MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester United, Robin van Persie anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kati ya wiki nne mpaka sita kutokana na majeruhi ya mguu aliyopata. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 30 alitolewa nje na machela baada ya kufunga mabao matatu-hat trick katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Olympiakos Jumatano iliyopita. Meneja wa United David Moyes amesema vipimo vya kwanza havikuonyesha ukubwa wa tatizo lakini baada ya kurudiwa tena inaonekana kuwa nyota huyo aliumia kuliko ilivyodhaniwa mara kwanza. Van Persie sasa anatarajiwa kukosa mechi zote za robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.
Saturday, March 22, 2014
KOMBE LA DUNIA 2018 LITACHEZWA URUSI KAMA ILIVYOPANGWA - BLATTER.
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amesema michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itachezwa kama ilivyopangwa nchini Urusi pamoja na mgogoro uliopo kuhusu jimbo la Crimea. Mapema mbunge wa Chama cha Labour, Andy Burnham aliiambia BBC kuwa FIFA inatakiwa kufikiria upya juu uamuzi wake wa kuipa Urusi uenyeji wa michuano hiyo. Lakini akiulizwa kuhusiana na suala hilo Blatter amesema kura zilipigwa kuipa uenyeji Urusi kuandaa michuano hiyo hivyo itafanyika kama ilivyopangwa. Rais wa Urusi Vladimir Putin alisaini mswada wa sheria jana kuhalalisha Urusi kulichukua jimbo hilo kutoka Ukraine. Hatua imekuja na kufuatiwa na vikwazo vipya vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya na Marekani, lakini Blatter haoni kama hatua ya Urusi iliyochukua dhidi ya Crimea kama inaweza kuathiri michuano hiyo.
UFALME WA BARCELONA KUTAWALA SOKA LA HISPANIA UMEKWISHA - VALDANO.
MCHEZAJI na kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid Jorge Valdano anaamini kuwa ufalme wa Barcelona katika Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga unaelekea mwishoni wakati wenzao wakianza kuimarika. Barcelona wameshinda taji la La Liga mara nne katika misimu mitano iliyopita lakini kwasasa wako nyuma ya vinara Madrid kwa alama nne huku kukiwa kumebaki michezo 10 ukiwemo wa kesho. Valdano amesema Madrid ndio wenye nafasi kubwa kushinda mchezo huo wa kesho dhidi ya mahasimu wao Barcelona ambao wanaonekana kama wanaporomoka kiwango. Kocha huyo mwenye umr wa miaka 58 amesema mchezo huo unaipa nafasi Madrid kwa mara ya kwanza baada ya kupita kipindi kirefu. Mbali na kuipa nafasi Madrid, Valdano pia anakiri kikosi alichokuwa nacho kocha Gerardo Martino ni cha aina yake ingawa anadhani timu hiyo haiwezi kuvuna vipaji kama hivyo tena.
CITY YAPATA PIGO AMBALO NI AHUENI KWA MAHASIMU WAO UNITED.
GABRIEL HEINZE ATUNDIKA DARUGA.
MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Argentina, Gabriel Heinze ametangaza kutundika rasmi daruga zake kufuatia kusumbuliwa na mejruhi ya muda mrefu. Beki huyo aliyekuwa akicheza katika klabu ya Newell Odl Boys amekuwa akipambana na majeruhi katika vipindi tofauti kwa miaka kadhaa mpaka kufikia uamuzi huo akiwa na umri wa miaka 35 sasa. Katika taarifa yake ilichapishwa katika mtandao wa klabu hiyo Heinze amesema kwa masikitiko kuwa kama ilivyo kwa kila kitu katika maisha hata ndoto pia zina mwisho wake. Heinze amesema pamoja na kwamba anapenda kuendelea kuitumikia klabu hiyo lakini anadhani mwili wake umekataa kutokana na majeruhi ambayo ymekuwa hayamwishi. Nyota huyo aliushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kipindi chote na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kadri atakavyohitajika. Heinze alianza soka lake kwa katika klabu hiyo kabla ya kutimkia Villadolid ya Hispania huku pia akicheza katika vilabu vya Paris Saint-Germain, Manchester United, Real Madrid, Olympique Marseile na Roma.
Friday, March 21, 2014
YANGA, RHINO KUCHEZA TABORA VPL.
YANGA inaumana na Rhino Rangers katika moja kati ya mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa wikiendi hii katika miji miwili tofauti. Mechi hiyo itafanyika kesho (Machi 22 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora ambapo kiingilio kitakuwa sh. 5,000 kwa jukwaa kuu na sh. 3,000 mzunguko. Nayo JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbeya City katika mechi itakayochezwa kesho Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Jumapili) kwa mechi nne ambapo Simba itacheza na Coastal Union katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Azam itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex. Mechi hizo mbili zitakuwa ‘live’ kupitia Azam Tv. Mechi nyingine za Jumapili ni Mgambo Shooting dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Ruvu Shooting na Ashanti United zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
NAHODHA WA KWANZA WA BRAZIL KUNYANYUA KOMBE LA DUNIA AFARIKI DUNIA.
ALIYEKUWA nahodha wa timu ya taifa ya Brazil iliyonyakuwa taji la Kombe la Dunia mwaka 1958, Bellini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83. Beki huyo alikiongoza kikosi cha Brazil akiwemo Pele aliyekuwa na umri wa miaka 17 kuwagaragaza wenyeji Sweden kwa mabao 5-2 katika mchezo wa fainali na kuifanya nchi hiyo kunyakuwa taji hilo kwa mara ya kwanza. Nguli anapewa heshima kubwa nchini Brazil kwa kuwa nahodha wa kwanza kunyanyua juu Kombe la Dunia. Nguli amefariki kwa kinachohofiwa kuwa shinikizo la damu na maradhi mengine yanayowakuta watu wenye umri mkubwa. Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo, Jose Maria Marin alituma salamu zake za rambirambi kwa familia ya nguli huyo na kumuelezea kama mtu muhimu na kiongozi imara kwa timu ya Brazil.
Subscribe to:
Posts (Atom)






