KLABU ya Barcelona imeendeleza wimbi lake la ushindi katika Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga baada ya kufanikiwa kuifunga Granada kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Camp Nou jana usiku.
Timu hiyo ilibidi ifanye kazi ya ziada baada ya Granada kutaka kugawana alama lakini bao la mchezaji Xavi Hernandez alilofunga dakika tatu kabla ya mpira kumalizika liliihakikishia ushindi wa alama zote tatu timu hiyo. Mara baada ya bao hilo Granada walionekana kushindwa kumudu vishindo vya Barcelona waliokuwa wakishambulia kwa kasi lango la wapinzani wao ambapo kabla ya kipenga cha mwisho beki wa timu hiyo alijifunga mwenyewe akiwa katika harakati za kuokoa shuti la chini kwa chini lililopigwa na mshambuliaji nyota wa timu hiyo Lionel Messi. Ushindi huo umeipaisha Barcelona ambao wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 15 katika michezo mitano waliyocheza wakiongeza pengo la tofauti ya alama 11 na mahasimu wao Real Madrid ambao watacheza na Rayo Vallecano baadae leo wakisaka ushindi wa kwanza ugenini.
Sunday, September 23, 2012
Friday, September 21, 2012
FIFA YAIONYA JAMAICA JUU YA SUALA LA KUVAMIA UWANJA MASHABIKI WAKE.
JAMAICA imeonywa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA juu ya suala la kuvamia uwanja kufuatia ushindi wa kushangaza wa mabao 2-1 wa timu hiyo dhidi ya Marekani katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia uliochezwa mwezi huu. Mamia ya mashabiki wenye furaha wa nchi hiyo walikimbia kuvamia uwanja mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa na kwenda kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo baada ya kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Marekani. Katika taarifa yake ambayo imetimwa kwa Shirikisho la Soka la Jamaica-JFF, FIFA imesema kuwa hilo litakuwani onyo la mwisho kwa nchi hiyo kuzuia tukio kama hilo kutotokea tena. Rais wa JFF, Horace Burrell ameahidi kuwa watakuwa makini kuimalisha ulinzi katika michezo itakayokuja ili kuzuia matukio kama hayo kutokea tena. Guatemala, United States na Jamaica wote wana alama saba kutokana na michezo minne waliyocheza katika kundi A amapo Jamaica inakabiliwa na mchezo mwingine dhidi ya Antigua unaotarajiwa kuchezwa Octoba 16 mwaka huu.
DROGBA AFURAHIA MAISHA YA CHINA.
MEXICO KUGOMBANIA NAFASI YA KUANDAA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2026.
![]() |
| Justino Compean. |
Thursday, September 20, 2012
TAARIFA KUTOKA TFF.
KLABU LIGI KUU, WADHAMINI VODACOM KUTETA
Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zimekubaliana kukutana na mdhamini (kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom) kuzungumzia kipengele cha mkataba wa ligi hiyo kinachozuia kampuni nyingine za mawasiliano kudhamini timu zinazocheza Ligi Kuu. Maazimio hayo yalifikiwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika kikao kati ya klabu hizo na Kamati ya Ligi kilichofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wallace Karia. Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura. Maazimio mengine ya kikao hicho ni TFF kuiandikia barua African Lyon ambayo itaipeleka kwa mdhamini wake (Zantel) ikielezea hatua hiyo ili kusimamisha udhamini huo wakati ikisubiri matokeo ya mazungumzo kati ya klabu hizo na mdhamini wa Ligi Kuu juu ya kipengele cha kuzuia washindani wa Vodacom. Katika mkutano huo, watendaji wawili wa Kamati ya Ligi ambayo iko katika kipindi cha mpito kuelekea kuundwa kwa Bodi ya Ligi walitambulishwa kwa klabu hizo. Watendaji hao ni Silas Mwakibinga ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) na Joel Balisidya ambaye ni Ofisa wa Ligi (LO).

SHAKIRA, PIQUE WATEGEMEA MTOTO.
MWANAMUZIKI nyota kutoka Colombia, Shakira amesema kuwa anategemea kupata mtoto wa kwanza na mpenzi wake ambaye ni mcheza soka wa kimataifa wa Hispania, Gerard Pique. Shakira mwenye umri wa miaka 35 aliandika katika mtandao wake kuwa yeye pamoja na Pique wako katika kilele cha furaha wakisubiria kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza na hilo ndio jambo pekee ambalo wanalitilia mkazo kwasasa. Mapema wiki hii mwanamuziki huyo pamoja na nyota mwingine wa R&B Usher Raymond walithibitishwa kuziba nafasi za Christina Aguilera na Cee Lo Green katika msimu wa nne wa mashindano ya kuimba yanayoandaliwa na NBC yanaoitwa The Voice. Shakira alianza kujulikana kimataifa katika muziki wa pop baada ya kuipua wimbo wake uliotamba mwaka 2006 unaoitwa Hips Don’t Lie na alikutana na Pique mwenye umri wa miaka 25 katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.
MAOFISA WA SOKA CAMEROON KUMWANGUKIA ETO'O.
MAOFISA wa soka nchini Cameroon wamegawanyika juu ya ujumbe ambao utasafiri kuelekea nchini Urusi kujaribu kuongea na mshambuliaji nyota na nahodha wa zamani wan chi hiyo Samuel Eto’o kujaribu kubadilisha uamuzi wake wa kuachana na soka la kimataifa. Kufuatia kuteuliwa kwake kuziba nafasi ya aliyekuwa kocha wan chi hiyo Denisi Lavagne, Jean Paul Akono ameweka suala ya kumrejesha mchezaji huyo kama jukumu lake la kwanza kabla timu hiyo haijakabiliwa na mchezo wa pili wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Cape Verde Octoba 13 mwaka huu. Kumekuwa na msuguano wa chini kwa chini kwakuwa baadhi ya maofisa wa wizara ya michezo ya nchi pamoja na wale wa soka wamekuwa wakipinga suala hilo la kwenda kumwangukia mchezaji huyo ili arejee kuitumikia Cameroon. Cameroon iko katika hatari ya kushindwa kufuzu michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Cape Verde katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Praia lakini kabla ya hapo Eto’o alijitoa katika timu hiyo kwa kile alichodai uongozi mbovu wa soka nchini humo.
Subscribe to:
Posts (Atom)