MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes amedai kuwa kikosi chake kilistahili kuenguliwa katika michuano ya Kombe la Ligi na Sunderland jana. Baada ya kushinda mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili katika Uwanja wa Old Traford timu zililazimika kucheza muda wa nyongeza na baadaye changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kutoka sare kwa mabao 3-3 katika michezo ya mikondo miwili waliyokutana. Katika changamoto ya mikwaju ya penati United walikosa mikwaju minne na kupelekea kutolewa katika michuano hiyo ambapo sasa majirani zao Manchester City watakwaana Sungerland katika mchezo wa fainali utakaochezwa katika Uwanja wa Wembley Machi 12 mwaka huu. Akihojiwa Moyes amesema kikosi chake hakucheza vizuri kustahili kusonga mbele na kuwapongeza Sunderland kuwa walistahili kusonga mbele kutokana na juhudi walizoonyesha.
Thursday, January 23, 2014
MAN UNITED YAMNASA MATA.
KLABU ya Chelsea imekubali ofa ya paundi milioni 37 kwa ajili kumuuza kiungo wao nyota wa kimataifa wa Hispania, Juan Mata kwa klabu ya Manchester United. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 amefanyiwa vipimo vya afya leo kabla ya kukamilisha uhamisho wake. Mata anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu kuitumikia United. Nyota huyo aliaga wachezaji wenzake na viongozi wa Chelsea katika mazoezi ya timu hiyo huko Cobham jana.
AUSTRALIA OPEN 2014: LI NA, CIBULKOVA KUKWAANA FAINALI.
MWANADADA nyota katika tenisi kutoka China, Li Na amefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya wazi ya Australia baada ya kufanikiwa kumchapa chipukizi Euginie Bouchard katika mchezo wa nusu fainali. Li ambaye amepoteza michezo yake yote mitatu ya fainali katika michuano hiyo alifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kumgaragaza Bourchard wa Canada kwa 6-2 6-4. Mwanadada huyo sasa atakwaana na Dominika Cibulkova wa Canada baada ya nyota huyo kumuondosha Agnieszka Radwanska kwa 6-1 6-2 katika nusu fainali nyingine iliyofabyika katika uwanja wa Rod Laver Arena. Wakati nyota watatu wanashika nafasi za juu katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake, Serena Williams, aliyekuwa bingwa mtetezi Victoria Azarenka na maria Sharapova wakiwa wametolewa hiyo itakuwa ni nafasi pekee kwa Li Na kunyakuwa taji hilo katika mchezo wa fainali Ijumaa baada ya kulisotea kwa miaka mitatu mfululizo.
KAMWAGA AUKWAA UKATIBU SIMBA, ASHA MUHAJI OFISA HABARI MPYA.
Wednesday, January 22, 2014
USAJILI WA OKWI YANGA WAZUIWA.
AUSTRALIA OPEN 2014: BINGWA MTETEZI AZARENKA OUT.
BINGWA mtetezi wa michuano ya wazi ya Australia, mwanadada Victoria Azarenka ameng’olewa katika michuano hiyo baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Agnieszka Radwanska katika mchezo wa robo fainali. Katika mchezo huo Azarenka anayeshika nafasi ya pili katika orodha za ubora wa mchezo huo kwa upande wa wanawake alishindwa kutamba mbele ya Radwanska anayeshika nafasi ya tano kwa kufungwa seti 2-1 zenye alama za 6-1 5-7 6-0. Kipigo hicho kinamaliza ubabe wa Azarenka kushinda mechi 18 katika viwanja vya jiji la Melbourne kuanzia mwaka 2012 na kumaanisha kuondolewa kwa nyota wote wanaoshika nafasi ya tatu za juu baada ya Serena Williams na Maria Sharapova kuondolewa mapema. Radwanska sasa atakwaana na Dominika Cibulkova katika mchezo wa nusu fainali baada ya mwanadada huyo kumuondosha Simona Halep katika mchezo war obo fainali.
BINGWA CHAN KUNYAKUWA KITITA CHA DOLA 746,463.
PAMOJA na kuenguliwa katika michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani,CHAN katika hatua ya makundi, timu ya taifa ya Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana haikutoka mikono mitupu baada ya kukabidhiwa kitita cha dola 175,000 kwa kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi lao. Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo imedai kuwa jumla ya fedha zote za zawadi inafikia kiasi cha dola milioni tatu. Bingwa wa michuano hiyo atanyakuwa kitita cha dola 746,463 na mshindi wa pili atachukua kiasi cha 396,270 huku wa tatu na wanne wote wakichukua dola 248,821 kila mmoja. Timu ambazo zitakwamia katika hatua ya robo fainali zitachukua 175,096 huku zile ambazo zimeshika mkia katika kwenye makundi yao zikiambulia dola 92,156 kila moja. Michuano hiyo inayoendelea nchini Afrika Kusini inatarajiwa kufikia tamati yake Februari mosi mwaka huu.
Subscribe to:
Posts (Atom)






