RAIS wa klabu ya Lazio, Claudio Lotito amedai kupokea zaidi ya vitisho 50 vya kifo toka klabu hiyo imuuze kiungo wake Hernanes kwenda Inter Milan siku ya mwisho kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa. Lotito aliwaambia waandishi wa habari kuwa amepokea simu kati ya 50 mpaka 80 kutoka kwa mashabiki ambao walimpataka aondoke Lazio na kutoa vitisho vya kumuua. Rais huyo amesema kwasasa anaishi chini ya ulinzi mkali na kuwa mashabiki ni sehemu ya klabu lakini sasa anadhani kuwa wmaevuka mipaka. Mbali na vitisho hivyo vya hivi karibuni lakini pia Lotito amesema amewahi kupokea vitisho Septemba mwaka jana baada ya klabu hiyo kushindwa kumsajili beki wa Uturuki Burak Yilmaz kutoka klabu ya Galatasaray. Lotito amesema mashabiki wanapaswa waelewe kuwa hakuna kitu wangeweza kufanya ili kuzuia Hernanes ambaye ni raia wa Brazil kuondoka kwenda Milan.
Tuesday, February 4, 2014
CHELSEA HAINA MPANGO NA UBINGWA WA LIGI KUU - MOURINHO.
MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amepuuzia madai kwamba kikosi chake ndio kinachopewa nafasi ya kunyakuwa taji la Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kuigaragaza Manchester City kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Etihad jana usiku. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Mourinho amesema kwasasa anatengeneza kikosi kwa ajili ya msimu ujao hivyo taji la ligi haliko katika mipango yake kwasasa ingawa wakifanikiwa kulichukua itakuwa ni hatua nzuri. Mourinho pia alikisifu kikosi chake kwa kucheza mchezo mzuri na pia kutengeneza nafasi nyingi ambazo zingeweza kumaliza mchezo huo mapema kulinganisha na wapinzania wao. Hii ni mara ya kwanza kwa City kushindwa kufunga bao wakiwa nyumbani toka walipotoka sare ya 0-0 na Birmingham City Novemba 2010.
KINNEAR WA NEWCASTLE AJIUZULU WADHIFA WAKE.
MKURUGENZI wa michezo wa klabu ya Newcastle United Joe Kinnear amejiuzulu wadhifa wake huo baada ya kuutumikia kwa kipindi cha nane. Kinnear mwenye umri wa miaka 67 alikuwa ndio bosi wa kocha Alan Pardew kwenye masuala ya utawala huku akitoa kwa mmiliki kuhusiana na masuala yote ya timu hiyo. Newcastle ilishindwa kusajili mchezaji yoyote wakati timu ikiwa chini ya Kinnear na Pardew amekataa kumuunga mkono kufuatia kipigo cha maba 3-0 walichopata kutoka kwa Sunderland Jumamosi iliyopita. Akihojiwa Pardew amesema kama angepewa nafasi ya kusajili pengine mambo yangekuwa tofauti lakini hakuwa na mamlaka hayo. Baada ya Newcastle kumuuza Yohan Cabaye kwenda Paris Saint-Germain kwa paundi milioni 19, timu hiyo ilishindwa kutafuta mbadala wake katika siku mbili za usajili wa dirisha dogo zilziobakia.
MAYWEATHER ATAKA MASHABIKI WAKE WAMCHAGULIE BONDIA WA KUZICHAPA NAE.
BINGWA wa dunia wa ngumi za uzito wa kati Floyd Mayweather amewataka mashabiki wake kuamua kama pambano lake litakalofuata liwe dhidi ya Amir Khan au Marcos Maidana. Khan ambaye ni raia wa Uingereza Desemba mwaka jana alisaini mkataba ambao unamuweka katika nafasi ya kupigana na Mayweather ambaye mpaka sasa hajawahi kupigwa na bondia yoyote. Khan mwenye umri wa miaka 27 ameshinda mapambano 28 kati ya 31 aliyopigana wakati Maidana ambaye ni raia wa Argentina yeye ameshinda mapambano 35 kati ya 38 aliyopigana. Mayweather mwenye umri wa miaka 36 alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwataka mashabiki wake kumchagulia bondia wa kupigana naye katika pambano litakalofuata kati ya Khan au Maidana.
Monday, February 3, 2014
MSHABIKI MBARONI KWA MADAI YA TIKETI FEKI.
MSHABIKI mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kukutwa na tiketi bandia kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Mbeya City iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Matei Cosmas (28) ambaye ni mkazi wa Buza Njiapanda Kitunda, Dar es Salaam amefunguliwa jalada namba CHA/IR/900/2014 kwenye Kituo cha Polisi Chang’ombe akidaiwa kupatikana na tiketi bandia. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo asubuhi (Februari 3 mwaka huu) limeamkia Kituo cha Polisi Chang’ombe kusaini hati ya maelezo dhidi ya mtuhumiwa. Ni imani ya Shirikisho kuwa mtuhumiwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchini. Tunatoa mwito kwa washabiki wa mpira wa miguu kuepuka kununua tiketi kutoka mikononi mwa watu, kwani kufanya hivyo ni kosa. Tiketi zinauzwa kwenye sehemu maalumu zenye chapa ya TFF.
RAIS WA TFF ATEMBELEA RUANGWA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametembelea Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Katika ziara hiyo aliyoifanya jana (Februari 2 mwaka huu), pia alikuwa mgeni rasmi mechi ya kugombea Kombe la Majaliwa kati ya Hull City na Mbagala City, na kuahidi kuwa TFF itaandaa kozi za awali za ukocha na uamuzi kwa Wilaya ya Ruangwa.
RAIS WA TFF ATEMBELEA RUANGWA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametembelea Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Katika ziara hiyo aliyoifanya jana (Februari 2 mwaka huu), pia alikuwa mgeni rasmi mechi ya kugombea Kombe la Majaliwa kati ya Hull City na Mbagala City, na kuahidi kuwa TFF itaandaa kozi za awali za ukocha na uamuzi kwa Wilaya ya Ruangwa.
ANCELOTTI AMKOSOA MWAMUZI KUHUSU KADI NYEKUNDU YA RONALDO.
MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amekosoa uamuzi uliotolewa na mwamuzi Miguel Ayza wa kumpatia Cristiano Ronaldo kadi nyekundi ya moja kwa moja wakati timu hiyo ikitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Athletic Bilbao jana usiku. Ronaldo alitolewa nje baada ya mabishano kati yake na wachezaji wa Bilbao, Carlos Gurpegui na Ander Iturraspe katika dakika ya 76 ya mchezo lakini Ancelotti anadhani nyota huyo wa kimataifa wa Ureno hakustahili kutolewa kwa tukio hilo. Akihojiwa Ancelotti amesema ni ngumu kwake kusema kwasababu hakuwa karibu na eneo la tukio lakini picha zinaonyesha kuwa tukio hilo halikuwa baya kiasi cha kutoka kadi nyekundu. Ancelotti pia alikiri kuwa kadi nyekundu kwa Ronaldo ilisababisha kikosi chake kipate wakati mgumu lakini ameridhishwa na matokeo ya sare waliyopata pamoja na kushindwa kuwapita mahasimu wao Barcelona waliochapwa mabao 3-2 na Valencia Jumamosi. Kwasasa Madrid wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa La Liga wakipitwa kwa alama tatu na vinara Atletico Madrid.
Subscribe to:
Posts (Atom)






