MSHAMBULIAJI wa zamani wa AS Roma ya Italia na Ajax Amsterdam ya Uholanzi, Mido ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu yake ya nyumbani ya Zamalek. Mido anachukua mikoba ya kocha Helmi Toulan ambaye alitimuliwa kufuatia sare ya bao 1-1 iliyopata Zamalek dhidi ya Haras El-Hodood katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Misri. Hiyo inakuwa mechi ya nne kwa Zamalek msimu huu ambapo klabu hiyo inashika nafasi ya nne baada ya kushinda mechi mbili kutoa sare moja na kufungwa moja. Mido ambaye anafikisha umri wa miaka 31 Februari mwaka huu anakuwa kocha mdogo zaidi katika historia ya soka nchini hiyo na hana uzoefu wa kutosha wa kufundisha. Nyota huyo ambaye alianza kusakata kabumbu Zamalek mwaka 1999 kabla ya kwenda kucheza Ulaya ameifungia timu ya taifa ya nchi hiyo mabao 19 katika mechi 51 alizocheza.
Wednesday, January 22, 2014
MAN UNITED MBIONI KUMSAJILI JUAN MATA.
KLABU ya Manchester United ina uhakika wa kumnyakua kiungo Juan Mata kutoka Chelsea kwa ada ya paundi milioni 37 mwishoni mwa wiki hii. Mazungumzo kuhusiana na uhamisho wa kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 25 yamefikia pazuri hivyo kuna uwezekano akafanyiwa vipimo vya afya kabla ya mwishoni mwa wiki. Mata amekuwa akitaka kuondoka Chelsea baada ya kushindwa kumshawishi kocha Jose Mourinho msimu huu. United ambao kwasasa wako katika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu wako katika changamoto kubwa ya kifedha kama wakishindwa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao.
NEGREDO KUFANYIWA VIPIMO VYA BEGA LAKE.
KLABU ya Manchester City, inatarajiwa kumfanyia vipimo Alvaro Negredo baada ya mshambuliaji huyo kuumia bega lake katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya West Ham United. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania alianguka vibaya mwishoni baada ya kufunga mabao mawili na kuisadia City kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo huo wa mkondo wa pili. Kocha wa City Manuel Pellegrini alikiri kuwa nyota huyo kuwa katika maumivu makali lakini inabidi wasubiri ili kujua ameumia kiasi gani baada ya kufanyiwa vipimo. Pellegrini pia aliwasifu wachezaji wake kwa kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo kwa kishindo baada ya kuingamiza West Ham kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi za mikondo miwili walizokutana.
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF.
MZUNGUKO WA VPL KUANZA JUMAMOSI
Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza Jumamosi (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi tano katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam, Tanga wakati mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting inahamishiwa uwanja mwingine. Ashanti United itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal Union itacheza na Oljoro JKT katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar. Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na Mgambo Shooting itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex wakati Simba na Rhino Rangers zitaumana kwenye Uwanja wa Taifa. Mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting iliyokuwa ichezwe Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine inahamishiwa uwanja mwingine kwa vile huo bado nyazi zake ambazo zimepangwa hivi karibuni hazijawa tayari kuhimili mechi hiyo. Hivyo Tanzania Prisons inatakiwa kutafuta uwanja mwingine unaokidhi viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya mechi hiyo, na nyingine dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Januari 29 mwaka huu. Pia matumizi ya tiketi za elektroniki yanaanza katika mzunguko huu kwa vile viwanja nane ambavyo tayari vimefungwa vifaa vya tiketi hizo. Vilevile tunakumbusha washabiki wa mpira wa miguu kuwa tiketi za elektroniki haziuzwi viwanjani.
TWIGA STARS KUIVAA ZAMBIA FEB 15 LUSAKA
Tanzania (Twiga Stars) itaivaa Zambia katika mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya michuano ya mchujo ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayofanyika Februari 15 mwaka huu jijini Lusaka. Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Nkoloma kuanzia saa 9 kamili kwa saa za Zambia na itachezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga kutoka Rwanda. Mukansanga atasaidiwa na Wanyarwanda wenzake; Francine Ingabire, Sandrine Murangwa na Angelique Tuyishime. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jackey Gertse kutoka Namibia.
KISHONGOLE, KESSY KUSIMAMIA MECHI ZA CAF
Shrikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Watanzania Alfred Rwiza Kishongole na Lina Kessy kuwa makamishna wa mechi za shirikisho hilo zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 mwaka huu. Kishongole ameteuliwa kusimamia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Cote d’Or ya Shelisheli na Kabuscorp de Palanca ya Angola. Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya mchujo itafanyika Shelisheli na itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa na Abdoul Ohabee Kanoso. Waamuzi wengine ni Basile Alain Rambeloson, Augustin Gabriel Herinirina na Andofetra Avombitana Rakotojaona. Naye Kessy atakuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Rwanda na Kenya itakayochezwa jijini Kigali. Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Cameroon. Mwamuzi wa kati ni Sylvie Abou wakati wasaidizi wake ni Winnie li Koudangbe, Lum Rochelle na Jeanne Ekoumou.

Tuesday, January 21, 2014
MALINZI AELEZEA MIKAKATI YAKE KWA LOWASSA.
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini. Malinzi ameeleza mikakati hiyo ya uongozi wake leo (Januari 20 mwaka huu) wakati alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Amesema uongozi wake umepanga malengo hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu ya kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) kuundwa na wachezaji kutoka katika klabu chache tu. Kwa upande wake Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini yake kwa uongozi mpya wa TFF katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kuimarisha na kuinyayua Tanzania katika ramani ya mpira wa miguu duniani.
CHAN 2014: UGANDA YAFUNGISHWA VIRAGO NA MOROCCO.
WAWAKILISHI pekee wa Afrika Mashariki katika michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani,CHAN timu ya taifa ya Uganda wameaga michuano hiyo baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Morocco katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Cape Town. Uganda walienguliwa kwa kufungwa mabao 3-1 na Morocco katika mchezo mkali wa kundi B ambao kama wangefanikiwa kushinda wangeweza kutinga robo fainali ya michuano hiyo. Katika mchezo mwingine w kundi hilo Burkina Faso nao walifungashwa virago kwa kutandikwa na Zimbabwe kwa bao 1-0. Michuano hiyo inaendelea tena leo ambapo Ethiopia ambao wameshatolewa katika michuano watakamilisha ratiba kwa kuchuana na Ghana katika Uwanja wa Free State, Mangaung huku Congo wakichuana na Libya katika Uwanja wa Peter Mokaba huko Polokwane.
BARCELONA KUUKARABATI UWANJA WA CAMP NOU KWA EURO MILIONI 600.
KLABU ya Barcelona imewasilisha mpango wa matengenezo ya Uwanja wa Camp Nou ambao utagharimu kiasi cha euro milioni 600 na kuwa na uwezo wa kuongeza mashabiki kufika 105,000. Mara ya kwanza Barcelona walikuwa wamefikiria kujenga uwanja mpya katika na eneo la Avenida Diagonal ambalo ni kituo kikubwa cha biashara katika jiji hilo lakini mpango huo ulikwama kutokana na gharama kubwa inayokadiriwa kufikia euro bilioni 1.2. Badala yake mabingwa hao watetezi wa La Liga wameamua kutumia nusu ya fedha hizo kuuukarabati uwanjani wa sasa ambapo utahusisha pia ujenzi wa paa kufunika uwanja huo. Rais wa Barcelona, Sandro Rosell amesema umekuwa uamuzi mgumu kutokana na mipango yote miwili kuvutia lakini wameamua kubakia hapo kwasababu ni sehemu ya historia ya klabu hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)