BEKI wa Barcelona, Gerard Pique amedai kuwa waamuzi nchini Hispania wanaipendelea Real Madrid baada ya klabu hiyo kuchapwa mabao 2-1 na Athletico Bilbao katika mchezo wa Kombe la Mfalme uliochezwa jana usiku. Barcelona walilalamikia penati mbili moja iliyomhusisha Neymar na nyingine Pique, ambazo zilikataliwa katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza hatua ya timu 16 bora, ingawa baadae wenyeji Bilbao walipoteza wachezaji wawili kwa kadi nyekundu Raul Garcia na Ander Iturraspe. Akihojiwa Pique amesema penati hizo zilikuwa za wazi kabisa lakini anadhani wanajua kwanini wanafanyiwa hivyo. Pique aliendelea kudai kuwa waamuzi wamekuwa wakiwakwamisha kwa kuonyesha upendeleo kwa Madrid akitolea mfano wa mechi yao ya jana dhidi ya Sevilla ambayo walishinda mabao 3-0.
Friday, January 6, 2017
TUZO ZOTE ZA AFRIKA ZILIZOTOLEWA.
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika.
1. Riyad MAHREZ (Algeria & Leicester City) – 361 votes
2. Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon & Borussia Dortmund) – 313 votes
3. Sadio MANE (Senegal & Liverpool) – 186 votes
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika – Ndani ya Afrika
1. Denis ONYANGO (Uganda & Mamelodi Sundowns) – 252 votes
2. Khama BILLIAT (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns) – 228 votes
3. Rainford KALABA (Zambia & TP Mazembe) – 206 votes
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika Wanawake
Asisat OSHOALA (Nigeria & Arsenal Ladies)
Mchezaji Bora wa Mwaka Anayechipukia
Kelechi IHEANACHO (Nigeria & Manchester City)
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Vijana
Alex IWOBI (Nigeria and Arsenal)
Kocha Bora wa Mwaka
Pitso MOSIMANE (Mamelodi Sundowns)
Klabu Bora ya Mwaka
Mamelodi Sundowns
Timu Bora ya Mwaka - Wanaume
Uganda
Timu Bora ya Mwaka - Wanawake
Nigeria
Mwamuzi Bora wa Mwaka
Bakary Papa GASSAMA (Gambia)
Kiongozi Bora wa Soka wa Mwaka
Manuel LOPES NASCIMENTO, President of Guinea Bissau Football Federation
Legend Award
Laurent POKOU - Former player of Cote d’Ivoire
Emilienne MBANGO - Former player of Cameroon
Platinum Award
His Excellency Muhammadu Buhari, President of the Federal Republic of Nigeria
Kikosi Bora Afrika XI
Kipa: Denis ONYANGO (Uganda & Mamelodi Sundowns)
Mabeki: Serge AURIER (Cote d’Ivoire & Paris Saint-Germain), Aymen ABDENNOUR (Tunisia & Valencia), Eric BAILLY (Cote d’Ivoire & Manchester United), Joyce LOMALISA (DR Congo & AS Vita)
Viungo: Khama BILLIAT (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns), Rainford KALABA (Zambia & TP Mazembe), Keegan DOLLY (South Africa & Mamelodi Sundowns),
Washambuliaji: Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon & Borussia Dortmund), Sadio MANE (Senegal & Liverpool), Riyad MAHREZ (Algeria & Leicester City)
Substitutes
Aymen MATHLOUTHI (Tunisia & Etoile du Sahel), Kalidou KOULIBALY (Senegal & Napoli), Salif COULIBALY (Mali & TP Mazembe), Islam SLIMANI (Algeria & Leicester City), Mohamed Salah (Egypt & Roma), Kelechi IHEANACHO (Nigeria & Manchester City), Alex IWOBI (Nigeria and Arsenal)

Thursday, January 5, 2017
TUHUMA ZA RUSHWA ZAMUWEKA HAYATOU KIKAANGONI.
RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika-CAF, Issa Hayatou ameitwa na waendesha mashitaka nchini Misri kwa uchunguzi kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi yake. Mojawapo ya tuhuma zinazomkabili ni ile ya kutoa haki za matangazo kwa michuano mbalimbali ya soka Afrika kwa kampuni ya inayojihusisha na masuala ya habari ya Legardere Sports. Kwa mujibu ya Mamlaka zinazosimamia mashingano mbalimbali nchini Misri, Hayatou anatuhumiwa kwa kutoweka wazi tenda za mashinano hayo kama inavyotakiwa na sheria za nchi hiyo. CAF makao yake makuu yako jijini Cairo, hivyo shughuli zake zozote inabidi zifuate sheria za hapo. Hayatou mwenye umri wa miaka 70, alichaguliwa mwaka 1998 na kwasasa anatumikia muhula wake saba.
EVERTON YANASA KINDA KUTOKA CHARLTON.
KLABU ya Everton imekamilisha rasmi usajili wa paundi milioni 11 wa mshambuliaji chipukizi wa Charlton Athletic, Ademola Lookman. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19 amesaini mkataba wa miaka minne ambao utamalizika Juni mwaka 2021. Lookman amefunga mabao saba katika mechi 25 za mashindano yote alizoichezea klabu hiyo ya daraja la kwanza msimu huu. Akihojiwa mara baada ya usajili huo, Lookman amesema anajisikia furaha kuwa mchezaji wa Everton kwani mapema aliposikia kuwa klabu hiyo inamuhitaji alijua kuwa hilo ndio sehemu sahihi kwenda.
HULL CITY WAMCHUKUA KOCHA WA ZAMANI WA OLIMPIAKOS.
MENEJA wa zamani wa Olympiakos, Marco Silva amethibitishwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Hull City. Meneja huyo mwenye umri wa miaka 39 raia wa Ureno, amesaini mkataba wa mpaka mwishoni mwa msimu na klabu hiyo yenye maskani yake katika Uwanja wa KCOM. Silva anachukua nafasi ya Mike Phelan aliyetimuliwa juzi kufuatia timu hiyo kuburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu. Silva aliondoka Olympiakos kiangazi mwaka jana na alikuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na klabu Championship ikiwemo Wolves na Nottingham Forest. Kibarua chake cha kwanza kitakuwa ni katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la FA dhidi ya Swansea City Jumamosi hii.
COQUELIN NJE MWEZI.
KIUNGO wa Arsenal, Francis Coquelin anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki nne baada ya kuumia msuli wa paja wakati wa mchezo wa Ligi Kuu waliotoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Bournemouth juzi. Kuumia kwa kiungo huyo kunamuacha meneja Arsene Wenger kuwa na upungufu ya wachezaji wa viungo wa kati kufuatia kukosekana kwa Santi Cazorla anayeuguza majeruhi ya kifundo cha mguu na Mohamed Elneny aliyeitwa Misri kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika. Viungo pekee wa kati alionao kwasasa ni Aaron Ramsey na Granit Xhaka. Akiongea na wanahabari mapema leo Wenger alithibitisha taarifa za kumkosa beki huyo kwa kipindi cha mwezi mmoja huku akiongeza kuwa mshambuliaji Danny Welbeck anaweza kurejea tena uwanjani katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la FA dhidi ya Preston North End Jumamosi hii.
SPURS WANAWEZA KUPIGANIA TAJI - CONTE.
MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amesema Tottenham Hotspurs wanaweza kupigania taji la Ligi Kuu baada ya kuwatandika mabao 2-0 na kumaliza utawala wao wa kushinda mechi 13 mfululizo.
Mabao mawili ya kichwa ya Dele Alli yalitosha kuipa Chelsea kipigo cha kwanza toka Septemba na kuwaacha Spurs wakiwa nyuma kwa tofauti ya alama saba katika nafasi ya tatu.
Akihojiwa Conte amesema Spurs ni timu imara ambayo inayoweza kupigania taji msimu huu.
Naye meneja wa Spurs Mauricio Pochettino amesema kikosi chake kinaweza kutoa changamoto kwa vitu vikubwa.
Msimu uliopita Spurs ndio waliokuwa washindani wa karibu wa Leicester City katika mbio za ubingwa kwa kipindi kirefu lakini walijikuta wakiteleza dakika za mwisho na kumaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Arsenal.
Toka kuanza kwa msimu huu Spurs hawajafungwa mchezo wowote nyumbani katika Ligi Kuu na Pochettino anadhani msimamo huo unaweza kuwa muhimu katika mafanikio ya kwenda kileleni.
Subscribe to:
Posts (Atom)