KLABU ya Guangzhou R&F inayoshiriki Ligi Kuu nchini China, imemteua kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Sven-Gran Eriksson kuwa kocha mpya wa klabu hiyo. Kwa mujibu a taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo Eriksson ambaye ambaye aliachia nafasi yake kama mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Al Nasr ya Muungano wa Falme za Kiarabu, amejiunga na Guanghzou kwa mkataba wa miezi 18. Uteuzi huo utamfanya Eriksson raia wa Sweden kukutana na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Italia Marcello Lippi ambaye anawafundisha mabingwa wa sasa wa ligi hiyo Guangzhou Evergrande. Pamoja na klabu hiyo kutotoa kiasi atakacholipwa Eriksson lakini vyombo vya habari nchini Uingereza vimekisia kuwa kocha huyo atakuwa akipewa kiasi cha paundi milioni 2 kwa mwaka katika klabu hiyo ambayo imemaliza katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
Tuesday, June 4, 2013
DJOKOVIC ATINGA ROBO FAINALI YA FRENCH OPEN PAMOJA NA MAJONZI.
NYOTA wa tenisi anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani, Novak Djokovic amerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kufiwa na kocha wake wa zamani na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya wazi ya Ufaransa kwa kumfunga Philipp Kohlschreiber wa Ujarumani. Djokovic raia wa Serbia alimfunga Mjerumani huyo kwa 4-6 6-3 6-4 6-4 na kutinga hatua hiyo ambapo sasa atakwaana na Tommy Haas kutafuta nafasi ya kucheza nusu fainali. Mara baada ya mchezo huo Djokovic alielezea masikitiko yake kwa kumpoteza kocha wake wa zamani Jelena Gencic aliyefariki akiwa na miaka 77 huko nchini kwao Jumapili iliyopita. Mwanamama huyo ndiye aliyemtambulisha Djokovic katika ulimwengu wa tenisi wakati akiwa na miaka sita ambapo nyota huyo amemuelezea kama mama yake wa pili kutokana na mafunzo aliyompatia na kumfanya kuwa mchezaji nyota duniani.
RONALDO ATASTAAFU AKIWA MADRID - PEREZ.
RAIS wa wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ana mategemeo kuwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo atabakia Santiago Bernabeu katika kipindi chote cha maisha yake ya soka. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno, mapema mwaka jana alidokeza kuwa hakuwa anafurahia maisha ya Madrid na toka wakati huko amekuwa akihusishwa na mpango wa kurejea Manchester United pamoja na Paris Saint-Germain-PSG. Lakini Perez amedai kuwa atafanya kila awezalo ili nyota huyo aweze kuwa na furaha katika klabu hiyo na kumalizika muda wake wa kucheza soka akiwa hapo. Perez pia aluzungumzia mustakabali ya mshambuliaji mwingine Gonzalo Higuain na kudai kuwa hakuna yoyote aliyemwambia kwamba mchezaji huyo ataondoka kwani klabu hiyo haijamuweka sokoni katika kipindi cha usajili. Ambapo aliongeza kuwa kama mchezaji mwenyewe ndio anataka kuondoka basi klabu itakayomhitaji itatakiwa kuwalipa lakini mpaka sasa ahkuna klabu yoyote iliyojitokeza kumtaka mchezaji huyo.
NATAKA KUMSAIDIA MESSI AENDELEE KUNG'ARA ZAIDI ULAYA - NEYMAR.
MSHAMBULIAJI nyota mpya wa klabu ya Barcelona, Neymar amesema anataka kumsadia nyota wa klabu hiyo Lionel Messi aendelee kung’ara duniani baada ya kukamilisha taratibu zote za uhamisho wake kutoka klabu ya Santos. Neymar mwenye umri wa miaka alikamilisha uhamisho wake wenye thamani ya euro million 57 na kumaliza utata wa miezi kadhaa juu ya mstakabali wa nyota huyo. Akihojiwa mara baada ya kutambulishwa rasmi mbele ya maelfu ya mashabiki katika uwanja wa Camp Nou, Neymar amesema anataka kuisaidia timu kwasababu Barcelona ni zaidi ya klabu na pia anataka kumsadia Messi aendelee kung’ara zaidi. Nyota huyo aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni ndoto zake kucheza katika klabu ambayo inahesabika kama mojawapo ya klabu bora duniani huku akizungukwa na wachezaji nyota. Neymar anaondoka Santos akiwa ameshinda Kombe la Brazil mwaka 2010, Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini mwaka 2011 huku akiwa amefunga mabao 138 katika mechi 229 alizocheza akiwa katika klabu hiyo.
Monday, June 3, 2013
MOURINHO ATUA RASMI CHELSEA KWA MKATABA WA MIAKA MINNE.
KLABU ya Chelsea imemteua tena Jose Mourinho kuwa meneja wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne. Mourinho ambaye ni raia wa Ureno atachukua nafasi ya Rafael banitez aliyejiunga na Napoli baada ya kuinoa klabu hiyo kwa miezi sita. Hii ni mara ya pili kwa Mourinho kurejea Stamford Brigde kama kocha kocha baada ya kuondoka miaka sita iliyopita. Mourinho ndiye alikuwa chaguo la kwanza la mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich baada ya kuinunua klabu hiyo mwaka 2003 na ndiye kocha pekee kati ya tisa waliopita klabuni hapo kuanzia kipindi hicho aliyeipa mafanikio zaidi.
ANZHI YAITAKA FECAFOOT KUTOMTUMIA ETO'O KATIKA MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA.
KLABU ya Anzhi Makhachkala ya Urusi imeliandikia Shirikisho la Soka nchini Cameroon-Fecafoot kuwataka kutomtumia mshambualiaji nyota wa timu hiyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Samuel Eto’o katika mechi zao ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Daktari wa viungo wa klabu hiyo Stijn Vendenbroucke amesema nyota huyo aliumia msuli katika fainali ya Kombe Urusi Jumamosi iliyopita na alitaka apumzike kwa wiki chache kabla ya kurejea uwanjani tena. Eto’o atasafiri kuelekea Cameroon leo ili aweze kufanyiwa vipimo vingine na daktari wa timu ya taifa ambaye ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho wa kama nyota huyo atakuwa fiti kucheza mechi dhidi ya Togo Juni 9 na nyingine dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC wiki moja baadae. Cameroon kwasasa wanaongoza kundi I wakiwa na alama sita, alama moja zaidi ya Libya wakati DRC wana alama nne na Togoalama moja.
USINGIZI WAMKOSESHA KULIONA BAO LA MWANAE.
WINGA wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Mark Chamberlain alikosa kuliona bao alilofunga mwanae Alex Oxlade-Chamberlain katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo na Brazil uliofanyika katika Uwanja wa Maracana. Baba wa nyota huyo amesema aliukosa kuuutizama mchezo huo kwasababu alikuwa akitaka kumuwahisha uwanja wa ndege alfajiri mama yake Oxlade-Chamberlain hivyo kulala mapema. Chamberlain ambaye alikuwepo katika kikosi cha Uingereza kilichoshinda mchezo dhidi ya Brazil mwaka 1984, amesema ametumiwa ujumbe mfupi na watu wengi wakidai kuwa kijana wake huyo alifunga bao zuri sana. Nyota huyo anayecheza katika klabu ya Arsenal alisawazisha bao kwa timu yake kwenye dakika ya 67, zikiwa zimepita dakika tano toka aingie akitokea benchi la wachezaji wa akiba.
Subscribe to:
Posts (Atom)






