Sunday, December 16, 2012
SITAFANYA MANUNUZI JANUARI - FERGUSON.
MENEJA wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema hatafanya manunuzi yoyote ya mchezaji katika kipindi cha dirisha dogo la usajili baada ya timu yake kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland. Ushindi huo ambao ulitokana na mabao yaliyofungwa na Robin van Persie, Tom Cleverley na Wayne Rooney umeifanya timu hiyo kubakia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya alama sita na mahasimu wao Manchester City ambao wanashika nafasi ya pili. Pia ina maana kuwa United imefanikiwa kushinda mechi zake tano za ligi zilizopita rekodi ambayo inamfanya Ferguson kutohitaji mchezaji mwingine wa kuongeza nguvu katika kipindi cha dirisha dogo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Ferguson ambaye amekuwa akihusishwa na tetesi za kumhitaji winga wa Arsenal Theo Walcott alikanusha taarifa hizo na kudai kuwa kikosi chake kina wachezaji wa kutosha ambao wanaweza kuhakikisha wananyakuwa taji la Ligi Kuu msimu huu.
KHAN AMCHAPA MOLINA.
BONDIA machachari kutoka Uingereza, Amir Khan amefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Carlos Molina baada ya kupoteza mapambano mawili yaliyopita katika pambano lililofanyika jijini Los Angeles, Marekani. Khan mwenye umri wa miaka 26 alipoteza mikanda yake ya WBA na IBF ya uzito mwepesi baada ya kukubali kipigi kutoka kwa Danny Garcia na Lamont Peterson lakini bondia huyo alionekana kuimarika kiwango chake katika pambano dhidi ya Molina ambalo alimlazimisha mpinzani wake huyo kushindwa kuendelea katika raundi ya 10. Bondia huyo aliyekulia jijini Bolton aliwasili katika ukumbi wa Memorial Sports Arena huku akiwa na kumbukumbu ya kupigwa na Garcia ambaye alimgaragaza chini mara tatu katika raundi ya nne ya pambano lao lililofanyika Julai mwaka huu. Kwa ushindi aliopata katika pambano hilo Khan sasa anaweza kuamua kutafuta pambano la maruadiano kati ya Garcia au Peterson.
Friday, December 14, 2012
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
WAKENYA KUCHEZESHA MECHI YA STARS, ZAMBIA
Mwamuzi Sylvester Kirwa kutoka Kenya ndiye atakayechezesha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars na mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kirwa anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) atasaidiwa na Elias Wamalwa na Marwa Range. Waamuzi hao wasaidizi ambao vilevile watatoka Kenya pia wanatambuliwa na FIFA. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini hoteli ya Tansoma, na inafanya mazoezi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake.
MTIBWA SUGAR YAICHAPA TOTO 3-1 KOMBE LA UHAI
Mtibwa Sugar ya Morogoro leo asubuhi (Desemba 14 mwaka huu) imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika mechi ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Juma Luzio alifunga mabao yote matatu (hat trick) katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Alifunga mabao hayo dakika za 44,81 na 88. Hata hivyo, Toto Africans ndiyo walioanza kufunga katika mechi hiyo ya kundi A. Bao hilo katika michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia maji Uhai lilifungwa dakjika ya 22 na Pastol Makula. Nayo Simba imenguruma baada ya kuitandika Mgambo Shooting ya Tanga katika mechi nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Wafungaji kwa washindi walikuwa Ramadhan Mdoe dakika ya 19, Mohamed Salum dakika ya 77 na Ramadhan Singano dakika ya 89. Michuano hiyo inaendelea leo mchana na jioni. Mechi ya Ruvu Shooting na Kagera Sugar iliyokuwa ichezwe mchana Uwanja wa Azam, Chamazi sasa itafanyika saa 10 kamili jioni katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Mechi nyingine za leo ni Coastal Union vs JKT Ruvu (mchana- Karume), African Lyon vs Azam (jioni- Chamazi). Vilevile mechi kati ya JKT Oljoro na Yanga inachezwa leo Uwanja wa Chamazi. Kesho (Desemba 15 mwaka huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea Jumapili kwenye viwanja vyote viwili- Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na Uwanja wa Azam- Chamazi.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA DRFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi (Desemba 12 mwaka huu) hoteli ya Mbezi Garden. Ushindi aliopata Almasi Kasongo aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa DRFA walivyo na imani kwao. TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya DRFA ambayo hivi sasa ina kinara mpya, na kwamba ina changamoto kubwa ya kuhakikisha inaendesha shughuli za DRFA kwa kuzingatia katiba na kanuni. Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA chini ya Juma Simba na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF. Safu mpya ya uongozi wa DRFA inaundwa na Kasongo (Mwenyekiti), Meba Ramadhan (Makamu Mwenyekiti), Msanifu Kondo (Katibu), Muhsin Said (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF), Benny Kisaka (Mwakilishi wa Klabu), Ally Hobe (Mhazini) na wajumbe Mohamed Shabani, Sunday Mwanahewa na Bakari Mapande.
CAF KUFANYA UKAGUZI WA ‘LESENI ZA KLABU’ JANUARI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litatuma ofisa wake nchini mwezi ujao kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwenye klabu za Ligi Kuu ya Tanzania kabla ya kutoa leseni kwa zile ambazo zitakuwa zimekidhi vigezo vilivyowekwa. Ili klabu ishiriki mashindano ya CAF ni lazima iwe na leseni hiyo. Kwa mujibu wa CAF, ofisa huyo atakuwa nchini kuanzia Januari 7 mwakani ambapo atafanya ukaguzi huo hadi Januari 14 mwakani. Mbali ya ukaguzi katika klabu, pia ofisa huyo atakagua viwanja vitakavyotumika katika mashindano yake na hoteli ambazo timu kutoka nje zitakuwa zinafikia kabla ya mechi. Baadhi ya masharti kabla ya klabu kupewa leseni ya CAF ni pamoja na kuwa na ofisi (physical address), uwanja wake wa mazoezi, programu ya maendeleo kwa vijana, sekretarieti ya kuajiriwa, hesabu za fedha zilizokaguliwa (audited accounts) na benchi la ufundi linaloundwa na watu wenye sifa zinazostahili.

LAMPARD AHOFIA CHELSEA KUMTEMA.
KIUNGO wa klabu ya Chelsea Frank Lampard anahofia muda wake kucheza soka katika klabu hiyo umekwisha katika kipindi hiki wakati mkataba wake umebakia miezi sita huku kukiwa hakuna mazungumzo yoyote mpaka hivi sasa. Lampard anataka kuongeza mkataba mwingine na klabu hiyo ambayo ameichezea kwa kipindi cha miaka 12 lakini inaonekana kama Chelsea hawahitaji huduma ya mchezaji huyo kwakuwa hakuna dalili zozote za kuanza mazungumzo juu ya mkataba mpya. Kiungo nyota tayari amehusishwa na taarifa za kwenda katika vilabu vya Los Angeles galaxy ya marekani, Paris Saint-Germain ya Ufaransa na vilabu vingine vya Urusi na China lakini akihojiwa jana usiku amesema kuwa angependa kubakia katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Lampard alijunga na Chelsea mwaka 2001 akitokea katika klabu ya West ham United kwa ada ya paundi milioni 11 na toka kipindi hicho amekuwa tegemeo na sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo inayotoka magharibi mwa jiji la London.
ABRAMOVIC KUFANYA KUFURU KWA FALCAO.
MMILIKI wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovic anajiandaa kumfanya Radamel Falcao kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu hiyo kwa kumpatia mkataba ambao utamuwezesha kuchukua kitita cha paundi milioni 10 kwa mwaka. Chelsea inampa kipaumbele mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia ili iweze kumsajili katika dirisha dogo na bilionea wa Urusi anataka kuhakikisha nyota huyo anatua Stamford Bridge. Klabu hiyo inayotoka magharibi mwa jiji la London inatarajia kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mkataba mnono ambao utamuwezesha kulipwa kiasi cha paundi 200,000 kwa wiki. Malipo hayo ya Falcao yatakuwa yamepita yale anayolipwa Fernando Torres ambaye analipwa paundi 175,000 kwa wiki.
XAVI KUZEEKEA BARCELONA.
KIUNGO wa klabu ya Barcelona, Xavi Hernandez anakaribia kufikia makubaliano ya mkataba mpya ambao unamaanisha ataastaafu kucheza soka akiwa katika klabu hiyo ambayo alijiunga nayo zaidi ya miaka 20 iliyopita. Xavi ambaye atatimiza miaka 33 mwishoni mwa mwezi huu alijunga na shule ya vijana ya Barcelona mwaka 1991 akiwa na umri wa miaka 11 na kuibuka katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Real Mallorca mwaka 1998. Mchezaji anahesabiwa kama mmoja wa viungo wazuri kuwahi kutokea katika ulimwangu wa soka ambapo ameisaidia klabu yake kushinda matahji 20 yakiwemo matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na sita ya La Liga. Pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Hispania ambacho kimekuwa na mafanikio makubwa katika miaka ya hivi karibuni akikisaidia kunyakuwa michuano ya Euro mwaka 2008 na 2012 pamoja na Kombe la Dunia 2010.
NAPAMBANA ILI NIREJEE TENA UWANJANI - ABIDAL.
BEKI wa klabu ya Barcelona, Eric Abidal amesema kuwa atapambana kuhakikisha anarejea uwanjani tena wakati huu akiendelea kupona taratibu baada ya kubadilisha ini. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa aligundulika kuwa na uvimbe katika ini lake mwishoni mwa mwaka 2011 na alifanyiwa uapsuaji mkubwa wa kupandikizwa ini jingine machi mwaka huu na toka kipindi hicho amekuwa akipambana ili kurejea katika afya yake ya kawaida. Abidal amesema madaktari wamemwambia kuwa sio kawaida kwa watu wenye matatizo kama yake kuendelea kuishi hivyo atapambana ili aweze kucheza soka tena lakini kama itashindikana haitakuwa na tatizo atabakia na familia yake. Nyota huyo alitoa kauli hiyo wakati akipokea tuzo ya Prix Pyrenees kwa juhudi zake katika kupambana na maradhi ambayo yalikuwa yakimsumbua ambapo aliwashukuru wote waliokuwa pamoja naye katika mwaka huu ambao anadai ulikuwa mgumu zaidi katika maisha yake.
Subscribe to:
Posts (Atom)