GOLIKIPA wa Manchester United David De Gea anaripotiwa kutaka kuendelea kubakia Old Trafford hata kama Real Madrid watarejea kumuwinda tena mwezi huu. Madrid wanatarajiwa kukata rufani adhabu ya kufungiwa kusajili waliyopewa wiki iliyopita lakini kama ikishindikana hawataweza kusajili mchezaji yeyote mpaka kiangazi mwaka 2017. Hata hivyo, bado wana uwezo wa kusajili katika kipindi hiki cha usajili wa Januari na kuna uwezekano wakaanza tena kumfukuzia De Gea. Usajili wa kipa huyo ulishindikana kidogo majira ya kiangazi mwaka jana kutokana na karatasi muhimu kutowasili kwa wakati. De Gea ambaye amesaini mkataba mpya wa miaka minne na United anadaiwa kuwa kwasasa hatoweza kukubali tena kuondoka Old Trafford.
Wednesday, January 20, 2016
PLATINI KUENDELEA KULAMBA MSHAHARA WA UEFA PAMOJA NA KUFUNGIWA.
SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limedai kuwa bado wanaendelea kumlipa mshahara rais wake aliyefungiwa Michel Platini mpaka itakapoamuliwa vinginevyo. Taarifa hiyo ya UEFA imekuja baada ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA nalo kudai rais aliyefungiwa Sepp Blatter ataendelea kulipwa stahiki zake mpaka atakapochaguliwa rais mpya katika uchaguzi wa Februari 26. Platini na Blatter wote walisimamishwa kwa siku 90 na kamati ya maadili ya FIFA Octoba 8 mwaka jana na baadae kufungiwa kujishughulisha na masuala ya michezo kwa miaka nane mwezi uliopita. Adhabu ya wawili hao imekuja kufuatia malipo ya dola milioni mbili aliyopewa Platini kutoka kwa Blatter mwaka 2011 kufuatia kazi za soka zilizofanyika miaka nane iliyopita. Msemaji wa UEFA alithjibitisha Platini kuendelea kulipwa stahiki zake na ataendelea kulipwa mpaka utakavyoamuliwa vinginevyo.
SINA MPANGO WA KUONDOKA MAN CITY - BONY.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ivory Coast, Wilfried Bony amedai kuwa hakuna ukweli wowote juu ya tetesi za yeye kutaka kuondoka Manchester City. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, alihoji sababu za uamuzi wa meneja wake Manuel Pellegrini kumuacha katika kikosi chake Desemba mwaka jana na toka wakati huyo amekuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kurejea Swansea City. Hata hivyo akihopjiwa Bony amekanusha taarifa hizo na kudai kuwa anafurahia kuwepo City kwani ni moja ya klabu kubwa nchini Uingereza. Bony alijiunga na City kwa kitita cha paundi milioni 28 na kupewa mkataba wa miaka minne na nusu Januari mwaka jana. Nyota huyo amefunga mabao nane katika mechi 23 alizocheza msimu huu lakini amekuwa akitumika kama mchezaji wa akiba toka mshambuliaji kiongozi Sergio Aguero aliporejea kutoka katika majeruhi Desemba.
INFANTINO AANZA KAMPENI ZA URAIS FIFA.
KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Gianni Infantino amesema Shirikisho la Soka Duniani-FIFA linapaswa kuandaa michuano ya Kombe la Dunia katika bara badala nchi moja au mbili. Kauli hiyo ya Infatino imekuja wakati akianza kampeni zake katika kinyang’anyiro cha urais wa FIFA ambao uchaguzi wake unatarajiwa kufanyika mwezi ujao. Infatino ameahidi michuano mikubwa ya Kombe la Dunia, mageuzi kufuatia kashfa iliyolikumba shirikisho hilo na fedha zaidi kwa nchi wanachama, kama akichaguliwa kuiongoza FIFA katika uchaguzi wa Februari 26 mwaka huu. Infatino ambaye amekuwa akifanya kazi chini rais wa UEFA aliyesimamishwa Michel Platini kwa miaka saba iliyopita amesema Kombe la Dunia kuongezwa na kufikia nchi 40 badala ya 32 za hivi sasa. Mgombea huyo amesema FIFA inapaswa kuangalia uwezekano wa kutanua michuano ya Kombe la Dunia badala ya kufanyika katika nchi moja au mbili iweze kufanyika katika bara zima husika ili kutoa nafasi kwa nchi nyingi zaidi kupata heshima na kunufaika kwa kuwa wenyeji.
Monday, January 18, 2016
TETESI ZA USAJILI ZILIZOJIRI HUKO MAJUU.
KLABU ya Manchester United imeripotiwa kuwa wanaweza kumsajili mtoto wa nguli wa zamani wa klabu hiyo Peter Schmeichel aitwaye Kasper kama David De Gea atatimkia Real Madrid majira ya kiangazi.
Chanzo: The Sun
KUFUATIA kuanza msimu kwa kusuasua, Chelsea inaweza kuwakosa nyota wake kadhaa majira ya kiangazi wakiwemo Eden Hazard, Diego Costa, Oscar na Thibaut Courtois.
Chanzo: The Sun
KUFUATIA tetesi za Neymar kufikiria kuondoka Camp Nou baada ya kutumbukizwa katika sakata la usajili wake wakati akitokea Santos, klabu ya Barcelona inajaribu kutafuta mbadala wake kama akiondoka na kuna uwezekano wa kuanza kumuwania Eden Hazard wa Chelsea.
Chanzo: Buzz Sport
KLABU ya Swansea City ina matumaini ya kukamilisha usajili wa Scott Sinclair na mshambuliaji wa AS Roma Seydou Doumbia katika kipindi hiki cha Januari.
Chanzo: The Daily Mail
KLABU ya Newcastle United imeruhusiwa na mmiliki wake Mike Ashley kutumia kiasi cha paundi milioni 100 kipindi hiki cha usajili wa Januari ambapo wamepanga kumuwania Saido Berahino kabla ya kumfukuzia Andros Townsend kutoka Tottenham Hotspurs.
Chanzo: The Daily Mail
KLABU ya Arsenal inajipanga kumuwania mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata katika kipindi ambacho Real Madrid watakuwa wakitumikia adhabu yao ya kufungiwa kusajili, kufuatia tetesi za klabu hiyo kutaka kumrejesha nyota huyo Santiago Bernabeu.
Chanzo: The Sun
Chanzo: The Sun
KUFUATIA kuanza msimu kwa kusuasua, Chelsea inaweza kuwakosa nyota wake kadhaa majira ya kiangazi wakiwemo Eden Hazard, Diego Costa, Oscar na Thibaut Courtois.
Chanzo: The Sun
KUFUATIA tetesi za Neymar kufikiria kuondoka Camp Nou baada ya kutumbukizwa katika sakata la usajili wake wakati akitokea Santos, klabu ya Barcelona inajaribu kutafuta mbadala wake kama akiondoka na kuna uwezekano wa kuanza kumuwania Eden Hazard wa Chelsea.
Chanzo: Buzz Sport
KLABU ya Swansea City ina matumaini ya kukamilisha usajili wa Scott Sinclair na mshambuliaji wa AS Roma Seydou Doumbia katika kipindi hiki cha Januari.
Chanzo: The Daily Mail
KLABU ya Newcastle United imeruhusiwa na mmiliki wake Mike Ashley kutumia kiasi cha paundi milioni 100 kipindi hiki cha usajili wa Januari ambapo wamepanga kumuwania Saido Berahino kabla ya kumfukuzia Andros Townsend kutoka Tottenham Hotspurs.
Chanzo: The Daily Mail
KLABU ya Arsenal inajipanga kumuwania mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata katika kipindi ambacho Real Madrid watakuwa wakitumikia adhabu yao ya kufungiwa kusajili, kufuatia tetesi za klabu hiyo kutaka kumrejesha nyota huyo Santiago Bernabeu.
Chanzo: The Sun
RONALDO AKIRI KUWA NA MAHUSIANO MAZURI NA MESSI.
MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesisitiza kuwa sasa wana mahusiano mazuri na Lionel Messi na kutania kuwa bado anasubiri malipo yake kwa kutoa huduma ya ukalimani wakati tuzo za Ballon d’ Or. Wawili hao wamekuwa mahasimu wakubwa katika tuzo hizo kwani katika kipindi cha miaka nane iliyopita ni wao ndio wamezitawala. Lakini akihojiwa mara baada ya Madrid kushinda mabao 5-1 dhidi ya Sporting Gijon, nyota huyo wa kimataifa wa Ureno amesisitiza kuwa kwasasa wana mahusiano mazuri na nyota huyo wa Barcelona. Ronaldo amesema wamekuwa karibu zaidi na wamekuwa wakifurahia uhusiano wao mzuri kulinganisha na miaka ya nyuma. Messi na Ronaldo walipanda jukwaani pamoja ambamba na Neymar katika sherehe za tuzo ya Ballon d’Or jijini Zurich na nyota huyo wa zamani wa Manchester United mebainisha kuwa ilibidi awaokoe nyota hao wa Barcelona. Ronaldo amesema wakati wakiwa juu ya jukwaa sio Neymar wala Messi ambaye anaweza kuzungumza kiingereza hivyo alibidi awe mkalimani wao na kutani kuwa alizungumza nao baadae na kuwaomba wamlipe.
UNITED YAMUWANIA SANCHEZ.
KLABU ya Manchester United, imeripotiwa kumuwania chipukizi wa Benfica, Renato Sanchez. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18, amekuwa akionyesha kiwango cha juu toka alipoibuka katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo na sasa amekuwa akifuatiliwa na vilabu kadhaa barani Ulaya vikiwemo Newcastle United, Swansea City na Aston Villa. Taarifa zaidi zinadai kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye ana mkataba unaomalizika mwaka 2020 ana thamani ya paundi milioni 58.8 kwa klabu itakayomuhitaji. Pamoja na hayo United inatajwa kumuwania ingawa haikuwekwa wazi kama watamuhitaji kipindi cha Januari au Kiangazi.
Subscribe to:
Posts (Atom)






