BEKI wa zamani wa Manchester United, Nemanja Vidic anaripotiwa kutamani kurejea Ligi Kuu na tayari ameshapewa ofa ya kujiunga na Aston Villa. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 aliondoka Inter Milan mapema wiki hii baada ya mkataba kusitishwa kwa maelewano. Villa ambao wamepania kuimarisha safu yao ya ulinzi kipindi hiki cha usajili wa Januari, wana hofu ya kuwakosa nyota wa Bordeaux Lamine Sane na Joleon Lescott ambaye anafikiria kwenda China na Marekani. Vidic pia amehusishwa na tetesi za kutakiwa katika klabu za Marekani lakini mwenyewe anapendelea zaidi kurudi Uingereza na Villa wanaangalia uwezo wake kwanza kabla ya kumchukua.
Thursday, January 21, 2016
WEST BROM YATAKA PAUNDI MILIONI 30 KWA BERAHINO.
Wednesday, January 20, 2016
TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.
MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal yuko tayari kuondoka katika timu hiyo majira ya kiangazi ikiwa ni mwa mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa miaka mitatu, sababu kubwa ikiwa ni shinikizo na shutuma anazopambana nazo.
Chanzo: Daily Mirror
KLABU ya West Ham United, inajipanga kumuwania mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge. West Ham imefikia hatua hiyo kufuatia meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kutishwa na majeruhi ya Sturridge hivyo kuwa tayari kupokea kitita cha paundi milioni 18.
Chanzo: Brentwood Gazette
MENEJA wa Watford Quique Sanchez Flores ameamua kuacha kumuwania Emmanuel Adebayor na kuifanya Crystal Palace kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo ambaye yuko huru kwasasa baada ya kuachwa na Tottenham Hotspurs.
Chanzo: Evening Standard
MENEJA wa Liverpool Jurgen Klopp ameripotiwa kusisitiza kusajiliwa kwa marc-Andre Ter Stegen ili kuleta ushindani kwa Simon Mignolet ambapo klabu hiyo inedaiwa kutoa ofa ya paundi milioni 10.8 lakini Barcelona wao wanataka paundi milioni 23 kwa kipa huyo.
Chanzo: Don Balon
KLABU ya Tottenham Hotspurs inajiandaa kumuwania kiungo wa Coventry James Maddison na kama wakifanikiwa watamuacha kwa mkopo katika klabu hiyo ya daraja la kwanza mpaka mwishoni mwa msimu huu.
Chanzo: The Independent
KLABU ya Liverpool ilikaribia kumsajili Dele Alli kutoka timu ya MK Dons kiangazi mwaka jana lakini walichemka kwa kumpa ofa ya mshahara wa paundi 4,000 kwa wiki nyota huyo ambaye kwasasa anang’aa katika klabu ya Tottenham Hotspurs.
Chanzo: Daily Mail
WAKALA wa Ezequiel Lavezzi, Alessandro Moggi ametua jijini London leo kufanya mazungumzo na Chelsea, lakini haijajulikana kama wanazungumza kuhusu uhamisho wa mshambuliaji kwenda PSG kipindi hiki cha Januari au kiangazi.
Chanzo: Sky Sport Italia
KLABU ya Chelsea inadaiwa kutaka kusajili wachezaji watatu ambao ni Alexandre Pato, Aymen Abdennour na Alex Teixeira kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili majira ya kiangazi huku wakiwaruhusu Papy Djilobodji na Charly Musonda kuondoka kwa mkopo.
Chanzo: Daily Mail
KLABU ya Liverpool inaripotiwa kuwepo katika mazungumzo na Juventus kwa ajili ya kumsajili Alvaro Morata kwa kitita cha euro milioni 58.1, wakati Arsenal na Manchester United nazo pia zikimmezea mate nyota huyo.
Chanzo: Gazzetta dello Sport

POLISI MATATANI KWA KUWEKA PASSPORT YA MESSI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII HUKO DUBAI.
POLISI mmoja wa Dubai anakabiliwa na kifungo cha miezi sita jela na faini ya euro 124,000 kwa kutuma picha za video za pasi ya kusafiria ya mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi, katika mitandao ya kijamii. Polisi huyo wa Uwanja wa Ndege aliyejulikana kwa jina la J.J anatuhumiwa na waendesha mashitaka kwa kuingilia mfumo wa mawasiliano na alikiri kosa la kuvunja Sheria ya Mtandao lakini aliomba kusamehewa. Messi alitua Dubai mwishoni mwa Desemba kuhudhuria sherehe za tuzo ya Globe Soccer ambao alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka na polisi huyo aliomba kama anaweza kupiga picha na nyota huyo lakini ilishindikana kwasababu alikuwa amechoka. Polisi huyo mwenye umri wa miaka 26, baadae aliingia katika chumba cha mawasiliano na kuirekodi video wakati Messi akionyesha pasi yake ya kusafiria kwa wana usalama kabla ya kuituma katika mtandao wa Snapchat.
MAN UNITED YAAMBIWA KUTOA PAUNDI MILIONI 65 KAMA WANAMTAKA LUKAKU.
KLABU ya Manchester United italazimika kulipa kitita cha paundi milioni 65 kama watahitaji kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku ambaye yuko katika kiwango bora msimu huu. Lukaku ambaye alisajiliwa Everton akitokea Liverpool kwa kitita cha paundi milioni 28, amefunga mabao 19 katika mshindano yote msimu huu hivyo kuzivutia klabu kubwa zikiwemo Real Madrid, Paris Saint-Germain, Chelsea na Manchester City. Lakini United ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumsajili kutokana na nia yao ya kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ambayo imeonekana kuwa butu msimu huu. United imekuwa ikimfuatilia Lukaku kwa karibu msimu huu lakini Everton wamepania kuendelea kubakia na nyota huyo.
ASHLEY COLE KUTIMKIA MAREKANI.
BEKI wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Ashley Cole amekubali kuhamia klabu ya Los Angeles Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani-MLS baada ya kuondoka AS Roma. Cole mwenye umri wa miaka 35, yuko huru kujiunga na mchezaji mwenzake wa zamani wa Uingereza Steven Gerrard baada ya mkataba wake na Roma kuvunjwa kwa maelewano. Beki huyo wa zamani wa klabu za Arsenal na Chelsea alijiunga na klabu hiyo ya Serie A Julai mwaka 2014 na kufanikiwa kucheza mechi 16. Akiwa ameichezea Uingereza mechi 101, Cole amefanikiwa kunyakuwa mataji matatu ya Ligi Kuu, saba ya Kombe la FA, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na moja la Europa League.
IRAQ YATANGAZA KUMUUNGA MKONO PRINCE ALI KATIKA UCHAGUZI WA FIFA.
CHAMA cha Soka cha Iraq-IFA kimetangaza kumuunga mkono Prince Ali Bin Al Hussein wa Jordan katika kinyang’anyiro cha urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA mwezi ujao. Prince Ali anatarajiwa kupambana na rais wa Shirikisho la Soka la Asia-AFC, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa, kaimu katibu mkuu wa zamani wa FIFA, Jerome Champagne, mwanasiasa na mfanyabiashara wa Afrika Kusini Tokyo Sexwale na katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Gianni Infantino, katika uchaguzi huo wa Februari 26. Rais wa IFA Abdul Khaliq Masood amesema katika taarifa yake iliyotumwa FIFA kuwa wameamua kura ya nchi hiyo itakwenda kwa Prince Ali kwasababu ya mchango wake mkubwa katika maendeleo y soka ya eneo hilo. Hii ni mara ya pili kwa Prince Ali kugombea nafasi hiyo bada ya kushindwa na rais anayeondoka Sepp Blatter katika uchuguzi uliofanyika Mei mwaka jana.
Subscribe to:
Posts (Atom)