VINARA wa Ligi Kuu nchini Uingereza, klabu ya Arsenal imepata ahueni baada ya winga wao mahiri Theo Walcott kurejea tena katika kikosi cha timu hiyo katika mchezo dhidi ya Southampton utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Emirates. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amepongeza uwepo wa nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza aliyejiunga na klabu hiyo akiwa na miaka 16 mwaka 2006 baada ya kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara msimu huu. Wenger amesema anapomkosa mchezaji kama Walcott huwa inakuwa tatizo katika kikosi chake kutokana na umahiri na umakini wake anakuwa karibu na lango la adui. Hata hivyo Wenger aliendelea kudai kuwa hawezi kumtumia nyota huyo moja kwa moja kwasababu ndio kwanza ametoka kwenye majeruhi hivyo ataangalia wakati unafaa kumtumia kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi.
Friday, November 22, 2013
BURKINA FASO WAFIKISHA MALALAMIKO FIFA.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA, limethibitisha kupata malalamiko kutoka Shirikisho la Soka la Burkina Faso kuhusiana na mchezo wao wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia ambapo nchi hiyo ilifungwa bao 1-0 na Algeria. Maofisa hao wa Burkinabe wameiandikia FIFA kulalamikia baadhi ya maamuzi yaliyofanywa na mwamuzi Badara Diatta wa Senegal wakati wa mchezo huo, maamuzi ambayo yalipelekea kukataliwa kwa bao lao katika kipindi cha kwanza. Shirikisho hilo pia limelalamikia kadi ya njano aliyopewa nahodha wa Algeria Madgid Bougherra wakidai kuwa alistahili kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi nahodha wa Burkinabe Charles Kabore katika eneo la hatari. Uamuzi wa FIFA unatarajiwa kuhusiana na tukio la mchezo huo unatarajiwa kutolewa Desemba 5, siku moja kabla ya ratiba kamili ya Kombe la Dunia.
AYEW KUFANYIWA UPASUAJI.
KLABU ya Olympique Marseille imedai kuwa mshambuliaji wake nyota wa kimataifa wa Ghana Andre Ayew atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili kutokana na majeraha ya mguu yanayomkabili. Ayew alipata majeraha wakati wa mchezo wa mkondo wa pili hatua ya mtoano ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia ambapo Ghana ilifungwa kwa mabao 2-1 na Misri Jumanne. Pamoja na kipigo hicho Ghana ilifuzu michuano hiyo itakayofanyika mwakani kwa jumla ya mabao 7-3 katika mechi mbili walizocheza na Misri. Nyota huyo ambaye anatarajiwa kufanyiwa upasuaji Jumatatu atakosa safari ya kwenda jijini London ambapo Marseille itakwaana na Arsenal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Thursday, November 21, 2013
POULSEN ATAJA 23 WATAKAOIWAKILISHA BARA KATIKA CHALENJI.
KOCHA Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 mwaka huu. Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho mwaka 2010 chini ya Kocha Jan Poulsen, na ambayo imepangwa kundi B katika michuano ya mwaka huu itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos. Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Tanzania Bara ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam). Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam). Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC). Kilimanjaro Stars inatarajia kuondoka Jumatatu (Novemba 25 mwaka huu) kwenda Nairobi kushiriki michuano hiyo itakayoanza Novemba 27 mwaka huu na kumalizika Desemba 13 mwaka huu.
MECHI DHIDI YA STARS, ZIMBABWE YAINGIZA MIL 50/-
Mechi ya kirafiki ya kimataifa ya FIFA Date kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (The Warriors) iliyochezwa juzi (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 50,980,000 kutokana na watazamaji 7,952. Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 7,776,610.17 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 3,682,560. Asilimia 15 ya uwanja sh. 5,928,124, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 7,904,166 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,976,041. Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 17,784,373 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 889,219 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
MECHI DHIDI YA STARS, ZIMBABWE YAINGIZA MIL 50/-
Mechi ya kirafiki ya kimataifa ya FIFA Date kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (The Warriors) iliyochezwa juzi (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 50,980,000 kutokana na watazamaji 7,952. Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 7,776,610.17 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 3,682,560. Asilimia 15 ya uwanja sh. 5,928,124, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 7,904,166 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,976,041. Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 17,784,373 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 889,219 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
BARCELONA KUWAKOSA MESSI NA VALDES MWAKA HUU.
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu nchini Hispania, Barcelona italazimika kucheza mechi zao nane zilizosalia kwa mwaka huu kuanzia mechi ya Jumamosi dhidi ya Granada bila ya mshambuliaji wake mahiri Lionel Messi na golikipa Victor Valdes. Messi yuko kitandani akiuguza msuli wa nyuma ya paja la mguu wake wa kushoto wakati Valdes ambaye amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu naye amechanika msuli wa mguu wake wa kulia. Kama hiyo haitoshi, kuingo mchezeshaji wa timu hiyo Xavi Hernandez naye kuna hati hati ya kuukosa mchezo wa Jumamosi kutokana na majeraha ya msuli wa kigimbi na Jordi Alba naye bado yuko kitandani akijiuguza. Hata hivyo majeruhi hayawezi kuibabaisha klabu hiyo kutokana na historia ya nyuma kwani Valdes na Messi wamewahi kukosekana katika kikosi kwa muda unaofanana mwaka 2007 na timu hiyo kufanikiwa kushinda mechi 13 kati ya 16 walizocheza bila yao.
GUARDIOLA APATA AHUENI BAADA YA BOATENG KUWA FITI TAYARI KWA DORTMUND.
KOCHA wa klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola amepata habari njema kutoka katika meza ya madaktari wa timu hiyo kuelekea katika mchezo wa mwishoni mwa wiki dhidi ya mahasimu wao Borussia Dortmund. Madaktari wa timu hiyo wamemhakikishia kocha huyo kwamba beki wake tegemeo Jerome Boateng anatakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo muhimu wa Bundesliga. Beki huyo wa kati aliumia kisigino wakati akiitumikia Ujerumani katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Uingereza ambao walishinda kwa bao 1-0 na Bayern walikuwa na hofu nyota huyo kukosekana katika mchezo huo wa Jumamosi. Hata Hivyo, Boateng mwenye umri wa miaka 25 alithibitisha kuwa atakuwepo katika mchezo huo utakaopigwa katika Uwanja wa Signal Iduna Park jijini Dortmund. Katika mchezo huo Bayern watakuwa wakisaka ushindi ili kuongeza pengo la alama kufikia nne katika msimamo wa Bundesliga wakati wapinzani wao watakuwa wakipambana ili kuhakikisha wanabakisha pengo la alama moja baina yao.
ALVES AMFAGILIA RONALDO KUCHUKUA BALLON D'OR.
BEKI mahiri wa klabu ya Barcelona, Dani Alves amekiri kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo yuko katika kiwango bora kuliko hasimu wake katika tuzo za Ballon d’Or Lionel Messi na Franck Ribery lakini anafikiri kukosa taji lolote kwa Ronaldo msimu huu kunaweza kumgharimu kuikosa tuzo hiyo. Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa katika kiwango cha juu toka kuanza kwa msimu wa 2013-2014, akiwa amefunga mabao 24 katika mechi 17 alizocheza huku akifunga mabao mengine manne yaliyoiwezesha Ureno kukata tiketi ya michuano ya Kombe la Dunia 2014. Wakati akikiri kiwango kikubwa cha nyota huyo, Alves anaamini kuwa kukosa taji lolote kwa Madrid katika msimu wa 2012-2013 kutamuweka katika nafasi mbaya kwenye tuzo hizo. Alves amesema karata yake inakwenda kwa Messi au Ribery na kama sio Messi basi anayestahili tuzo hiyo ni Ribery kwasababu ameshinda kila na alikuwa mhimili muhimu kwa timu ya Bayern Munich.
Subscribe to:
Posts (Atom)






