Monday, December 17, 2012

Full HD real madrid vs Espanyol 2-2 2012 All Goals 16-12-2012

BOLT ASHINDA TUZO YA BBC.

MWANARIADHA nyota wa mbio fupi Usain Bolt ameteuliwa kupewa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka kutoka nje tuzo ambayo imetolewa na BBC. Bolt mwenye umri wa miaka 26 raia wa Jamaica aling’ara katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika London mwaka huu baada ya kufanikiwa kutetea medali zake mbili katika mbio za mita 100 na 200 pamoja na zile za kupokezana vijiti za mita 400. Mafanikio hayo aliyopata katika olimpiki yanamfanya kuwa mwanaridha pekee aliweza kutetea medali zake katika michuano ya olimpiki miwili tofauti. Mbali na hivyo Bolt pia anakuwa mwanariadha pekee kuwahi kutokea kwa kunyakuwa medali sita katika olimpiki huku hiyo ikiwa ni mara ya tatu kunyakuwa tuzo hiyo katika kipindi cha miaka mitano.

BARCELONA YAJIKITA ZAIDI KILELENI.

KLABU ya Barcelona imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga baada ya kuisambaratisha Atletico Madrid kwa mabao 4-1 katika mchezo uliochezwa jana usiku. Ushindi huo unaifanya timu hiyo kuongoza La Liga kwa tofauti ya tisa dhidi ya Atletico ambao wanashika nafasi ya pili huku wakiwaacha wapinzani Real Madrid kwa alama 13 baada ya timu hiyo kupata sare ya kushangaza ya mabao 2-2 dhidi ya Espanyol jana. Barcelona mbao wananolewa na kocha Tito Vilanova ilibidi wapambane katika mchezo wa jana baada ya mshambuliaji nyota wa Atletico Radamel Falcao kuipa timu yake bao la kuongoza kabla yaAdriano kusawazisha bao hilo na Sergio Busquest akiongeza lingine huku mabao mengine mawili yakifungwana Messi. Barcelona sasa inaongoza La Liga ikiwa na alama 13 baada ya kucheza michezo 16 wakifuatiwa na Atletico wenye alama 37 huku mabingwa watetezi Madrid wakiwa katika nafasi ya tatu kwakuwa na alama 33.

Sunday, December 16, 2012

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF.

WARAKA WA MAREKEBISHO YA KATIBA YA TFF WAPITA
Waraka wa marekebisho ya Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umepita baada ya kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe wa Mkutano Mkuu waliopiga kura. Jumla ya wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 wameunga mkono wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa, hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho kikatiba. Kura zilizosema ndiyo kutoka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa vyama vya mikoa ni 46, wajumbe kutoka vyama shiriki ni 13 wakati klabu za Ligi Kuu zilizounga mkono ni kumi na moja. Kamati ya Utendaji ya TFF inawashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu- kwa waliounga mkono na waliokataa kwa vile walikuwa wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba. Vipengele vilivyoingizwa ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais. Vilevile Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF. Mkutano Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na 24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya Mkutano Mkuu siku 60 kabla.

MIKOA SITA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI TWFA
Mikoa sita ambayo ni wanachama wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) haitashiriki katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro. Kwa mujibu wa taarifa ya TWFA, wanachama hao hawatashiriki kwa vile hadi sasa haijapokea taarifa za uchaguzi kwenye vyama hivyo. Vyama hivyo ni vya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na Tabora. Uchaguzi huo utafanyika kwenye hoteli ya Midland, na wagombea ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia Mkafum (Katibu Mkuu), Zena Chande (Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji.

MESSI KUSAINI MKATABA MNONO BARCELONA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi anatarajia kusaini mkataba wa maisha na klabu hiyo ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mnono zaidi kuliko mchezaji yoyote wa ligi kubwa barani Ulaya. Baba wa nyota huyo, Jorge tayari amekwishaanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu suala la kuongeza mkataba wa sasa na hiyo inamaanisha kuwa Messi atabakia Barcelona mpaka atapofikisha umri wa miaka 31. Rais wa Barcelona, Sandro Rosell amepanga kumuongeza mkataba wa miaka miwili mchezaji huyo ili kuhakikisha anabakia klabuni hapo kabla ya kumpa mkataba mrefu nyota huyo wa Argentina kabla hajastaafu wadhifa huo. Messi kwasasa anachukua kitita kabla ya posho paundi milioni tisa kwa mwaka akiwa nyumba ya mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic anayechukua paundi milioni 12 kwa mwaka na Samuel Eto’o ambaye anachukua kitita paundi milioni 16 kwa mwaka akiwa na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.

WILSHERE KUONGEZA MKATABA ARSENAL.

KIUNGO Jack Wilshere anatarajia kuipa ahueni klabu yake ya Arsenal pamoja na meneja Arsene Wenger aliyekalia kuti kavu kwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano ambao una thamani ya paundi milioni 20. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20, aliapa kuwa kizazi kipya cha wachezaji wa Arsenal kitaleta furaha katika klabu hiyo ambayo sasa imefikisha miaka saba na nusu bila kunyakuwa taji lolote. Wilshere ambaye anatarajia kukubali kusaini mkataba mpya hivi karibuni ikiwemo mshahara unaoanzia paundi 80,000 kwa wiki pia alibainisha nia yake ya kuja kuwa nahodha wa klabu hiyo katika siku za usoni. Mbali na Wilshere lakini pia winga Alex Oxlade-Chamberlain aye anatarajiwa kusaini mkataba mpya hivyo habari hizo kuwapoza mashabiki wa klabu hiyo ambao wiki iliyopita walishuhudia klabu yao ikitolewa katika Kombela Ligi na Bradford City.

WEST HAM KUIPA WAKATI MGUMU ARSENAL KWA KUMUONGEZA MSHAHARA DIAME.

KLABU ya West Ham United inajipanga kumuongeza mshahara mara mbili ya kiwango anachopata hivi sasa kiungo wake Mohamed Diame ili kuizuia Arsenal kumchukua mchezaji huyo katika kipindi cha dirisha dogo Januari mwaka huu. Kiungo huyo alijiunga na West Ham kama mchezaji huru akitokea Wigan Athletic katika kipindi cha majira ya kiangazi na amekuwa akionyesha kiwango bora toka atue katika klabu hiyo mpaka kuifanya Arsenal ianze kumnyatia. Diame ambaye ni raia wa Senegal anakadiriwa kuwa thamani ya paundi milioni 4.5 lakini maofisa wa West Ham wanajiamini kumbakisha mchezaji huyo kwa kumpa mshahara wa paundi 75,000 ambapo watasababisha na thamani ya mchezaji huyo kupanda pia. Klabu za Newcastle United, Fulham na Liverpool nazo pia zimeonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 lakini Arsenal ndio wenye uhitaji zaidi wa kiungo katika safu yake baada ya Abou Diaby kukaa nje kutokana na majeruhi mara kwa mara.