KLABU ya Borussia Dortmund imedai mapema leo kuwa hakuna makubaliano yeyote yaliyofikiwa kwa ajili ya uhamisho wa Ousmane Dembele kwenda Barcelona. Kauli hiyo ya Dortmund inakuja kufuatia taarifa kutoka nchini Ujerumani kudai kuwa tayari makubaliano baina ya pande hizo kwa ajili ya Dembele yamekamilika. Akizungumza na wanahabari, msemaji wa Dortmund amesema wamewapa muda Barcelona hivyo kuna kitu kinaweza kikatokea au kisitokee pia. Taarifa zingine zinadai kuwa Barcelona imekubali kutoa kitita cha euro milioni 120 hivuo kumfanya kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi duniani baada ya Neymar.
Friday, August 25, 2017
Monday, August 21, 2017
BARCELONA KUMGEUKIA DI MARIA WAKIMSHINDWA COUTINHO
KLABU ya Barcelona inatarajiwa kugeukia kwa Angel Di Maria kama wakishindwa kumsajili Philippe Coutinho kutoka Liverpool. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Catalan zimedai kuwa nafasi ya Barcelona kumsajili kiungo huyo wa Brazil imekuwa finyu hivyo kuna uwezekano klabu hiyo ikaamua kuachana naye. Kutokana na hilo Barcelona sasa inaweza kuhamishia nguvu zao kwa Di Maria ili waimarishe kikosi chao. Katika hatua nyingine, Afisa mkuu wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke amedai kuwa nafasi ya Ousmane Dembele kujiunga na Barcelona ni chini ya asilimia 50. Watzke aliwaambia wanahabari kuwa kama Barcelona wanamtaka Osmane lazima walipe ada wanayotaka kwakuwa mchezaji huyo bado ana mkataba wa miaka minne.
ARSENAL HUENDA IKAMUUZA MUSTAFI
KLABU ya Arsenal inadaiwa kukataa ya mkopo kutoka Inter Milan kwa ajili ya beki wake wa kimataifa wa Ujerumani Shkodran Mustafi wiki iliyopita. Hata hivyo taarifa zinadai kuwa Arsenal wanaweza kukubali kumuuza beki huyo kama Inter wataweza kutoa kiasi cha milioni 35 ambacho walilipa wakati walimnyakuwa kutoka Valencia kiangazi mwaka jana. Mustafi amekuwa akipata kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal lakini amekuwa akipata tabu kidogo kuelewana na wachezaji wenzake hatua ambayo inaweza kupelekea suala la kuuzwa liwezekane. Kama Arsenal ikiamua kumuuza nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, italazimika kutafuta mbadala wake ili kuimarisha safu yao ya ulinzi.
WEST BROM WAIKATIA RUFANI KADI NYEKUNDU YA ROBSON-KANU
KLABU ya West Bromwich Albion imekata rufani dhidi ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa Hal Robson-Kanu katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa Ligi Kuu jana. Mshambuliaji huyo alitolewa nje dakika za mwishoni kufuatia kumchezea hovyo beki wa Burnley Matthew Lowton. Robson-Kanu ndiye aliyefunga bao pekee kwenye mchezo huo na kuifanya West Brom kuanza vyema mechi zao mbili za mwanzo za ligi. Taarifa ya West Brom imedai kuwa watatuma malalamiko yao kutokana na uamuzi huo kwenda Shirikisho la Soka la Uingereza-FA.
NEYMAR AWASHAMBULIA VIONGOZI WA BARCELONA
MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain-PSG, Neymar amewaponda wakurugenzi wa klabu yake ya zamani na kudai kuwa Barcelona inastahili viongozi bora zaidi yao. Akizungumza na wanahabari mara baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 6-2 waliopata PSG dhidi ya Toulouse, Neymar amesema viongozi wa Barcelona waliopo madarakani hawastahili kuwepo hapo. Neymar aliandelea kudai kuwa amekaa Barcelona kwa miaka minne na amekuwa na furaha wakati wote lakini sio kwa viongozi wa klabu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amesema Barcelona inastahili uongozi bora zaidi na dunia nzima inafahamu hilo.
Friday, August 18, 2017
LIVERPOOL YAKATAA OFA YA TATU YA BARCELONA KWA COUTINHO
KLABU ya Liverpool imekataa ofa ya tatu kutoka Barcelona inayoamikika kufikia paundi milioni 114 kwa ajili ya Philippe Coutinho. Wiki iliyopita Liverpool walikataa ofa ya paundi milioni 90 kutoka kwa klabu hiyo ya La Liga ambapo baadaye nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 alituma maombi ya kuondoka. Coutinho amekosa mechi mbili za ufunguzi za Liverpool msimu huu kutokana na majeruhi ya mgongo, lakini klabu hiyo imeshaweka wazi nia yake kutotaka kumuuza kiungo huyo. Pamoja na kauli hiyo ya Liverpool, Barcelona bado wamekuwa wakidai kuwa wanakaribia kunasa saini ya kiungo huyo.
COSTA AENDELEA KUTOA POVU SAKATA LAKE NA CHELSEA
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Hispania, Diego Costa amesema Chelsea wanataka kiasi ambacho Atletico Madrid hawataweza kukitoa kwa ajili ya kumalisha usajili wake wa kurejea kwenye klabu yake hiyo ya zamani. Conte mwenye umri wa miaka 28 bado yuko nchini Brazil baada ya kutumia ujumbe mfupi Juni mwaka huu na meneja Antonio Conte akimwambia kuwa hatakuwepo katika mipango yake msimu huu. Chelsea walimsajili Costa kutoka Atletico kwa kitita cha paundi milioni 32 Julai mwaka 2014. Akizungumza na wanahabari huko Brasil, Costa amesema wakati alipokwenda Chelsea walilipa kiasi kidogo kulinganisha na wanachopewa hivi sasa. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa anaona kama Chelsea wanamkomoa kwa kudai kiasi kikubwa cha fedha ili Atletico washindwe kumsajili jambo ambalo anaona sio sawa kwakuwa klabu hiyo imeshaweka wazi kuwa hawamuhitaji.
Subscribe to:
Posts (Atom)






