MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger ametaka kanuni za kutoa kibali cha kufanya kazi kwa ajili ya wachezaji ambao hawamo kwenye Umoja wa Ulaya zifutwe. Wenger anajaribu kumsajili Gabriel Paulista kutoka Villarreal ambaye atahitaji kibali cha uidhinisho toka nchini kwake sababu hajawahi kulitumikia taifa lake. Kocha huyo amekosoa mpango wa mapendekezo ya kupunguza idadi ya wachezaji toka mashirikisho yasiyo ya Umoja wa Ulaya katika Ligi Kuu Uingereza msimu ujao. Kwasasa kibali cha kufanyia kazi kwa nchi zisizo Umoja wa Ulaya kinahitaji mchezaji awe anatoka katika nchi zilizo ndani ya nafasi 70 za viwango vya FIFA na awe amecheza kwa asilimia 75 katika timu ya taifa ndani ya miaka miwili. Chama cha Soka cha Uingereza kinataka kupunguza idadi ya wachezaji wasiokua wenyeji wa Umoja wa Ulaya kufikia asilimia 50 kwenye ligi. Lakini Wenger anadhani kuondoa kanuni itakuwa bora zaidi kwa ajili ya wachezaji chipukizi wa nchi hiyo. Wenger amesema alitaka kumsajili winga wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria wakati akiwa na umri wa miaka 17 lakini kibali cha kazi kikaleta shida.

Friday, January 23, 2015
BENITEZ ASISITIZA KUBAKIA NAPOLI.
MENEJA wa Napoli Rafa Benitez amesisitiza anafurahi kuwepo katika klabu hiyo na anatarajia kufanya mazungumzo kuhusiana na mustakabali mwishoni mwa msimu huu. Mkataba wa sasa kocha huyo na klabu hiyo unatarajiwa kumalizika Juni mwaka huu. Benitez amesema anatarajia kuzungumzia mustakabali wake na rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis mwanzoni mwa kiangazi huku akidai kuwa hajafanya mazungumzo na klabu yeyote. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anafurahi kuinoa Napoli ndio maana anataka kuendelea kubakia hapo na kuiwezesha timu hiyo kunyakuwa mataji.
AUBAMEYANGA AKIRI KUCHEZA CHINI YA KIWANGO.
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang amekiri kuwa chini ya kiwango katika mchezo waliofugwa dhidi ya Congo Brazzaville juzi. Baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wao wa ufunguzi Jumamosi iliyopita, Gabon walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo lakini mambo yalibadilika baada ya Congo kuwafunga bao 1-0. Aubemeyang ambaye alikuwa nyota katika mchezo wao wa kwanza amekiri kuwa hakuwa katika kiwango chake katika mchezo dhidi ya Congo. Nyota huyo anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani amesema walishindwa kutengeza na kutumia mchezo wao hali ambayo iliwafanya kuiga mchezo wa wapinzani jambo lililokuwa baya kwao. Hata hivyo, Aubameyang anaamini wanaweza kuamka katika mchezo wa mwisho na kuhakikisha wanaibuka na ushindi. Gabon itamaliza mechi zake za makundi kwa kucheza na wenyeji Guinea ya Ikweta Jumapili hii.
RONALDO ANAWEZA KUITUMIKIA MADRID KWA MIAKA 10 ZAIDI - MENDES.
WAKALA wa mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amedai kuwa mteja wake huo bado ana miaka 10 zaidi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno mapema mwezi huu alinyakuwa tuzo yake ya tatu ya Ballon d’Or ikiwa ni ya pili toka atue Santiago Bernabeu lakini hivi karibuni amekaririwa akidai kuwa anafikiria kuhamia nchini Brazil kabla ya kutundika daruga zake. Hata hivyo wakala huyo Jorge Mendes ana uhakika Ronaldo atamalizia soka lake akiwa Madrid huku akidai kuwa nyota huyo bado ana miaka 10 zaidi ya kucheza soka katika kiwango cha juu. Mendes amesema ana uhakika Ronaldo atastaafu akiwa Madrid na umri wa miaka 38 au 39 kwasababu bado ana miaka mingi ya kucheza soka. Mendes aliendelea kudai kuwa kikubwa kinachomfanya kuamini kwamba anaweza kufikia huko ni kutokana na jinsi anavyojiweka fiti mpaka kuwa mfano kwa wachezaji wenzake.
Thursday, January 22, 2015
TETESI ZA USAJILI ULAYA: CHELSEA YAMTENGEA PAUNDI MILIONI 40 WINGA WA FIORENTINA, UNITED NAO WAINGIA KATIKA MBIO ZA KUMUWANIA PAULISTA.
KATIKA habari za tetesi za usajili klabu ya Chelsea inaripotiwa kuanza mazungumzo na Fiorentina kwa ajili ya kumsajili winga wa kimataifa wa Colombia Juan Cuadrado mwenye umri wa miaka 26 katika kipindi hiki cha usajili. Vinara hao wa Ligi Kuu wanadaiwa kuongeza nguvu katika harakati zao za kumsajili winga huyo baada ya ofa yao ya paundi milioni 20.6 kukataliwa jana. Chelsea wanadaiwa kutaka kufidia gharama za Cuadrado kwa mauzo ya winga Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 22 au mshambuliaji Andre Schurrle mwenye umri wa miaka 24. Schurrle anaripotiwa kujipanga kurejea katika klabu ya Wolfsburg ya nchini kwake Ujerumani. Mbali na hayo Chelsea pia inahusishwa na taarifa za kutenga kitita cha paundi milioni 40 kwa ajili ya kumuwania kiungo wa Juventus Paul Pogba mwenye umri wa miaka 21 ambaye aliondoka Manchester United mwaka 2012. Klabu ya Valencia nayo imejipanga kuizidi kete Liverpool kwa kusajili kiungo wa Manchester James Milner mwenye umri wa miaka 26. Arsenal wanatarajiwa kuchuana na Manchester United katika kuwania kumsajili beki wa kati wa Villarreal Gabriel Paulista ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 16.
MAN UNITED YAKWEA MPAKA NAFASI YA PILI KATIKA ORODHA YA VILABU TAJIRI DUNIANI.
KLABU ya Manchester United imerejea tena katika orodha za juu za vilabu tajiri ambapo sasa wamepaa mpaka nafasi ya pili katika klabu zinazoingiza fedha nyingi wakiwa nyuma ya vinara ya Real Madrid. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa leo, mapato ya vilabu 20 tajiri vilivyomo katika orodha hiyo yamepanda mpaka kufikia euro bilioni 6.79 kwa msimu wa 2013-2014 ikiwa ni ongezeko la euro milioni 873 ukilinganisha na misimu ya nyuma. Mabingwa Ulaya Madrid wao wanaongoza orodha hiyo kwa miaka 10 mfululizo lakini Ligi Kuu Uingereza imeendelea kuonyesha kwamba wana nguvu za kiuchumi kwa nane kutoka huko kuingia katika orodha hiyo. Pamoja na msimu mbovu waliokuwa nao msimu uliopita United bado imepaa kwa nafasi mbili na kuwa klabu ya pili duniani inayoingiza fedha nyingi zaidi duniani kutokana na mapato ya euro milioni 565. Klabu za Manchester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool zote zimechomoza katika orodha ya 10 bora wakati Tottenham Hotspurs wao wapo katika nafasi ya 20 bora sambamba na Newcastle United na Everton wanaongia katika orodha hiyo kwa mara ya kwanza. Barcelona waliokuwa wakishika nafasi ya pili safari hii wameanguka mpaka nafasi ya nne kwa kuingiza mapato ya euro milioni 528 huku mabingwa Bayern Munich wao wakiwa nafasi ya tatu kwa kuingiza euro milioni milioni 531. Paris Saint-Germain wako katika nafasi ya tano wakiingiza kiasi cha milioni 517 wakifuatiwa na Manchester City katika nafasi ya sita wakiliongiza euro milioni 452, nafasi ya ssaba inakwenda kwa Chelsea waliongiza euro milioni 423. Wengine ni Arsenal katika nafasi ya nane waliongiza euro milioni 412.3 wakifuatiwa na Liverpool katika nafasi ya tisa waliongiza kiasi cha euro milioni 334 na Juventus ndio wanaofunga orodha ya 10 bora kwa kuingiza euro milioni 279.4. Kwa upande wa timu nyingine za Uingereza zilizopo katika orodha ya 20 bora, Spurs wao wako katika nafasi ya 12 kwa kuingiza kiasi cha euro milioni 104.9 wakati Newcastle waliongiza euro milioni 169.4 na Everton euro milioni 157.3 wako katika nafasi ya 19 na 20.
RONALDO AZIKATA MAINI MAN UNITED NA CHELSEA KWA KUDAI HANA MPANGO WA KWENDA UINGEREZA.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amewanyong’onyesha mashabiki wa klabu za Manchester United na Chelsea baada ya kudai kuwa amepanga kwenda kumalizia soka lake nchini Brazil mara baada ya kuondoka Hispania. Wadau wengi walikuwa akitabiri kuwa Ronaldo anaweza kurejea United mara baada ya kumaliza mkataba wake Madrid lakini mwenyewe amekaririwa na gazeti la Metro akidai kutimkia Brazil katika klabu za Corinthians au Flamengo. Ronaldo ambaye ameitumikia United kwa muda wa miaka sita kabla ya kuhamia Madrid mwaka 2009 amekuwa akieleza mapenzi yake kwa mashabiki wa timu hiyo huku akihusihwa pia na kwenda Chelsea. Ronaldo alikaririwa akidai kuwa Corinthians na Flamengo ni vilabu vikubwa ambavyo anaweza kucheza katika mojawapo kwani amekuwa na marafiki wengi sana Brazil.
Subscribe to:
Posts (Atom)