma, Qarabag
Kundi D: Juventus, Barcelona, Olympiakos, Sporting
Kundi E: Spartak Moscow, Sevilla, Liverpool, Maribor
Kundi F: Shakhtar Donetsk, Manchester City, Napoli, Feyenoord
Kundi G: Monaco, Porto, Besiktas, RB Leipzig
Kundi H: Real Madrid, Borussia Dortmund, Tottenham, Apoel
KLABU ya Liverpool inadaiwa kujiandaa kumuwania kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye alitua Allianz Arena majira ya kiangazi mwaka jana, anataka kutafuta timu atakayopata nafasi ya kucheza mara kwa mara na meneja Jurgen Klopp yuko tayari kufanikisha suala hilo. Sanchez ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na kiwnago bora alichoonyesha katika michuano ya Ulaya akiwa na kikosi cha ushindi cha Ureno kiangazi mwaka jana, kwa kipindi kirefu amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwaniwa na Manchester United. Bayern wanaweza kukubali kumuacha kwa mkopo kiungo huyo kwani bado wanamuhitaji nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa siku zijazo.
KLABU ya Tottenham Hotspurs inadaiwa kukubali kumsajili Serge Aurier kutoka Paris Saint-Germain-PSG kwa kitita cha paundi milioni 23 na beki huyo amefanyiwa vipimo vya afya jijini Paris. Lakini usajili wa beki huyo wa kimataifa wa Ivory Coast hautakamilika mpaka Aurier atakapopata kiali cha kufanya kazi Uingereza. Mabingwa Serie A Juventus bado wanamtaka beki huyo kwa mkopo kama akishindwa kuhamia Ligi Kuu. Nyota huyo wa PSG alinyimwa visa ya kuingia Uingereza kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal Novemba mwaka jana kwasababu ya kuhukumiwa kwa kosa la kumshambulia polisi. Mawakili wake wanafanya kazi kutafuta suluhu la suala hilo ambalo ndio lilichangia Chelsea na Manchester United kuacha kuwania saini yake.
KLABU ya West Bromwich Albion imemsajili winga wa kimataifa wa Scotland Oliver Burke kutoka RB Leipzig ya Ujerumani kwa kitita cha paundi milioni 15 na kumpa mkataba wa miaka mitano. Burke mwenye umri wa miaka 20, alikuwa mchezaji ghali zaidi kutoka Scotland wakati alipojiunga na klabu hiyo ya Bundesliga kwa kitita cha paundi milioni 13 Agosti mwaka 2016. Winga huyo amecheza mechi 25 za ligi msimu uliopita na kuisaidia Leipzig kufuzu makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akizungumza na wanahabari baada ya uhamisho huo, Burke amesema anadhani sasa ni wakati wake wa kucheza mechi nyingi zaidi. Burke ambaye anaweza kuanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stoke City Jumapili hii, anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na West Brom kipindi hiki cha majira ya kiangazi.
KLABU ya Borussia Dortmund imedai mapema leo kuwa hakuna makubaliano yeyote yaliyofikiwa kwa ajili ya uhamisho wa Ousmane Dembele kwenda Barcelona. Kauli hiyo ya Dortmund inakuja kufuatia taarifa kutoka nchini Ujerumani kudai kuwa tayari makubaliano baina ya pande hizo kwa ajili ya Dembele yamekamilika. Akizungumza na wanahabari, msemaji wa Dortmund amesema wamewapa muda Barcelona hivyo kuna kitu kinaweza kikatokea au kisitokee pia. Taarifa zingine zinadai kuwa Barcelona imekubali kutoa kitita cha euro milioni 120 hivuo kumfanya kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi duniani baada ya Neymar.
KLABU ya Barcelona inatarajiwa kugeukia kwa Angel Di Maria kama wakishindwa kumsajili Philippe Coutinho kutoka Liverpool. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Catalan zimedai kuwa nafasi ya Barcelona kumsajili kiungo huyo wa Brazil imekuwa finyu hivyo kuna uwezekano klabu hiyo ikaamua kuachana naye. Kutokana na hilo Barcelona sasa inaweza kuhamishia nguvu zao kwa Di Maria ili waimarishe kikosi chao. Katika hatua nyingine, Afisa mkuu wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke amedai kuwa nafasi ya Ousmane Dembele kujiunga na Barcelona ni chini ya asilimia 50. Watzke aliwaambia wanahabari kuwa kama Barcelona wanamtaka Osmane lazima walipe ada wanayotaka kwakuwa mchezaji huyo bado ana mkataba wa miaka minne.