BEKI wa zamani wa vilabu vya Juventus, AC Milan na Barcelona Gianluca Zambrotta amesema wote Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni wachezaji wa kipekee lakini anaamini Messi ambaye walicheza wote akiwa Barcelona ana kipaji cha ziada kuliko Ronaldo. Zambrotta ambaye amecheza misimu miwili Barcelona kuanzia mwaka 2006 mpaka 2008 amekiri kufahamu mara moja kuwa Messi ana kipaji cha kipekee. Zambrotta amesema alipofika Barcelona mwaka 2006 Messi alikuwa bado mdogo lakini kipaji chake kilikuwa kinajionyesha wazi kwani alikuwa mtu wa kawaida nje ya uwanja lakini pindi aingiapo ndani anabadilika na kuwa mtu mwenye ufanisi wa hali ya juu. Nyota huyo wa zamani aliendelea kudai kuwa pamoja na kwamba wote wana uwezo sawa katika kufunga mabao lakini kwa mawazo bado anadhani Messi ana vitu vua ziada ambavyo vinaweza kubadilisha mchezo wakati wowote kuliko ilivyo kwa Ronaldo.
Monday, September 22, 2014
VAN GAAL AWAANGUSHIA LAWAMA WACHEZAJI.
MENEJA wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal amesema timu yake ilipoteza ushindi wakati Leicester City walipotoka nyuma kwa mabao mawili na kuibuka na ushindi wa kipekee wa mabao 5-3. United walikuwa wanaongoza kwa mabao 3-1 huku kukiwa kumebaki dakika 30 kabla ya mchezo kumaliza lakini penati yenye utata iliyofuingwa na David Nugent ndio ilileta balaa kwa mabeki wa timu hiyo kushindwa kuzia kasi ya Leicester. Akihojiwa Van Gaal amesema sio jambo zuri kwasababu walikuwa tayari wanamiliki mchezo huo na baadae kujikuta wakipoteza ushindi huo kirahisi. Pamoja na penati ya Nugent kuwa na utata lakini Van Gaal amewalaumu wachezaji wake wa safu ya ulinzi kwa kushindwa kuwa makini wakati wa kuokoa hatari katika eneo hilo. Van Gaal amesema hajui kama ilikuwa penati au la lakini jambo la msingi mchezaji mwenyewe anapaswa kutambua eneo alilopo na kuepuka kufanya makosa kama timu.
ZAMA ZA LAMPARD ZIMEKWISHA - MOURINHO.
MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesisitiza kuwa hadithi za upendo za Frank Lampard na klabu hiyo zimekwisha baada ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 kufunga na kuinyima ushindi timu yake hiyo ya zamani dhidi ya Manchester City jana. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Mourinho alikataa kumzungumzia Lampard na kiwango alichoonyesha kwa kudai kuwa mchezaji huyo ni mali ya City kwa alipoamua kwenda kwa wapinzani na hadithi yake iliishia hapo. Mourinho amesema kumzungumzia mchezaji huyo ni jambo ambalo halihitaji kwasasa kwani amekwenda katika timu nyingine na akiwa meneja anatakiwa kuzungumzia kuhusu wachezaji wake. Lampard ambaye ameitumikia Chelsea kwa miaka 13, hakushangilia mara baada ya kufunga bao hilo la kusawazisha.
PELLEGRINI AIPONDA CHELSEA KWA KUPAKI BASI.
MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini ameiponda Chelsea kwa kucheza kama timu ndogo wakati timu hizo zilipotoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa katika Uwanja wa Etihad jana. Nyota wa Chelsea Andre Schurrle ndio aliyeifungia Chelsea baop la kuongoza kabla ya Feank Lampard aliyetokea benchi kuisawazishia Cioty bao hilo. Akihojiwa Pellegrini amesema wapinzani wao Chelsea walicheza kama timu ndogo kwani muda mwingi walikuwa wakijihami badala ya kucheza mpira. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa sio jambo zuri kamwe wakati timu moja inapofanya kazi ya kuzuia kwani kunakuwa hakuna ladha ya soka.
Saturday, September 20, 2014
SAMATTA, ULIMWENGU KIBARUANI LEO.
WASHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu leo watakuwa na kibarua kizito pale klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC itakapomenyana na Entene Setif ya Algeria. Mchezo huo wa nusu fainali ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika itachezwa katika Uwanja wa Setif maarufu kwa jina la Mei 8, 1945. Hii itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kukutana ambapo mara ya kwanza ilikuwa katika mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ambapo Mazembe walifanikiwa kutoa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza huku wakiwatandika Setif kwa mabao 4-2 katika mchezo wa marudiano uliochezwa jijini Lubumbashi. Setif ilishindwa kufurukuta katika kundi B walilokuwepo baada ya kuburuza mkia, wakati Mazembe waisonga mbele mpaka hatua ya nusu fainali mpaka fainali na baadae kuja kufungwa na CS Sfaxien ya Tunisia kwa jumla ya bao 1-0 na kuibuka bingwa wa michuano hiyo. Mchezo mwingine wa nusu fainali unatarajiwa kuchezwa kesho jijini Kinshasa ambapo AS Vita watakuwa wenyeji wa Sfaxien.
LIGI KUU TANZANIA BARA KUANZA RASMI LEO.
LIGI Kuu Tanzania bara inaanza kutimua vumbi rasmi leo kwa viwanja mbalimbali nchini vikitarajiwa kuwaka moto katika mechi za ufunguzi huku mashabiki wakiwa na hamu kubwa ya kuona jinsi timu zilivyojiandaa kwa ajili ya msimu mpya. Kwa upande wa Dar es Salaam leo mabingwa watetezi Azam FC wao wataanza kampeni zao kwa kuikaribisha Polisi ya Morogoro katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii kwa Yanga. Yanga mabingwa wa Ngao na washindi wa pili wa ligi msimu uliopita wao watakuwa na kibarua kizito pale watawavaa wakata miwa wa Mtibwa Sugar Jamhuri mkoano Morogoro, wakati Mbeya City washindi wa tatu wa ligi wao wakianzia nyumbani katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kwa kuikaribisha JKT Ruvu. Timu za Stand United ya Shinyanga na Ndanda FC ya Mtwara ambazo zote zimepanda daraja msimu huu nazo zitakuwa dimbani kuonyeshana kazi katika Uwanja wa Kambarage, Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar katika Uwanja wa Mkwakwani huku Ruvu Shooting wakiwakaribisha Tanzania Prison katika Uwanja wa Mabatini.
Friday, September 19, 2014
MOURINHO AANZA KUCHONGA.
MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mpourinho amedai kuwa hana tatizo na kikosi chake kujipa motisha wenyewe kabla ya kuivaa Manchester City Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa katika Uwanja wa Etihad. Meneja huyo raia wa Ureno ameshuhudia kikosi chake kikishinda kila mchezo wa Ligi Kuu msimu huu lakini waligonga mwamba kwa Schalke Jumatano wakati walipolazimishwa sare. Hata hivyo, Mourinho anaamini Chelsea ina uwezo wa kuwafunga mahasimu wao hao katika mbio za ubingwa na kusisitiza wanajiamini kwa uwezo wao kuelekea katika mchezo huo. Mourinho mwenye umri wa miaka 51 amesema siku zote ni jambo zuri kucheza dhidi ya timu kubwa kwani inafanya kazi yake kuwa rahisi. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wanaiheshimu City kwasababu wanastahili lakini wao pia wanajiamini kufanya vyema katika mchezo huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)






