
Tuesday, January 17, 2012
HATIMAYE RONALDINHO ASAFIRI NA FLAMENGO.
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Flamengo ya Brazil Ronaldinho amesafiri na kikosi hicho Jumatatu kuelekea nchini Bolivia kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini. Ronaldinho amesafiri na timu hiyo pmoja na vitisho alivyotoa vya kutosafiri na kikosi hicho endapo hatalipwa mshahara wake wa miezi mitano ambao hajalipwa na klabu hiyo. Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona na AC Milan amekuwa sehemu ya wachezaji 16 wanaounda kikosi hicho waliosafiri kwa ya mchezo wa ugenini dhidi ya timu ya Real Potosi. Wakala wa Ronaldinho Roberto Assis ambaye pia ni kaka yake amesema wamefikia makubaliano na klabu hiyo pamoja na kampuni ambayo inalipa sehemu ya mshahara wa mchezo kuwa watalipa fedha hizo zinakadiriwa kufikia kiasi cha euri milioni mbili Jumatano.
WE'RE FINALLY READ-AFCONS CO HOSTS.
WENYEJI wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu nchi za Equatorial Guinea na Gabon wana ukakika licha ya wasiwasi uliokuwepo na baada ya uwekezaji mkubwa waliofanya katika viwanja, barabara na mahoteli sasa wako tayari kwa ajili michuano hiyo mikubwa barani Afrika. Wakati wanakubaliana kuandaa michuano hiyo nchi hizo mbili ambazo zina utajiri mkubwa wa mafuta katika ukanda wa Magharibi mwa Afrika wamepitia katika magumu mengi mpaka kufikia hatua hiyo ya mwishoni. Equatorial Guinea imejenga kiwanja kimoja kipya chenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 uwanja ambao umejengwa katika jiji la Malabo wakati uwanja uliopo katika jiji la Bata ambao ndio utakuwa wa ufunguzi wa michuano hiyo Jumamosi una uwezo wa kumeza watu 38,000. Gharama za viwanja vyote viwili zinakadiriwa kufikia kiasi cha euro milioni 75 huku asilimia 85 ya barabara za nchi hiyo zikiwa zimefanyiwa marekebisho na zingine kujengwa upya huku mahoteli katika jiji la Malabo nazo zikiwa zimefanyiwa marekebisho na nyingine zikiwa ni mpya. Wakati Equatorial Guinea ikifanya hayo hali ilikuwa tofauti kwa Gabon ambao wao walichelewa ujenzi kwani tokea mwaka 2006 walipopewa dhamana ya kuandaa michuano hiyo mpaka 2009 hakuna chochote kilichofanyika kwa ajili ya maandalizi hayo. Ilikuwa ni wakati Rais wan chi hiyo Ali Bongo Ondimba alipoingia madarakani kazi rasmi za ujenzi zilipoanza huku kamati ya maandalizi ikiingiwa na utata mkubwa baada ya kubadilisha viongozi wake mara tatu. Mwezi Machi mwaka jana Shirikisho la Soka la Afrika-CAF lilikiri kuwa na wasiwasi kutokana na maandalizi yanavyokwenda taratibu na matokeo yake uwanja wa kihistoria wa Omar Bongo umeshindwa kutumika katika michuano hiyo kwakuwa bado uko katika ukarabati. Michezo ambayo ilitakiwa kufanyika jijini Libreville sasa itachezwa katika Uwanja wa Amitie Agonje ambao ulimalizika Novemba mwaka jana wakati ukarabati wa Uwanja wa Franceville ukiwa ndio kwanza umekamilika.
Monday, January 16, 2012
MARADONA ALAZWA DUBAI.
KLABU ya Al Wasl ya Dubai imetangaza kuwa kocha wake mkuu Diego Maradona amelazwa katika Hospitali moja nchini humo baada ya kugundilika kuwa na mawe katika figo yake. Maradona mwenye umri wa miaka 51 alienda hospitalini hapo mapema Jumapili iliyopita kwa ajili uchunguzi na kwasasa amewekwa katika uangalizi ili baadae aweze`kufanyiwa upasuaji kuondoa mawe hayo. Msemaji wa klabu ya Al Wasl amesema kuwa mchezaji huyo alikuwa akijisikia maumivu kabla ya kupelekwa hospitalini hapo ambapo alitarajiwa kufanyiwa upasuaji Jumapili jioni kabla ya kuruhusiwa leo. Klabu hiyo ilitarajiwa kutoa taarifa zaidi kuhusu afya ya Maradona inavyoendelea baadae leo.
MTANDAOWA TWITTER WAMKATISHA MTU MMOJA KWA KUTOA UJUMBE WA KIBAGUZI.
POLISI nchini Uingereza wamemkamata mtu mmoja kufuatia kutuma ujumbe wa kibaguzi katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwalenga wachezaji wawili wa Rangers. Mtu huyo mwenye umri wa miaka 41 ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anashikiliwa na polisi baada ya malalamiko kuwa beki wa Rangers Kyle Bartley na mchezaji mwezie wa timu hiyo Maurice Edu kutumiwa ujumbe huo wakibaguzi kwenye Twitter. Bartley ambaye yuko kwa mkopo kwa mabingwa hao wa nchini Scotland akitokea klabu ya Arsenal aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa amesikitishwa sana na kauli ya huyo mtu na anashangaa kwamba mpaka kipindi hiki bado watu wana mambo kama hayo ila anaamini pilisi watafanya kazi yao. Edu naye aliandika katika ukurasa wake kuwa imekuwa ni siku mbaya kwake kuona kwamba watu wanafikiria kuandika ujumbe wa kibaguzi katika mtandao huo badala ya kupinga vitu hivyo katika karne hii.
BARCA YAJIPANGA KUPINGA KADI YA INIESTA.
MENEJA wa Barcelona Pep Guardiola amefafanua kuwa klabu hiyo inajipanga kukata rufani ili kupinga hatua ya mchezaji wake Andres Iniesta kupewa kadi ya njano katika mchezo baina ya timu na Real Betis ambao walishinda kwa mabao 4-2 katika Uwanja wa Camp Nou. Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alipewa kadi hiyo kwa kujiangusha katika eneo la hatari katika kipindi cha pili cha mchezo huo ingawa hata hivyo ilionekana dhahiri kabisa kwamba beki wa Betis Jefferson Montero alimkwatua. Guardiola akihojiwa baada ya mchezo huo amesema kuwa haikuwa penati kwakuwa mwamuzi hakuona tukio lile vizuri lakini wanatarajia kupinga Iniesta kupewa kadi ya njano. Guardiola pia alikisifia kikosi chake kwa moyo wa kujituma walioonyesha kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu katika mchezo huo.
GHANA YAFURAHISHWA NA UJIO WA ESSIEN.
SHIRIKISHO la Soka nchini Ghana-GFA limesema limefurahishwa kwa hatua ya kiungo wake Michael Essien kurejea uwanjani baada ya kukaa nje kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua. Essien alikuwa nje ya uwanja karibu miezi sita na matokeo yake amekosa fainali zingine za Kombe la Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kuanza Januari 21 mwaka huu huko Gabon na Equatorial Guinea. Rais wa GFA Kwesi Nyantakyi amesema katika taarifa yake kuwa kurudi kwa mchezaji huyo ni jambo kubwa kwa kwa klabu yake ya Chelsea pamoja na nchi yake. Nyantakyi aliendelea kusema kuwa pamoja na kwamba mchezaji huyo atakosa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika lakini wanamuombea kupona huko kumpe changamoto mpya ili hapo baadae aweze kurejea kulitumikia taifa lake.
Subscribe to:
Posts (Atom)